Labda tunahitaji mwongozo wa “Mzee Kifimbo Cheza.”
Kama wewe ni mfuatiliaji wa kampeni za uchaguzi, huwezi kuwa umepitwa na mjadala huu wa Dr. Slaa “kupora” mke wa mtu. Lakini baada ya kusoma sehemu mbalimbali juu ya hili suala, nimekuja kugundua vitu vikuu viwili. Kitu cha kwanza, hatujui Kiswahili, pamoja ya kuwa hii ni lugha yetu ya taifa. Pili, ni mwamko wetu katika masuala ya udaku, kitu ambacho si kigeni miongoni mwetu.
Mambo haya mawili yanatosha kuakisi taswira ya jamii yetu, kuwa ni jamii ya aina gani. Pamoja na kuwa tunaweza kuangalia haya mambo mawili kwa haraka haraka bila kufikiria mara mbili, lakini kuna siri kubwa iliyojificha. Tuanze na hili la lugha, kabla ya kugusia suala la mapenzi yetu na mambo ya udaku.
Lugha ni nyenzo muhimu sana katika jamii ye yote ile, na jamii ya watu wenye akili timamu hilo linafahamika. Kwani lugha hutunza mila na desturi zetu, historia yetu, huonesha ukuaji wa jamii, mwenendo wa jamii na mambo mengineo. Hivyo utunzaji wa lugha ni jambo la muhimu, pamoja na kuiheshimu.
Leo hii Kiswahili, kama Kiingereza, kimekua kwa uzuri na ubaya. Ukuaji wa lugha umechangiwa na vitu mbalimbali, kama teknolojia, mabadiliko ya maisha na kadhalika. Kwa mfano kwenye katuni hii, tunaweza kuona ni jinsi gani teknolojia ya sms ilivyobadili utumiaji wetu wa maneno na lugha kwa ujumla.
Utumiaji wa lugha wa namna hii unaweza kuangaliwa au kutafsiriwa kama ushahidi wa ongezeko la umomokaji wa maadili. Pia, kuonesha ni jinsi gani jamii yetu ilivyobadilika haraka — kutoka kuwa jamii makini mpaka jamii inayochukulia mambo kirahi-rahisi. Ukweli huu usichukuliwe kama ni sifa, bali fedheha kubwa.
Sasa tukirudi kwenye matumizi ya lugha, na leo nitajadili matumizi ya maneno haya mawili, kuporwa na kuiba au kuibiwa. Nimeona nijadili kwani yametumika sana siku mbili hizi kwenye vyombo vya habari mbalimbali. Hofu yangu ni kuwa wengi wetu hatujui matumizi fasaha ya maneno hayo; labda yametumika makusudi, ili kuamsha hisia badala ya fikra. Pamoja na kuchochea udaku badala ya busara.
Ndugu Daniel Mahimbo, amelalamika kuwa “ameporwa” mke na mgombea urais wa Chadema, huku wengine wakitumia neno “kuiba”. Lakini je, neno “ameporwa” au “kupora” ni sahihi? Uelewa wangu mdogo wa neno kuporwa au kupora linahusihwa na uwizi, hivyo huweza kuamsha hisia za kifedhuli kirahisi na haraka. Na hilo ni kweli, kwani leo hii tunaona mawazo mengi ya kifedhuli katika mijadala mbalimbali kuhusiana na hili suala.
Pili, mtu ukiporwa, inamaana umeibiwa, na kwa kawaida katika taratibu za kijamii, unatakiwa kupeleka hilo suala polisi. Hapo hapo inaleta picha ya unyang’anyi, tena wa kutumia nguvu. Lakini, je, hilo ndilo lililotokea kwenye hili tukio?
Pia, mtu kawaida unaporwa mali yako, kwa maana ya kitu, lakini unaposema umeporwa mke, hiyo inaleta hisia ya kuwa mke ni mali yako. Sasa mjadala huo unaweza kutupeleka kwenye mambo mazito ya kijinsia, hilo ningeomba tujadili siku nyingine tena.
Tatu, kuiba kwa kawaida ni tendo ambalo mtendewa hufanyiwa bila kujua. Sasa, je, ndugu Mahimbo hakujua kuwa mke wake haishi nyumbani kwao tangia mwezi wa tatu? Kama hivyo ndivyo ilivyo, nadhani na yeye inabidi atazamwe alikuwa mume wa aina gani. Pia na kama alikuwa baba wa aina gani, kama alikuwa anajali familia yake, au alikuwa na tabia kama za wanaume wengi ambao hutelekeza familia zao kilolela-holela.
Tatizo langu kuu juu ya habari hii ni ukosefu wa umakini. Kivipi?
Lugha za kirahisi-rahisi zikitumika kwenye vyombo vya udaku, inaeleweka, kwani lengo hasa ni kutumia lugha ambazo zitaamsha hisia na sio fikra. Vyombo hivyo hutengeneza pesa kwa kutumia lugha na picha kucheza na watu kisaikolojia.
Lakini vyombo vya habari visivyo vya udaku vinapotumia lugha nyepesi-nyepesi unabidi upatwe na wasiwasi juu ya mustakabali wa jamii yetu na huko tunapoelekea. Wasiwasi wangu zaidi ni kuwa taaluma ya uandishi wa habari imeanza kuingiliwa na mamluki, na hadhi yake imeanza kupotea kwa kasi inayotisha.
Maneno fasaha yangetumika yangesaidia kutupa usahihi wa suala hili, na majadiliano ya kijinga yasingekuwa mengi. Kwani matumizi sahihi ya lugha huziba mianya ya uwezekano wa mawazo tata au ya kijinga kupenya na kutuathiri sisi zote. Hii si kwa habari hii tu, ipo mifano mingi.
Kwa mfano, sote tunajua kuwa Mheshimiwa Lowassa hakustahafu, bali alijiuzulu. Lakini kila atokeapo kwenye chombo cha habari, yeye huitwa Waziri Mkuu mstahafu. Kwanini? Neno kustahafu huficha ukweli wa hali halisi na kupotosha mantiki, na hata kulaghai historia ya kilichotokea kwa kizazi kijacho.
Hapo hapo, neno kustahafu humlinda mhusika na kunyamazisha watu ambao wangependa kuuliza maswali juu ya kitendo cha kujiuzulu. Kujiuzulu huleta picha ya kuwa kuna dhuluma fulani ilitokea, lakini neno kustahafu huhusishwa na busara. Hapo tunazidi kuona nguvu ya lugha jinsi ilivyo nyenzo muhimu sana katika jamii; si tu kama chombo cha kutuwezesha kuwasiliana peke yake.
Lakini kabla sijamalizia na aya ya mwisho, nimejaribu kujiuliza: Kwanini jamii yetu ina mwamko mkubwa wa mambo ya udaku? Je, hii ni ishara kuwa umakini wetu ndio huo unatutupa mkono? Je, utandwazi ndio wa kulaumu?
Lakini labda ya kutokana na maisha kuwa magumu, watu wanatumia habari za udaku kupunguza misongo ya maisha. Pia inawezekana habari nyingi kuhusu jamii zetu ni habari za kusikitisha au kuudhi, hivyo watu wamechoka na kuamua kupunguza mawazo na habari za udaku au ‘nyepesi.’ Hii labda inatokana na (ukweli kwamba) watu walio wengi wamepoteza imani ya mabadiliko yanayohitajika kutokea, hivyo kutojali tena. Labda nimekosea kabisa? Sijui.
Mwisho ningependa kuwasihi, jamani tuwe makini na matumizi ya lugha, kwani matumizi yetu ya lugha yanaweza kutujenga au kutubomoa sisi na jamii yetu. Na hata kutuchochea kuwa watu wenye kutumia fikra au kutuhamasisha kuwa watu wajinga. Hili ni dhahiri, kwani tumehamasika kweli-kweli na hili suala la “uporwaji” wa mke, ikichangiwa na lugha inayotumiwa na vyombo vya habari. Bila kutilia maanani kuwa mpaka sasa hatujui ukweli na undani. Lakini baada ya kuona tu maneno, “kuporwa” na “kuiba,” basi tumepandwa na jazba, bila ya kufikiri. Kama jinsi ‘tunapovimba vichwa’ tuitwapo “wananchi wenye hasira kali.” Na kuhalalisha matendo yetu ya kinyama. Hii si ishara nzuri, kwani tukiendekeza hii hali tutakuwa watu wa kuongozwa na hisia na sio fikra; tutafanya mambo mengi kwa papara na sio kwa busara.
The best teachers and schools do not exist where they are needed most. Can work-group computers help?
Wakati tukitafuta suluhisho bora kuhusu tatizo la elimu nchini, baadhi ya washikadau wanafanya majaribio ya kisasa kusaidia ufundishaji bora wa wanafunzi. Sugata Mitra na wenzake wanataka kufahamu je, bila uwepo wa mwalimu wanafunzi wanaweza kujifundisha wenyewe kwa kutumia kompyuta? Endelea kwa kutazama video hii ili ujionee maajabu kuhusu yepi yanawezekana.
Tumepata mwanga kuwa wanafunzi wadogo wanaweza kujifundisha wenyewe, na hasa katika makundi madogomadogo. Ni mambo gani yamekugusa ulipoangalia video hii? Binafsi ninapoangalia vitu kama hivi ninamuwaza mwanafunzi wa kule Kalamazwite, Rukwa au pale Mwembe-makumbi, Unguja na kutamani siku moja naye apate nafasi ya kuunganishwa katika gridi ya utandawazi kwa njia kama hii, ili baadaye naye aweze kuwa na usawa wa kiushindani akilinganishwa na wengine popote duniani. Je, tunaweza kutumia njia kama hii ya kompyuta ili kusaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu? Tujiulize maswali gani kabla ya kudandia project kama ya one-laptop-per-child (OLPC)?
Picha kwa hisani ya www.jamiiforums.com
Niambieni jamani, maana’ke hizi ni mbwembwe au?
Lekchara kaniboa kichizi leo! Yaani nilikuwa nina lekcha moja tu, lakini sikumuelewa prof wala nini. Kichwa kilikuwa kinauma kinoma… Nadhani keroro za jana usiku hazikunisaidia. Kama kawaida, usiku ukiwa mnene, lazima leo nipate gambe tena.
Sina mzuka wa kuongea na mtu — yaani hata kutoa hi kwa waliopendeza siwezi. Kugeuza shingo kuwakagua ninaopishana nao imekuwa adhabu. Jua la utosi linanipiga makonzi, kwahiyo bora nitulie kidogo kwenye internet café kabla ya kwenda maskani.
Baada ya kulipa, kuketi na kuanza kutumia kompyuta, kitu cha kwanza ninachoona mbele yangu ni homepage: Globu ya Jamii. Yaani kampeni mpaka huku? Rangi ya bluu inamezwa na ya kijani! Haiwezekani, labda Ankal ni kada wa CCM! Na kuna watu wanatoa maoni yao; kwa maneno mengine, wanampaka Issa.
Ila hiyo sio shida yangu,naamua kuzama kwa mdogo wake. Yale yaleeee. Huku ni kijani kitupu pia. Mambo gani tena haya?
Hivi, Wabongo wangapi wanatumia mtandao? Hizi kampeni zinalenga kina nani hasa? Wazamiaji na wabeba boksi hawatapiga kura — angalau mwaka huu.
Na leo kila sehemu kuna nyuuuz za Dr Slaa kumnyang’anya mtu mke. Dah, watu wanaongea kama vile wake za watu ni mizigo. Yaani unaweza kumpokonya mtu tu mwandani wake mtaani. Ingekuwa hivyo, sasa hivi mi’ ningekuwa nimeshamuoa Faraja Kotta zamaniiii!
Ngoja nipandishe mzuka kabla ya kwenda nyumbani. Huu ndio muda wa kucheki skillzz zangu za kutumia Google. Maujanja ni kujua key words; na leo najaribu “Ze Utamu arudi.” Kama zali vile, Ze Utamu amerudi kutupangusa! Nabofya link ya kwanza kabisa…
Mambo gani haya? Inanipeleka kwenye hiki kijiwe kinachoboa kinoma.
Ngoja niende kuanza kufaidi weekend… Sh*t! Kumbe leo Jumanne.
Kila mtu anaweza kufanya kitu kusaidia kujenga nchi yetu.
Tarehe 4 Septemba, 2010, Metty Nyang’oro wa Radio Mbao alipata fursa ya kumhoji mjasiriamali Modesta Mahiga kwa kirefu. Ni mahojiano ya kina yanayogusa nyanja mbalimbali nchini Tanzania. Ukiacha suala la ujasiriamali kwa ujumla, Modesta alijadili kwa kirefu mambo yafuatayo:
- Fikra za Watanzania (kwenye suala la kutafuta ajira)
- Juhudi na kuwajibika
- Jinsi ya kuleta mabadiliko nchini
- Kufanya mambo ya ziada kujiendeleza
- Mfumo wa elimu
- Uwekezaji
- Vipaji vya vijana
- Na mambo mengine chungu mzima…
Nakusihi, ukipata muda sikiliza mahojiano haya:
“Tanzania ndani ya miaka 10 (ijayo) itakuja kubadilika… kuwa kitu cha ajabu.”
(w. Englist subtitles) Ujumbe, nasaha, hali halisi; ubunifu, vipaji, taaluma; ubora, umakini na kupenda kazi. Haya ndio matokeo yake.
Nilishawahi kuiweka hii enzi zile wakati tovuti hii ilipokuwa inatembelewa na watu wawili watatu… kwa siku; mimi na mtu mwingine. Ila kuna mtu ameniasa kuianika tena.
Burudika na ujifunze (kama hujawahi kuiona). Kama umeshawahi kuiona, itazame tena!
Music seems to be one of a few languages of the world, but what is really happening behind the scenes to those that speak it?
This past weekend, I had a one-hour set to DJ at an established venue in Dar-es-Salaam. I was supposed to be guest-DJ’ing, but there were a few issues to begin with. Issue number one: It had been planned very spontaneously; as of 4 hours before my set, the owner still did not know I was going onto the booth. He found out eventually. Issue number two: The venue attracted listeners of all styles, but most especially hip-hop and R&B, which brings me to issue number three: I prefer playing house, and although in my lifetime as a DJ I have had to learn (the hard way) that you need to respect your listeners and play along their vibes, I felt like sticking to my preferred genre that night.
So my hour came by, and I went up there, and mixed into the resident DJ’s last track (he was playing BEP’s track with David Guetta, I got a feeling) with a bootleg house remix of Snoop’s Sensual Seduction. That’s about all I got to play, because as soon as I was mixing in Beltek’s Niagara Falls, I saw the owner come up to the resident DJ, motion to him to get me out of there, and within a minute, the resident had slammed on Andre 3000’s Hey Yeah, and I had to gather my CDs and bounce from that booth. The reason? The owner had seen a few people stop dancing. This is the first time I had been ushered out of a set after about 4 minutes of playing. What could I say to the owner? He was just looking out for his clients. And what could I say to his clients? They were just having a good time… well, not during my set, apparently.
Now here’s the thing: I, and other artists in Tanzania that deal with music, need to understand that radio stations control the tastes in this country. Radio is the most proliferated source of media in Tanzania today. More people have access to radio than newspaper, television and computer or mobile media. In addition, most of these radio stations hire staff to produce their media, so those staff become neo-agents for new and budding artists in the Tanzanian market, me included. They aren’t really legal agents because they do not contractually represent any artists. They represent them in intangible forms however, because artists may or may not achieve a following depending on how much the radio station staff expose a new track, album, or mix on their shows.
A few weeks ago I was visiting one such radio station which was fortunate enough to also have staff that produced programming for TV and print. While signing in at the front-gate, I bumped into two young hip-hop artists. They saw me sign in under the name of Vijana FM, and began asking me about whether or not we ran a radio station. I told them we didn’t run an FM broadcast station, but that we were working on marketing educational and entrepreneurial content. They gave me a sample CD (I will be sampling their music next week here), in hopes that I would play it somewhere they could be heard and be exposed to the general Tanzanian population. I hope Vijana FM can help.
The point I’m trying to illustrate is that it is difficult for artists in Tanzania to break through current styles, partly because radio stations are not staying on point with genres across the board. You might be able to catch a new Rihanna track, or hear Drake playing 10 times a day, but you won’t hear the Swedish House Mafia, or Ian Carey. We rinsed Bob Marley’s music but left Lauren Hill behind. We say we appreciate Bongo flava, yet we don’t make room for the younger artists who end up in school abroad and achieve a following there. I might have missed something along the way, but isn’t the point of a radio station to cater to different styles? I understand it is a business and businesses have specific markets they serve, but then radio stations who listen to and play specific genres should be open and honest about that. At least that way, other stations know where they stand. Otherwise they end up undermining the musical talent that exists across the country; artists end up feeling forced to create something that is not truly theirs, and is not truly new. In turn, this undermines what the public likes listening to, because the radio stations are not being open to what else could be played.
Radio in Tanzania should make more room for budding artists. That is the only way venues, concerts, and entertainment in general will make space for innovation. Until people have access to other forms of media, this responsibility lies on the staff who produce programming at radio stations.
And by all means, other interest groups – like Vijana FM – should be encouraging this. How? Through the production of media that is (1) listener-friendly, (2) socially beneficial (ie: good for the public, including artists), and (3) playable in partnership with radio stations.
Ila kuna wanaojaribu kujadili changamoto zinazotukabili kwa kina, na kuna wale wanaoangalia tu picha juu juu.
Njoki Ngumi explains why she doesn’t like to read Kenyan newspapers, and wonders what will happen in 2012. Yet another excellent message from Kuweni Serious!
Why are we – East African youths – running away from activism, NGOs, politics, governance, leadership and many more activities that shape our future in one way or the other? Thinking discussing things like that ain’t sexy?
Get to know a revolutionary artist.
Nneka Egbuna is a new blood of social and political consciousness flowing through the veins of the African continent. She has been compared to Lauryn Hill, and if you listen to her lyrics, you’ll start to understand why. One of her famous song today is called heartbeat, very metaphorical.
Still doubt that music can connect and liberate people? I’ll suggest you listen to Nneka: Nnekaworld and Heartbeat (remix) feat. Nas.
If you cant get enough of her, check out another interview by CNN on Kenyan Vibe.
Reflections and lessons – Thinking about the future? Want to be part of a greater Tanzania of 2061?
It’s 2061, 100 years on since Tanzania became independent, some of us are dead or in our 70s, a history student at Thobolola (for pioneer) University is interested and amazed by the economic developement that her country has reached. Determined to find out the reason behind such development she immenses herself to research on factors that might have contributed to such a growth.
She goes back to the year 2010 when the country seemed hopeless but, a few years later, it had realized her purpose and hence attained such growth: per capita GDP has grown from $1,416 to $28,193, economy is steadily growing at a double digit rate of 14.02%, there is food security, everyone has access to electricity, and the economy is both agriculture and technology driven.
By chance she finds an article online about the ground work that was set by her fathers which could suggest some of the reasons for such growth. Tanzania of 2040 according to The Tanzania Development Vision 2040 developed by many agents of development in the country would be characterized by, she reads:
Ideally, a nation’s development should be people-centred, based on sustainable and shared growth and be free from abject poverty. For Tanzania, this development means that the creation of wealth and its distribution in society must be equitable and free from inequalities and all forms of social and political relations which inhibit empowerment and effective democratic and popular participation of social groups (men and women, boys and girls, the young and old and the able-bodied and disabled persons) in society.
In particular, by the year 2040, racial and gender imbalances will have been redressed such that economic activities will not be identifiable by gender or race. All social relations and processes which manifest and breed inequality, in all aspects of the society (i.e., law, politics, employment, education, culture), will have been reformed.
A nation should enjoy peace, political stability, national unity and social cohesion in an environment of democracy and political and social tolerance. Although Tanzania has enjoyed national unity, peace and stability for a long time, these attributes must continue to be cultivated, nurtured and sustained as important pillars for the realization of the Vision.
Tanzania cherishes good governance and the rule of law in the process of creating wealth and sharing benefits in society and seeks to ensure that its people are empowered with the capacity to make their leaders and public servants accountable. By 2040, good governance should have permeated the national socio-economic structure thereby ensuring a culture of accountability, rewarding good performance and effectively curbing corruption and other vices in society.
- Attain self reliance driven by the psychological liberation of the mindset and the people’s sense of confidence in order to enable the effective determination and ownership of the development agenda with the primary objective of satisfying the basic needs of all the people – men, women and children.
- Be a nation whose people have a positive mindset and a culture which cherishes human development through hard work, professionalism, entrepreneurship, creativity, innovativeness and ingenuity and who have confidence in and high respect for all people irrespective of gender. The people must cultivate a community spirit; one which, however, is appropriately balanced with respect for individual initiative.
- Be a nation with high quality of education at all levels; a nation which produces the quantity and quality of educated people sufficiently equipped with the requisite knowledge to solve the society’s problems, meet the challenges of development and attain competitiveness at regional and global levels.
Means through which this vision was achieved:
- Food self-sufficiency and food security.
- Universal primary education, the eradication of illiteracy and the attainment of a level of tertiary education and training that is commensurate with a critical mass of high quality human resources required to effectively respond and master the development challenges at all levels.
- Gender equality and the empowerment of women in all socio-economic and political relations and cultures.
- Access to quality primary health care for all.
- Access to quality reproductive health services for all individuals of appropriate ages.
- Reduction in infant and maternal mortality rates by three-quarters of current levels.
- Universal access to safe water.
- Life expectancy comparable to the level attained by typical middle income countries.
- Absence of abject poverty.
Good Governance and the Rule of Law
- Desirable moral and cultural uprightness.
- Strong adherence to and respect for the rule of law.
- Absence of corruption and other vices.
- A learning society which is confident, learns from its own development experience and that of others and owns and determines its own development agenda.
A Strong and Competitive Economy
- A diversified and semi-industrialized economy with a substantial industrial sector comparable to typical middle-income countries.
- Macroeconomic stability manifested by a low inflation economy and basic macroeconomic balances.
- A growth rate of 8% per annum or more.
- An adequate level of physical infrastructure needed to cope with the requirements of the Vision in all sectors.
- An active and competitive player in the regional and world markets, with the capacity to articulate and promote national interests and to adjust quickly to regional and global market shifts.
Still digging, she outlines a few remarks that:
- A nation can reach economic development if it finds bold approaches to solving its challenges.
- Identifying its purpose and where it wishes to get in the future is central to development of a nation.
- Health security is achieved through equipment of health service providers by providing them with both a better training and better facilities.
- Building a well-informed and independent society is the right way to go.
Nadhani siku mbili tatu zilizopita tumekuwa na mambo mazito sana hapa. Muda wa kazi umepita; sasa ni wakati wa dawa.
Burudika na muvu za kucheza muziki kutoka enzi zileeeeeeee!
Nawatakia weekend njema watu wote mnaokuja hapa mara kwa mara. Orodha inazidi kuwa ndefu.












