Zinduka ni mpango wa kuweneza ufahamu juu ya janga la malaria kwa nia ya kutokomeza ugonjwa huu. Mpango wa ‘Zinduka’ unatumia sanaa ya muziki kuhamasisha wananchi ili kujiunga katika kupigana na malaria na kujenga Tanzania iliyokuwa haina malaria, kwani ‘inawezekana’. Sasa sijui ni mikakati ipi hiyo serikali ilinayo ya kutokomeza malaria kabisa kama bado kuna mazingira kibao yanayochochea kuzaliana kwa mbu, swali hilo kwa walengwa wakuu. Malaria = Umasikini au, sasa kama tunakubaliana na hoja hiyo, hivyo lipi tulishughulikie kwa kasi, malaria au umasikini ambao unauchochea, ni wazo tu.
Mpango huu umenifurahisha jambo moja, na hilo ni kutumia muziki wa Bongo Flava katika kujaribu kuhamasisha na kuelimisha jamii katika kupambana na malaria. Nyimbo hii inanikumbusha nyimbo ya ‘We Are The World’ kwa ajili ya Ethiopia na ya hivi kitambo kwa ajili ya Haiti. Nimependa sana wazo hili la uhusishwaji wa vijana katika mpango kwa njia ya bongo flava ambao unasikilizwa na wengi, kwani vijana na sisi tunaadhirika na janga hili la malaria. Nadhani serikali inabidi ihusishe vijana zaidi katika maswala ya kijamii, kwani sisi ndio wajenzi na waadhirika wakuu wa magonjwa na umasikini. Tanzania bila malaria haiwezekani mpango umasikini upunguzwe na makazi ya watu kuboreshwa, lakini bila hivyo tunajaza maji kwenye gunia.
Ningependa kusikia mawazo kwenye upande wa uzuri wa muziki wenyewe , kama kweli unamvuto na unaweza kuvutia watu na kuwahamasisha au hauna mvuto kihivyo. Mimi nadhani utunzi na utengenezaji wa nyimbo yenyewe ungeweza kuwa mzuri zaidi. Lakini wanasema, kila safari ndefu huanza na hatua moja, na hivi ndivyo tunaanza hivyo hongereni mwanzo mzuri.