Fid Q – Bongo Hip Hop Star

Fareed Kubanda a.k.a Fid Q ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Hip Hop wenye uwezo mkubwa katika utunzi wa mashairi. Album yake mpya inayoitwa “Propaganda” haitakuwa na uchache wa vina na misemo, kwani fasihi simulizi ya Fid Q katika kughani niya hali ya juu. Fid Q kama wasanii wengine wa hip hop/ bongo flava, wameanza kuchanganya lugha, yaani kiingereza na kiswahili katika nyimbo zao. Msanii mwingine ni K-Lynn na nyimbo yake ya I am not a flirt. Hili ni jambo jipya kidogo, kwani mpangilio huu umezoeleka zaidi na wasanii wa genge wa Kenya. Nimejaribu kufikiria ni nini hasa kimepelekea sababu hii, na jibu moja nililojipatia ni, kutaka kupenyaza hip hop ya bongo katika soko la dunia.

Lugha ya kiingereza itaweza saidia watu wa nje waweza kuelewa na hapo hapo bila kuwapoteza wapenzi wa bongo hip hop wa nyumbani kwa kutumia kiswahili pia. Kitu kimoja ambacho bado sijaelewa ni kwanini album za hip hop Tanzania haziwezi kuuzwa kwenye itunes, ili kuwapa watu wa nje urahisi wa kuzinunua na hapo hapo kuwaongezea wasanii wenyewe kipato kwani mauzo yataongezeka. Kama nia ya uchanganyaji lugha nipanua wigo wa watu wanaokusikiliza na kupenyeza kwenye soko la dunia la mziki, basi kuna umuhimu pia kuuza album kupitia itunes.

Video yake yakitambo kidogo ya nyimbo “I am a Professional” inazidi kudhihirisha mpangilio mpya wa kuchanganya lugha mbili katika nyimbo za bongo hip hop/ bongo flava

I think its important we support local artists, because people like Fid Q have the ability and the skills like many of the US rappers, and even better than some of them. But like I said before, the idea of selling bongo hip hop albums on itunes is something that needs to be looked into. Look for Fid Q new album called “Propaganda” and listen to this guys word play skills.

Hii ni single mpya ya Fid Q Danger kutoka kwenye album yake ya “Propaganda”
To listen to more of Fid Q music visit his facebook

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 2 Comments

2
  1. hiphop imesimama bongo sema watoto wadogo wanaichezea fasihi kazi mbovu punch zao haziwezi kupganishwa na mistari ya harakati waimbe na kubanja vizuri hila waache kupga kelele iko hvyo hiphop ni wito na co kila mtu ameitwa wagonge kazi na co mapenzi

  2. mwana umetisha ni miongoni mwa majembe ambayo nayakubali sana TANZANIA na ni kweli nina maanisha what am talking.100

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend