Msanii Afande Sele alipataga kutunga wimbo uliotwa, “darubini kali”, ambao ulimwongezea umaarufu hadi kumsaidia kushinda tuzo ya Mfalme wa Rhymes. Nyimbo ya “darubini kali”, ilizungumzia mambo mbalimbali ya jamii. Nyimbo hiyo pia ilifanikiwa kuonyesha uhusiano kati ya kazi ya sanaa, mfano sasa Bongo Flava, na jamii inayozungukwa nayo. Katika maneno yake mwenye, Afande alisema, “mimi ni msanii, mimi ni kioo cha jamii”, hivyo kujenga hoja kuwa sanaa ni chombo ambacho kinatumia fasihi kuyaweka bayana matatizo yaliyomo ndani ya jamii zetu.
Hivyo basi, leo hii ninadiriki kusema bongo flava inakibarua kikubwa cha kuzungumzia maswala ya jamii ya sisi vijana. Sanaa hii inatoa moja kati ya nafasi chache ambazo vijana tunazo kuelezea na kujadili matatizo yetu. Pamoja na ukweli kuwa zipo nyimbo ambazo zinazungumzia matatizo haya, lakini ubunifu wa kisanii si wakuridhisha sana. Mimi ninaamini, ili sauti ya msanii iweze kusikika na watu wengi, lazima kazi ya msanii iwe na ubunifu utakaofanikisha kutofautisha kazi yake na kazi za wasanii wengine. Sasa basi, kwakuwa swala ni kuwakilisha vijana na kuwasilisha matatizo ya vijana, nimefurahishwa sana na nyimbo hii ya “samahani wanangu” ya msanii Mrisho Mpoto. Bwana Mpoto amezungumzia matatizo yetu vijana na baadhi ya vyanzo vya matatizo hayo.
Nitapenda sote tusikilize maudhui yaliyomo ndani ya kazi hii ya kisanaa na kuwa makini katika kusikiliza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika nyimbo hii.
Mrisho Mpoto na ‘Samahani Wanangu”
Mrisho Mpoto akihojiwa na starlink