Wajapani wamekuja na ujuzi ambao kinadharia unaweza tatua tatizo la usambazaji wa chanjo. Wameweza kumtumia mbu kusambaza dozi ya chanjo kila atakapokuwa ananyonya damu (hapa walitumia panya). Walichofanya ni kumbadili mbu maabarani ili aweze kutengeneza dawa ya chanjo dhidi ya Leishmania ndani ya gland zinazotengeneza ‘mate’ (mbu hutema ‘mate’ yake kabla ya kunyonya damu ili kuzuia damu kuganda). Wameweza kupima muongezeko wa antibodies kwenye panya waliong’atwa na hivyo kinadharia kufanikisha chanjo.
Je, si itakuwa ‘kali’ pia tukiweza kutumia mbu kusambaza chanjo dhidi ya malaria na sio mdudu mwenyewe?
Matokeo ya utafiti huu hayako kamili, kwani bado hawajapima uwezo wa chanjo hiyo kupunguza maambukizi ya ugonjwa wenyewe, ila ni tafiti pekee na ya kwanza kuweza kutumia mbu kwa namna hii. Je tutaacha kutumia sindano hapo mbeleni? Je utakubali mbu kama hawa watumiwe kusambaza chanzo za malaria hapo baadaye? Kuhusu dozi je – ukingatwa mara 1000 na mwingine mara 50? Hapa kengele ya maadili na kanuni (ethics) za sayansi inaendelea kulia.
* http://ngm.nationalgeographic.com/2007/07/malaria/finkel-text