Wiki chache zilizopita, tulikuwa na mjadala hapa kuhusu Dambisa Moyo na ujumbe wake kuhusu athari za misaada ya maendeleo katika ukuaji wa uchumi wa Afrika. Leo nimetazama hotuba ya mchumi mwingine mashuhuri kutoka Ufaransa, Esther Duflo, mshindi wa mwaka huu wa medali ya Clark, almaarufu kama ‘the baby nobel’.
Prof. Duflo anafanya utafiti unaojaribu kufahamu ufanisi wa misaada hii katika kupambana na umaskini. Kwa kutumia field experiments ameweza kuainisha umuhimu wa baadhi ya misaada hii katika kupambana na umasikini. Baadhi ya tafiti hizo ni; umuhimu wa ugawaji bure wa neti zenye dawa ya mbu, mapambano dhidi ya minyoo mashuleni katika kusaidia upatikanaji wa elimu, umuhimu wa incentives kwenye miradi ya chanjo, n.k. Hapa mjadala sio uwepo wa misaada au la, bali ni namna gani tunaweza kutumia kwa ufanisi fedha au rasilimali za miradi ya upambanaji wa umasikini.