Utoaji mimba

Kuna mambo nyeti ambayo hupaswa kuangaliwa na kujadiliwa kwa utulivu wa hali ya juu. Hatuna budi kujaribu kuweka hisia na “uzoefu” wetu pembeni ili tuweze kupata suluhisho ambalo litasaidia mabinti na dada zetu; bila kusahau vizazi vyetu vijavyo kwa ujumla.

Kutokana na utoto wangu, nimekuja kulielewa na kuanza kulifuatilia suala la utoaji mimba nilipokuwa kidato cha pili. Wakati ule nilikuwa nashangaa: Vipi, Vijana wanaonekana wanashiriki sana kwenye vitendo vya ngono, lakini “matokeo” (ukiacha Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa) mbona siyaoni? Na akili yangu ilikuwa inaniambia hivi vitu vitatu vina tabia ya kwenda sambamba kwenye jamii zenye desturi kama zetu.

Bahati mbaya watu walionipa mwangaza kwenye mambo yanayoendelea mitaani walikuwa ni Vijana wenzangu vijiweni.

Utoaji mimba… Unashtukia binti fulani anatoweka darasani kwa siku kadhaa halafu akirudi unaona kuna mabadiliko fulani. Ingawa bado nilikuwa kinda, lakini kuna ile sauti kichwani kwangu iliyokuwa inaniambia kuwa vitu haviko sawa kama inavyotakiwa.

Wiki mbili zilizopita Serikali imeamua kuvalia njuga hili suala na kuanza kufunga zahanati na vituo vyote ambavyo hushiriki (kwenye) utoaji mimba. Inaonekana Serikali kama inatumia ile tactic ya kijeshi ya kumshtukiza adui wakati hategemei kabisa kushambuliwa. Lakini tukumbuke hapa tunapigana vita na kuuana wenyewe tu.

Mimi sio mtaalamu wa afya na nisingependa kuhusisha imani za dini kwenye huu mjadala. Kwa kifupi — kwa maoni yangu binafsi — nadhani wazee wetu wangejaribu kulivalia njuga hili suala kwa upole kiasi. Kwanza, kuangalia nini hasa ni chanzo cha hizi mimba zisizo na mpangilio. Pili, kujaribu kupunguza haya matukio kwa kutumia elimu na sauti ya utulivu. Tatu, kuwaonya na kuwaambia watu wanaohusika na utoaji mimba kuwa ‘tunawaona, tunawajua na tunaamuru muanze kusafisha nyumba zenu!’

Bila kusahau kuwaasa wazazi kuongea na watoto wao kwa uwazi – mabinti na wavulana, pia. Kwasababu inaonekana jamii yetu bado ina ile soni ya kuongelea mambo ya ngono na madhara yake.

Nisingependa kuwapotezea muda wenu kwasababu nina uhakika hamtajifunza jipya kutoka kwangu. Kwahiyo, nawaasa wale ambao wanasomea haya mambo, kuyafuatilia au kufuatilia nchi ambazo takwimu zao kwenye mambo kama haya ni nzuri, kutupa ujuzi na maoni.

Natumaini sauti zetu zitawafikia wahusika, kwasababu hili jambo ni nyeti mno na linahitaji kuguswa kwa utulivu kama tunavyotoa uchafu kwenye mboni za macho yetu.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 3 Comments

3
  1. najaribu kutafakari zaidi bila kuwa mnafiki… sitaki kusukumwa na maadili bali uchambuzi na hali halisi, nikitazama ushahidi huu… 'Unfortunately only 33 percent of boys and 50 percent of the girls reported using condoms in their first sexual encounter: “About one in 10 students who have had sex did not know whether a condom had been used. A similar pattern is seen for condom use at last sex.” halafu tena 'in South Africa, 23% of females had their first sexual experience with someone much older than themselves. The data suggests that much early sexual experience is conducted in contexts where there are such marked power and maturity differentials that manipulation must be considered an important determinant of early sexual experience'. Binafsi nimeshiriki katika utafiti wa hali za vijana Lesotho, na zaidi ya 40% ya wasichana wanasema their first sex was a rape… katika hali hii na ushahidi hapo juu ni kuwa asilimia kubwa ya wasichana hufanya ngono mara ya kwanza bila ridhaa yao. katika hali hii wengi hupata mimba wasizotarajia na mbaya ni kuwa kina baba wanawatelekeza, wasichana wanafukuzwa shule na nyumbani pia ilhali wanaume wanapeta. Hawakupanga kupata mimba. msichana anapobakwa hapangi kupata mimba. Hivi unamsaidiaje binti kama huyu? Azae tu ili ajifunze? Kwanini mtu ajifunze kwa makosa ya mtu mwingine? Angalau wanaume wangekuwa wanabeba mimba wangeelewa.
    Binafsi sioni tatizo la safe abortion, si kwa sababu ya kuiga umagharibi bali katika hali ambayo inalazimu kumsaidia mtoto wa kike? Vipi kama inalazimu kufanya abortion ili kuokoa maisha ya mama! bahati mbaya tunagubikwa na mitazamo ambayo inang'ang'ania maadili bila maarifa.Najua watu wa mrengo wa pro-life wanachukia sana lakini huwezi kupingana na ukweli na hali halisi. leo nilikuwa nasikiliza presentation toka mtu wa Ministry of Health Tz hapa Kampala, huwezi amini kuwa mahitaji ya supplies za reproductive health ni 9bln Tsh lakini pesa ambayo imekuwa allocated ni 2bln Tsh, hii ni pamoja na contraceptives na family planning methods… sasa jiulize ni wangapi hasa vijana hususani wanapata? Inawezekana kuwa ni kweli utoaji mimba haujasaidia? lakini mbona inafanyika tena sana na kwa kificho ambayo ni hatari zaidi? siungi mkono kuwa hili jambo lifanyike kiholela lakini lazima kujenga mazingira ambayo yatafanya utekelezaji wake ufanyike kwa umakini na usalama. hata tukijidanganya bado itaendelea… mbaya zaidi tunajifunika shuka la maadili na kuziba nyuso tusione ukweli… KWELI NDIO ITATUWEKA HURU

  2. Wakati nafikiria kuandika hii makala ili kuchokoza mawazo ya watu, nilikuwa naombea utokee mjadala ambao utafundisha wengi (hasa vijana). Tovuti niliyoiambatanisha hapo juu (kwenye post) inakupa picha ya mambo ambayo hayaongelewi kabisa; ni mwiko kujadili — lakini watu wamepewa nafasi na wameamua kutoa ule ukweli wa mambo yanayofanyika kwenye giza.

    Kwahiyo, nashukuru Ndg Shakim kwa kutuletea facts. Nilipata fursa ya kuangalia documentary moja (ya Bondeni) ambayo inasema katika kila wasichana wanne, mmoja amebakwa angalau mara moja! Inasikitisha lakini ndio ukweli — hatuwezi kuyafumbia macho haya mambo na kujifanya kila kitu ni shwari.

    Ninachojaribu kusema ni hiki: Kama Shakim alivyosema hapo juu, ukweli ndio utatuweka huru. Ongeeni na watoto wenu vizuri. Jiulizeni kwanini wanakimbilia kutoa mimba kiholela? Hatari?

    Na kwa upande mwingine, Wizara ya Afya kukurupuka na kuamua kufunga hizi zahanati zote, nadhani hii italeta madhara zaidi kuliko manufaa kwa jamii.

  3. Samahanini lakini hivi inakuwaje hata akina dada, wazuri, masister du wa nguvu anapata mimba? (hapa jamani sizungumzii wale wa vijijini, nazungumza hao waliofika zaidi ya form 6 ambapo tunapishana nao viwanja). Tusikatae manake hawa wa mjini, ndo wanaongoza kwa shughuli hiyo mpaka dawa zinatolewa pharmacy kama panadol tu!

    Hivi hawajui namna ya kujikinga wasipate hizo mimba au ni kuwa utoaji mimba umekuwa mwepesi sana kiasi cha kuwa hakuna anaejali?

    (hawajali madhara ya utoaji kama wasivyojali madhara ya uwezekano wa kupata maradhi kama Ukimwi na mengineyo)

    Hivi anaeweza kwenda dukani kununua dawa ya kutoa mimba kweli anashindwa kwenda dukani kuchukua contraceptives za kuzuwia kutunga mimba kweli?

    aah I forgot, contraceptive karibia zote lazima uwe na nidhamu katika ulaji wake or else hazifanyi kazi. Na sie wabongo hatujazowea, kwa hiyo bora kutoa tu! ….Kweli binaadamu hatujihurumii…duh

    http://allafrica.com/stories/201101100328.html

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend