Tumepata waraka huu kutoka kwa mmoja wa wasomaji wa Vijana FM (Japhet Joseph):
Tanzania Commission for Universities (TUC) ilibadilisha utaratibu wa wanafunzi kujiunga na elimu ya juu kupitia Central Admission System (CAS), ambapo mtu analazimika kutumia simu ya mkononi na mtandao (internet) kuomba nafasi.
Mfumo huu umesaidia kwa kiasi fulani lakini tatizo linakuja kwa wale ambao hawajajiunga mpaka tarehe hizi za mwisho, ambapo mwanafunzi analazimika kukaa kwenye internet café hadi saa tano usiku na kuendelea ili kupata huduma hii — wakati huu system inakuwa haijaelemewa.
Suala lingine ni kwa wale waliopo vijijini. Hivi wanajua taratibu hizi mpya au wanaendelea kusubiri matangazo ya redio ili wakachukue fomu za vyuo vikuu? Tunaomba wanaohusika na huduma hii waboreshe taratibu hizi nyeti ili wanafunzi wote wapate fursa ya kuomba nafasi kwenye vyuo.
Tunashukuru kwa msaada wenu.