Na Japhet Joseph
Mashindano makubwa kabisa duniani ya mpira wa miguu – au kama wengine wanavyouita macharange au kabumbu – ndio yananukia; kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya Afrika! Wasanii mbalimabli wamejitokeza kuwashawishi watu wa FIFA kuwateua ili wapate nafasi ya kutumbuiza wakati huo.
K’naan (ft. Bisbal) – Waving Flag:
Lakini baada ya kufaidi mambo kama haya na ukatulia, huna budi kujiuliza: Hivi, mbona sisikii hata wimbo mmoja wa Kiswahili? Wasanii wetu walijaribu kuimba nyimbo kwa ajili ya Kombe la Dunia? Walijaribu kutafuta nafasi ya kutumbuiza? Au DJs wa FIFA/Bondeni wanatubania tu (wanataka mshiko kwanza)?
Kama hamkujaribu, aisee, mmepoteza bonge la nafasi la kuitangaza nchi, lugha na kazi zenu.
Ni mtazamo tu.