Msanii mkongwe Sugu au kama alivyokuwa akifahamika enzi zile kama Mr II anakuja na album itakayoitwa antivurus. Mixtape hii itakayoshirikisha wasanii wengi wa bongo flava, inakuja kwa dhumuni la kupigania sanaa hii na kupigania haki ya badhii ya wasanii wa sanaa hii ya bongo flava na bongo hip hop.
Hivi karibuni kumekuwa na mijadala kadhaa kuhusu mwelekeo wa sanaa ya bongo flava, lakini kidogo kimekuwa kikifanyika kuitetea ipasavyo. Katika makala ya penye kufuka moshi niliweza kujadili uhasama unaoanza kujengeka kati ya wasanii wapya na wale wakongwe. Wasanii wakongwe wamekuwa wakiwalaumu wasanii chipukizi kuwa wanachangia katika kuudhofisha mziki huu wa bongo flava. Nadhani kila mtu analake la kusema juu ya malumbano haya, kutegemeana na upande unaoshabikia.
Shauku yangu na hii mixtape ya antivirus ya Sugu ni kuwa itasaidia kuweka hili tatizo bayana kwa kuwataja wahujumu wakuu wa sanaa hii. Nadhani muda umefika kwa baadhi ya wasanii kuweka msimamo na kusimama pamoja kutetea mziki huu. Tuombe harakati hizi ziweza kuzaa matunda, kwani wengi wanaamini mziki huu umepoteza dira kwa kiasi fulani, sasa sijui kama wewe unakubaliana au kupingana na hoja hii.
Habari hii kwa hisani ya bongo5.com