Mwandishi wa habari kutoka Afrika Kusini, Sam Rogers , (Mtengenezaji wa Filamu za Factuals — kitengo cha Uhalifu na Uchunguzi) ametunukiwa tuzo ya mwandishi bora mwaka 2010 kutokana na filamu yake “Curse of the Nobody People.” Filamu ya Sam inazungumzia matatizo ya walemavu wa ngozi, Tanzania; ubaguzi na mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi.
Mtu mwingine aliyetunukiwa tuzo hii kwa mwaka 2009, ni John-Allan Namu, mwandishi wa habari wa KTN, ambaye aliaandaa filamu inayoitwa “In the Shadow of the Mungiki.” Wasilikilize walikuwa na yapi ya kusema (kwa kifupi):
Matatizo wanayoyazungumzia sio mapya masikioni mwetu. Nimeperuzi haraka haraka na nimevutiwa na kazi zao. Nadhani unaweza ukazipata kazi za John-Allan kwa urahisi youtube. Nitajaribu kutafuta filamu zao zenye ubora unaokubalika na kuziweka hapa Vijana FM ili tujifunze mawili matatu.