Anti-Virus mixtape imenena

Dawa ya virusi ndio imeshamwagwa mtaani, na  parapanda ndio imeshalia. Msanii wa muda mrefu, Sugu ndio ameshapakua ile mixtape yake ya AntiVirus niliyolonga juu yake kitambo kidogo. Mixtape hii imeleta mshikemshike jijini na sitashangaa kama pia imeleta kizunguzungu kwenye jamii ya wana bongo flava.

Nyimbo ya I Wanna Kill Ru.., unaopatikana kwenye mixtape hiyo umepelekea Sugu kuitwa na kuhojiwa na polisi. Pamoja na mistari ya nyimbo hiyo kuwa mikali kidogo, lakini je, ni kweli kuwa Sugu anataka kuua au ni utundu tu wa mashairi?

Mixtape hii imeibua hoja kadhaa, moja ikiwa ya uhusiano kati ya redio na wasanii, pamoja na nafasi ya redio katika kukuza sanaa nahata nafasi ya redio kuuwa sanaa. Neno bongo flava lilizaliwa redioni, na redioni huko huko ndipo bongo flava ilipolelewa na kukuwa mpaka hapa ilipofikia. Lakini je, redio zimefanya kazi ya kutosha kukuza ubunifu katika sanaa hii ya bongo flava? Kwani, swala la ma-Dj kuwa mameneja wa wasanii linapigiwa kelele kila siku, kwani ma-dj hao mamaeneja wanashukiwa kuwapendelea wasanii wao. Kama hii ni kweli, upendeleo huo ni ufa, tena ni ufa unaoweza kuhatarisha maendeleo ya sanaa hii inayoajiri vijana wengi.

Pamoja na yote, mashairi ya Sugu na wenzake katika mixtape hii yanaweza kuangaliwa katika pande mbili. Pande ya kwanza, ni kuwa mashairi yao yanachochea chuki na hata kuleta fujo. Pande ya pili, ni kuwa mashairi yao yanaongea ukweli mtupu, na lugha kali waliyotumia ni kutokana na kuchoshwa na unyonyaji katika sanaa ya bongo flava. Inawezekana pia Sugu ameamua kujitoa muhanga na kutuonesha roho ya udhubutu, kwani Watanzania tuna sifa ya kukubali yaishe. Sasa basi, kama mashairi ya mixtape hii yataleta fujo, Sugu na wenzake watakuwa na kesi ya kujibu. Lakini kama tunakubaliana kuwa mabadiliko “changes” huja mara nyingi kutokana na mapambano ya aina fulani, basi Sugu ndio anatuonesha njia, kama Bob Marley alivyoimba Get Up Stand Up.

Swali, je Mixtape ya Antivirus inatetea muziki wa bongo flava dhidi ya wachache wanaouyumbisha au inataka kuchochea fujo zinazotokana na chuki kibinafsi? Sasa soma tamko rasmi alilotoa Sugu kwa vyombo vya habari juu ya kasheshe zilizomkumba siku mbili hizi tangia Mixtape ifike mtaani.

Download Anti-Virus mixtape hapa…

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 9 Comments

9
  1. Sijui sheria gani zitambana Sugu kutokana na lyrics zake – labda a defamation suit, ila haiwezekani kila mwanamuziki awe anatoa malalamiko kwa watu hao hao. There has to be something true about huu uonevu wa wanamuziki wetu.

  2. Mixtape haziuzwi ila ni kwa ajili ya publicity. Kusema kweli bongo flava imeshuka mno, yaani ile mipini ya kweli ya miaka ya nyuma imepotea kabisa. Ndio tatizo la ku-commercialize muziki bila kujali creativity ya wasanii…ukweli ni kwamba kuna waburudishaji (entertainers) wengi kwenye bongo flava na sio wanamuziki halisi.There’s a thin line between defamation of character and freedom of expression. It’s up to the targeted audience to judge.

  3. Hii mixtape imenichekesha sana, hasa skit za humo ndani. Nitapenda kuona walengwa watarespond vipi, manake upande mmoja umeshatoa dukuduku lao. Nadhani hii mixtape itasaidia kuanzisha mjadala kuhusu redio na jinsi inavyoua sanaa hii. Sugu alikuwa kati ya watu wa kwanza kufanya mziki wa bongo flava kukubalika, hasa baada ya ile nyimbo yake ya “ni wapi tunakwenda, tu tunakwenda”, na nadhani atakuwa miongoni wa wasanii wa kwanza katika kuleta mapinduzi dhidi ya wanyonyaji wa sanaa hii.

    Nimependa idea yake, kwani wasanii wa aina zote wanadharauliwa na kunyonywa, uwe mchoraji, mchongaji n.k, naona mwanzo wa kupigania haki za wasanii na sanaa zao ndo unaanza kama hivi.

    Kwanza hizo redio bila nyimbo za wasanii sijui watafanya nini, hivyo sielewi ni kwanini hawaheshimu. Nadhani hilo liligusiwa kwenye hii mixtape. Hizo redio zinahitaji wasanii na kazi zao ili wao waendelee kuwepo hewani, hivyo kama vipi wasanii wanaweza kuwasusia alafu tuone.

  4. “wengi hawajajua Sugu ni kama mvua….napotaka kunyesha nanyesha tu” lol

    Sugu ndo N.W.A wetu.

  5. angalia hao watangazaji wanaajiriwa vipi? Ukweli wanaokotwa mitaani na hata kwa mfano Gadna alitolewa kazi ya kaunta baa hadi studio kutangaza… maadili hovyo, elimu husika hakuna, je hawataishia kulamba miguu ya ruge? sioni watakachojibu. Ruge ameita kundi la wasanii ili kutengeneza promo kuonyesha mafanikio ambayo wasanii wamepata kupitia Clouds ili kuipa picha nzuri mbele ya jamii lakini anti virus ishamwagwa
    Sugu ni mwanamapinduzi na mapinduzi ni kujitoa mhanga…

  6. Sasa, jamaa kajitoa mhanga; inaonekana anaamini kuwa kuna watu wako pamoja nae.

    Ujumbe natumaini umefika kwa wahusika. Lakini kuna sehemu ya akili yangu inayoshindwa kuelewa kwanini wametumia lugha ambayo sio nzuri kwenye masikio ya watu wengi (wasio vijana). Labda kero zimezidi; frustrations za miaka nenda rudi.

    Mimi kama kijana nimewaelewa wanachosema na nimesikia kilio chao. Bahati mbaya nina mashaka labda hakuna litakalobadilika sana (kwenye maslahi na haki za wasanii), hasa kwasababu wahusika wakuu hawakutumia hata ubeti mmoja kujadili suluhisho la matatizo yao.

    Unaweza ukawatupia mawe watu kila siku, lakini usipofanya juhudi za maana, hakuna lolote litakalobadilika (pia, kumbuka kuna wasanii wengi tu ambao wanafaidika na kinachotokea sasa hivi). Nimeshawashauri wanamuziki kuwa na UMOJA… wanaweza wakawa wanachanga — kila baada ya show hela kiasi fulani inaenda kwenye chama au umoja wao ambao utakuwa unashughulikia haki/maslahi yao.

    Kwa mfano, kila msanii akichanga sh. 50,000 kila mwezi ili waanzishe kampuni ya kusambaza kazi zao, haitapunguza kunyonywa kwa kiasi fulani??

  7. Yeah, tsup!E bana soon after tachin’ the mixtape my mwili ulitetema ileile. The torrential rain has hit the mawingu so what we are eager to know ni mpango wa kuckia hzo response dha hao watangazaji-wanamuziki wa kukurupuka coz wanafiikiri ku-hold micro4nes everyday kwa radio stations ndo kujua ku flow. Meeeeen, mziki sio mlenda. If those pepo can do wacha wajibu hiyo mix-tape. Punk

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend