Mashabiki wa Vijana FM

Takwimu zifuatazo zinaonesha watembeleaji wa Vijana FM kuanzia siku tulipohamia http://vijana.fm, tarehe 21 Juni, hadi 5 Julai, 2010. Napenda kutanabahisha kuwa wanaohesabiwa ni visitors na sio page loads; kwa maneno mengine, uki-refresh ukurasa wa tovuti, mtambo haukuhesabu kwasababu tayari uko maskani!

Nchi zinazoongoza kwa kuwa na watembeleaji wengi:-

Africa:

  • Tanzania – 135
  • Kenya – 11
  • Afrika Kusini – 7

Asia:

  • Syria – 22
  • India – 16
  • China – 14

Amerika ya Kaskazini:

  • Marekani – 261
  • Kanada – 45

Ulaya:

  • Uholanzi – 194
  • Ujerumani – 134
  • Uingereza – 109

Pia, ukiacha da’ Subi ambaye hutembelea Vijana FM mara kwa mara, miji ifuatayo ina watu ambao nadhani huja hapa kijiweni karibia kila siku: Xian na Wuhan (China), Eindhoven na Maastricht (Uholanzi), Vienna (Austria), Stuttgart na Bremen (Ujerumani), Zurich (Uswizi) na Kharkov (Urkraine). Wengine wanatoka Vasteras (Sweden), Oslo na Tromso (Norway), Seoul (Korea ya Kusini kwa kina Ji Sung Park) na Arusha (Tanzania).

Tunaomba msaada wa kuitangaza Vijana FM hasa Afrika Mashariki, kwa watu ambao mnadhani watafaidika na tunayoongelea na kujadili. Bila kusahau wanafunzi walioko India, Malaysia, Thailand na Afrika Kusini.

Natanguliza shukrani za dhati (kwasababu nimepata somo la Jiografia tosha) na nawaomba muendelee kutembelea Vijana FM!

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 7 Comments

7
  1. Hongera sana VijanaFM kwa hatua mliyopiga kufikia hapa, kumbuka, “A journey of a thousand miles begins with a single step,” Lao-tzu, Chinese philosopher (604 BC – 531 BC)!

  2. Dah! Mazee hii ni HATUA nzuri sana mliofikia mpaka sasa. Natumaini baada ya muda watu watalipata fresh hili libeneke murua kwa vijana huku nasi(mimi binafsi nikiongoza mashambulizi) tukiongeza chumvi kusaka wadau wapya bila kusita hapa chini ya Jua.

    Count on my support..

  3. Mzee Meko, pamoja! Uko kwa kina Ji-Sung au?

    Mallaba, bila shaka wewe ndio yule wa kutoka Xian! 谢谢

    Nilipata nafasi ya kutembelea tovuti ya organization yako – http://www.mallaba.org/ – jana jioni. Nakutakia wewe na timu yako nzima kila la heri. Nadhani wenyeji wako wanasema: 最好的祝福。

  4. Yap yap kaka, niko kwa Kijana Ji-Sung Park na vijana kadhaa wakiongozwa na Alex kutoka U.K. tukilikuza libeneke kwa sana tuu…

    Kaka Malaba nimetembelea kwako pia na kukuta mambo mazuri muno. Hongera sana na nakutakia kila kheri katika kuwaonyesha watu njia za kupata NONDOZZZZ ughaibuni/mtoni…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend