Habari zilizofanyiwa utafiti

Kama kawaida yangu, nilikuwa naperuzi kurasa za tovuti ya jirani siku chache zilizopita na nikapata maoni ya Watanzania wenzangu kuhusu uandishi wa habari Tanzania, na bila kusahau mapungufu yanayojitokeza mara kwa mara kwenye taarifa tunazopata.

Kuna wachache sana ambao wanastahili pongezi, lakini hatuwezi kunyamaza pale tunaposikia kuwa hata Rais wetu mstahafu, Benjamin Mkapa, alishawahi kuwapaka waandishi wa habari wa Tanzania; kwa kuwa wavivu kufanya utafiti kabla ya kufanya mahojiano na matokeo yake hushindwa kuuliza maswali ya msingi au kuwa na mijadala ya maana itakayoweza kuinufaisha jamii kwa ujumla.

Mimi ni mpenzi wa habari zilizofanyiwa utafiti kwasababu huwa zinanifumbua macho na kujisikia kama nimeshafika au kuona sehemu mbalimbali. Kwa maneno mengine, zinanipa picha halisi ya maisha ya watu kutoka sehemu mbalimbali. Leo hii nikikutana na watu kutoka Uswazi, najua wapi pa kuanzia mazungumzo. Au naelewa mambo gani hasa yanayomzunguka mhusika. Nikikutana na mtoto wa geti kali au wale wa matawi ya juu, siwezi kuishiwa na maneno!

Miezi michache iliyopita mwandishi wa habari wa KTN, Kenya, John-Allan Namu alitunukiwa tuzo ya Mwandishi Bora Afrika (2009) kwa habari yake ya utafiti wa kina kuhusu Mungiki. Ni mengi sana utajifunza kutoka kwa kijana mwenzetu. Na wale ambao wana ndoto za kuwa waandishi wa habari hawana budi kuwaangalia kina John-Allan na Vicky Ntetema. Ninaamini kuna hadithi nyingi sana mitaani ambazo zinahitaji uvumilivu kwenye utafiti; inaweza kuchukua siku kadhaa, miezi au hata mwaka, lakini habari zikifikia hadhira, matunda yake yataonekana.

Hii yote ni katika kujifunza na kukubali majukumu yanayoambatana na kuwa mwandishi wa habari.

Binafsi, kazi hii ya John-Allan imenivutia mno:

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 3 Comments

3
  1. Tatizo waandishi wetu wengi wanatoa habari kwa ajili ya kuganga njaa bila utafiti wowote, na muda mwingine kitu wanachokitoa wao wenyewe wanakuwa hawana uhakika nacho. Basi inabakia tu kama biashara ya kutoa anachokisikia.

    Habari iliyofanyiwa utafiti siku zote inakuwa na mvuto wake, hata jamii inaposikia kwani kunakuwa na maswali mengi ya: Je, haya yalianzia lini? Wapi? Je, itakuwaje baada ya hayo?

  2. Sote tunajua kuwa kufanya documentary ya kitafiti itakayooneshwa kwa saa moja yahitaji miezi kadhaa ya kazi. NANI ANATAKA HILO?

    Ni wafanyakazi wangapi wa Radio wako tayari “kusaga lami” kutafut habari?
    Na mwisho swali laja kuwa ni nani mwenye control hapa. Waandishi aa wasikilizaji? Hebu tazama Blogu zetu kaka. Zile zenye number kubwa ni zile ziandikazo UDAKU.

    Si unaona idadi ya watembeleaji na watoa maoni humu? Ni walewale kina siesie tuandikao. Hutakuta “photo-journalist” anatoa maoni humu na pengine hata ku-follow blog yako kwa kuwa INACHOSHA. Hawatufuatilii, hawatujali na kwao habari ni kubandika picha na kuanza mbele.

    CHEAP SHOTS.

    Ndilo kubwa wanalopenda. Na jamii inazidi kujikita huko. Ati wanasema ni habari, lakini wenzetu nje ya nchi hata UDAKU unafanyiwa utafiti na ukidhi mahitaji yooote ya kihabari. Na ndio maana kwenye matukio yahusuyo maisha ya watu, hata vyombo vikuu vya habari vyachukua channel za udaku as their source.
    Mfano alipofariki Michael Jackson, watu wa kwanza kuhakikisha hilo hewani walikuwa TMZ. Kisha CNN na vyombo vingine vikubwa vikawanukuu TMZ mpaka baadae saana walipohakikisha wao. Japo ni udaku, lakini UMEHAKIKISHWA. Kwetu si hivyo.

    Kwetu ni kama vile 95% ya radio na muda ni muziki (kwa kuwa wasanii wanalipia nyimbo zao kuchezwa radioni) na hiyo 5% iliyobaki ni TAARIFA na si HABARI (kama nilivyowahi andika hapa [bofya].)

    INASIKITISHA SAANA.

  3. Mzee, sidhani hata kama wanasikia kilio chetu. Yaani, tumeandika, tumewakosoa, lakini bado uozo ndio unazidi kuendelea!

    Sasa, tatizo ni elimu wanayopata ambayo labda hawafundishwa majukumu yao kama wana-habari; kuitumikia na kuifunza jamii; kujaribu kutoa habari “sahihi”?

    Kibaya zaidi, hata vijana wengi hawajui kinachoendelea… Kwasababu mtu anatumia blog au tovuti au redio moja tu kama chanzo cha habari. Ndio matokeo yake tunayaona… Nikiendelea nitapata ghadhabu! Ngoja niifurahie Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend