Marehemu Prof. Mwaikusa kwa wengi alikuwa mwalimu wa sheria Chuo Kikuu Dar es salaam (UDSM). Lakini wengi tulimjua kama mwanafamilia. Wengi waliokulia chuo wakiwa wadogo wataelewa ni nini ninachokisema. Hatuwezi kumuongelea Prof. Mwaikusa bila kuzungumzia suala la uzalendo.
Hili suala la uzalendo bado linaendelea kuwa tete katika Tanzania yetu. Ninasema hilo kwani, kama wazalendo wa kweli bado wapo, wengi basi watakuwa wamejificha, kwani wanaoongea ni wachache. Leo tumepoteza mmoja aliyekuwa anaongea; tumepoteza mzalendo wa kweli, na sio ninasema tu kwa kuwa neno uzalendo ni zuri, bali maisha na kazi zake zinadhihirisha hilo.
Mpaka mauti ya kusikitisha yanamkuta, Prof. Mwaikusa alikuwa akitetea suala la wagombea binafsi, kwani hiyo ndio demokrasia. Hili ni swala muhimu kwani viongozi tulio nao uwezo wao ni wa kutilia walakini, na hao wa upinzani vyama vyao vinasikitisha. Hilo ni jambo moja kati ya mambo mengi aliyofanya Prof. Mwaikusa. Tofauti yake kubwa na wasomi wengine, Mwaikusa alitumia usomi wake kupigania mambo ya haki katika jamii. Leo hii wasomi walio wengi ambao wamesoma lakini hawakuelimika, wamejawa na tamaa ya pesa.
Tanzania tunazidi kupoteza kizazi cha wazazi wetu walio wasomi na wazalendo. Jambo la kusikitisha zaidi, wakati kizazi hiki kinazidi kutokomea, kizazi chetu bado hakioni kuwa hii iwe changamoto kwetu kukamata usukani.
Wakati wengi wenu mnanunuliwa kwa masinia ya pilau na mvinyo, pamoja na ahadi za umaarufu wenye harufu, walio na misimamo ya kweli ndio hivyo tunazidi kuwapoteza. Majonzi na machozi hayatakuwa ya maumivu, kwani tunamlaza mzalendo wa kweli mahali pema peponi…
Amen.
I am A Fighter — by late Prof. Jwani Mwaikusa:
I was once a fighter,
A fighter of great prowess,
A fighter of great calibre.
“I am a fighter!” I shouted,
And before I had realised it,
I had won the fight.
My opponents gave way
And surrendered with fear
“You have won, ” they said,
And grim faced, they left.
Without another glance at me, they saw the fighter,
Carried shoulder high by cheering supporters.
“I am a fighter!” I shouted
But there was nobody to fight,
So I had to relax.
But how can a fighter relax
Except by fighting?
How can a killer repose
Except by killing?
How can a dancer recreate
Except by dancing?
I had to relax too,
I had to repose,
I had o recreate.
“I am a fighter!” I shouted
But my enemies were no longer there,
They had long joined the mocking audience
Looking at me with nobody to fight.
So
I turned grimly to my supporters
Holding me high in worship:
“I am a fighter!” I declared to them.
May he rest in peace. Tumempoteza gwiji wa sheria za kikatiba.
So sad,…tunasema Watanzania tunajivunia amani na upendo kati yetu…kwa njia gani labda??? kwa kuwanyamazisha wanaojitokeza kutetea haki za Watanzania wenzao wasio kuwa na usemi ???
Safari ni ndefu, lakini tutafika tu. Kama sio kizazi chetu hiki, basi watoto wetu…
Salamu za rambirambi kwa familia nzima ya Mwaikusa na wanafunzi wa Sheria UDSM.
Inasikitisha kwa kweli. Naskia jamaa waliingia nyumbani na kumuua kwa mapanga, binamu yake akataka kusaidia na yeye akauwawa, jirani akataka kusaidia na yeye akauwawa.
Jamaa hawakuchukua kitu chochote kile. Something is not right here? Jamaa lazima watakuwa wametumwa. Bongo tunakoelekea kunatisha….
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi na awape watoto wake baraka,msafiri na ammu nguvu kwenye wakati huu mgumu.
Amen!
Hii Habari imetuhuzunisha wanachuo, au wana mlimani wa enzi hizo. Nadhani tunazidi kupoteza wazalendo wasomi kwa kasi kuzidi kasi ya inayojaribu kuziba mapengo yaliyoachwa nao.
Habari za kuaminika kwa kiasi kikubwa, zinasema aliuwawa kwa kupigwa risasi. “Majambazi” hao walimpiga risasi akiwa ndani ya gari lake kabla ya kuingia nyumbani kwake. Baada ya milio ya risasi kusikika, ndio binamu yake alitoka kwenda kusaidia na yeye ndipo alipouwawa pamoja na jirani aliyejitokeza kujaribu kusaidi.
Huu ni msiba mkubwa. Pamoja najua kuna conspiracy kadhaa zimezagaa mtandaoni, nadhani ni vyema tusubiri upelelezi wa awali tuone utasemaje. Najua mazingira ya kifo chake yana utata kwa kiasi fulani, lakini tusibiri kabla ya kuhukumu, lakini hapo hapo hakuna kosa kuuliza maswali penye sababu ya kuuliza.
Nadhani kwa sasa tuwaombee akina Baraka na familia yote ya Mwaikusa.