A while ago we had fruitful discussions regarding education opportunities and life as a Tanzanian student abroad. Since such questions arise again and again especially on matters of financial aid and advice on study program choice, today and in the next few days we shall present here the views from Tanzanian students who are studying abroad with regards the above matters. This information is to help any Tanzanian high school student out there who is at the cross-roads and is contemplating university education abroad. In the end of the series we shall put a database of such FAQs in our resources page . Today we begin with Tanzanian students studying in Canada and Germany. (Please click the hyperlinked text for more information)
Name: Richard
Institution of study: Carleton University – Ottawa, Canada
High School: Aga Khan Mzizima Secondary School – Dar es Salaam
University study program: Aerospace Engineering
Kwanini ulichagua kusoma nje ya nchi? Program hii haipo vyuoni Tanzania?
Program yangu haipatikani Tanzania wala Afrika Mashariki na Kati.
Ni masuala yapi muhimu uliyozingatia wakati unatuma maombi katika chuo unachosoma sasa au pengine katika vyuo vingine ulipotuma maombi?
Nilizingatia kwa makini ni program gani nilitaka kusoma, gharama ya tuition na pia kama kuna uwezekano wa kupata scholarship.
Vipi masuala ya gharama ya elimu na maisha – scholarships zipo?
Scholarships zipo sema ni entrance scholarships ambazo zinatolewa kulingana na high school performance. Gharama ya elimu kwa mwaka wa masomo ni kama Dola za Canada 20,000 bila scholarship.
Ni changamoto gani ulikumbana nazo wakati wa transition kutoka maisha ya masomo Tanzania na hapo ulipo?
Challenge kubwa ni aina ya kazi zinazogaiwa na kiasi kikubwa cha kazi hizo nilizopata. Tanzania nilikuwa nimezoea kusomea mitihani tu, kulikuwa hamna push yoyote ya kufanya assignments maana zilikuwa hazihesabiki in the long run. Lakini huku kila kitu kinahesabika, jambo ambalo ni zuri maana inakutayarisha kwa mitihani vizuri na uelewa wa ndani wa masomo, ila kuna wakati work-load inakuwa kubwa kupita kiasi.
Ni yapi yanayohimizwa zaidi huko kuliko Tanzania, na ni yapi unadhani Tanzania tunahimiza na hauyaoni huko?
Mambo yanayohimizwa huku ni creativity na work-load throughout the year. Tanzania tunahimiza sana kusoma kwa bidii, cramming, na mazoea ya kujifunza kufanya maswali magumu. They all go hand in hand.
Je, mtaala wa elimu yetu ya Tanzania ulikusaidia vipi (kama kweli) katika mwaka wako wa mwanzo wa masomo hapo? Au ni juhudi zako binafsi?
Elimu ya Tanzania ilinisaidia sana mwaka wa kwanza hasa kwenye upande wa hisabati. Elimu ya Tanzania inahimiza kusoma na kujifunza mwenyewe mambo mengi, kwahiyo nilikuwa nimeshazoea kuji’challenge na maswali magumu hivyo sikupata shida sana mwaka wa kwanza.
Tueleze zaidi kuhusu mwaka wako wa COOP/internship?
Mwaka wa co-op ilinipa nafasi ya kupata field experience kwenye kampuni ya uhandisi. Mpango huu unamwezesha mwanafunzi ku’network na wahandisi katika fani yako na hivyo kuongeza nafasi yako ya kupata kazi baada ya graduation. I strongly advice anyone who is considering studying abroad to take this option if it is offered in their institution. Hapa Canada inakurudisha nyuma kwa mwaka mmoja, ila it is worth it; hasa ukiweza kupata kazi nzuri unayotaka. Also, it allows the student to explore the industry to know what he likes and doesn’t like.
Utamshauri nini mwanafunzi aliyesoma A-level na kutihaniwa na NECTA kuhusu kutuma maombi katika chuo chako?
1, Asome kwa bidii maana elimu ya Tanzania ni ngumu zaidi, na hivyo wakati wa kutuma maombi anashindana na waliosoma elimu ya IB au GCSE ambazo kwa maoni yangu ni marahisi – admission office hawatofautishi mitaala. 2, afikirie kwa makini sana ni program gani anataka kusoma majuu. 3, Akae kitako na mzazi kuulizia uwezo wa familia utakaoweza kugharimui masomo hayo. Jambo hili ni muhimu sana kwani wazazi wengi bongo hawako tayari kutoa financial information zao kwa watoto, lakini ni muhimu kujua ni vyuo gani utakavyotuma maombi au kufahamu namna ya kujaza fomu za financial aid au kama utahitaji scholarship.
Swali la kizushi: Una mpango wa kurudi Tanzania?
Kurudi kwangu Tanzania inategemea na kama nitapata kazi katika field yangu huku. Nikipata kazi huku, Tanzania nitakuwa ninarudi kutembea tu.
Pengine nataka niongezee kwamba, ukipata admission usifikirie ya kwamba elimu na maisha ya huku yatakua marahisi, hata kama mwaka wa kwanza ulikuwa mzuri. Kwani elimu inazidi kuwa ngumu kadri miaka inavyokwenda – speaking from personal experience; ukidharau elimu, grades zako zitashuka.
* * * *
Name: BK
Institution of study: Jacobs University – Bremen, Germany
High School: Kibaha Secondary School – Pwani
University study program: Electrical Engineering and Computer Science
Kwanini ulichagua kusoma nje ya nchi? Program hii haipo vyuoni Tanzania?
Kwa sababu nilitaka degree ya kimataifa, ambayo ingeniwezesha kufanya kazi sehemu yoyote duniani. Program hii haipo Tanzania, ila kuna degree mbili tofauti, yaani B.Eng Electrical Engineering, na B.Sc Computer Science lakini si kama program moja.
Ni masuala yapi muhimu uliyozingatia wakati unatuma maombi katika chuo unachosoma sasa?
Internationality, limitless opportunities upon graduation, and financial aid.
Vipi masuala ya gharama ya elimu na maisha – scholarship zipo?
Kuna financial aid, ambayo inajumuisha scholarship, grant na/au mkopo. Gharama za maisha hapa ni kubwa. Kuna kazi za kufanya campus/off campus ambazo zina kiwango cha masaa unachoruhusiwa kufanya kazi. Kama ukipata kazi maisha hayawi mabaya. Kama sivyo, pengine itabidi nyumbani (familia na marafiki) wakusaidie. Ukichangamka unapata kazi.
Ni changamoto gani ulikumbana nazo wakati wa transition kutoka maisha ya masomo Tanzania na hapo ulipo?
Kozi za Sayansi ya Tarakilishi (programming) kwa kweli zilisumbua akili yangu mwanzoni. Changamoto za kimaisha haikuwa shida kuzoea.
Ni yapi yanayohimizwa zaidi huko kuliko Tanzania, na ni yapi unadhani Tanzania tunahimiza na hauyaoni huko?
Utafiti hata kama ni mwanafunzi wa undergraduate, pamoja na ujenzi wa sifa za kiuongozi wa baadaye unahimizwa sana. Nadhani nyumbani Tanzania hakuna azimio la wazi la nini tunataka kufanya kielimu.
Je, mtaala wa elimu yetu ya Tanzania ulikusaidia vipi (kama kweli) katika mwaka wako wa mwanzo wa masomo hapo? Au ni juhudi zako binafsi?
Kwa masomo yangu hapa mtaala wa nyumbani naweza kusema haukuwa na msaada sana. Style ya kufundisha hapa ni tofauti sana, na masomo yanaangalia sana teknolojia ya sasa na ya kesho. Haya yote hauyapati nyumbani.
Utamshauri nini mwanafunzi aliyesoma A-level na kutihaniwa na NECTA kuhusu kutuma maombi katika chuo chako?
Aombe. Aje aone, ajifunze na arudi kujenga nyumba yake (maana Tanzania ndo nyumbani, na kila mmoja atajenga nyumba yake). Mambo ya kuzingatia wakati wa A-level ni kuwa na matokeo mazuri darasani, pamoja na ushiriki katika shughuli nje ya darasa katika mambo unayoyapenda (uongozi unapendwa zaidi). Haijalishi ni michezo au vyama vya kielimu – vyote ni muhimu wakati unatuma maombi katika vyuo vya huku.
Swali la kizushi: Una mpango wa kurudi Tanzania?
Nitarudi nyumbani.
* * * *
More information regarding admission procedures (requirements, deadlines) to the above universities is found here:
If you are an East African student studying abroad and would like to take part in this project, drop a line at: joji (at) vijana (dot) fm.
Mimi pia ni Mtanzania niliyesoma Carleton [University] kuanzia 2002 – 2005 na 2007 – 2009. Na aliyosema Richard yote ni kweli. Kitu cha muhimu sana ni kuiweka elimu mbele. Ukiwa kule, kuna mambo kibao ya kukuchanganya akili. Mambo ya kazi, mambo ya ku-enjoy maisha na kutoka-toka sana, lakini inabidi ukumbuke ni kwanini umeondoka Tanzania kwenda nje; kwa ajili ya elimu. Ukishakumbuka hayo, itakusaidia sana kuwa focused. Of course maisha ya huko ni magumu kama tu yalivyo Tanzania. Hata kama wewe ni tajiri [kiasi] gani, lazima uelewe kuwa masomo yanazidi kuwa magumu kadri uendeleavyo. Kwahiyo inabidi uiweke elimu mbele!
Joji, hili ni wazo zuri sana. Shukrani na hongera kwa ubunifu.
Pia, shukrani ziwaendee kina Richard na BK kwa kujitolea kukupa majibu na maelezo mazuri.
Nisingependa mjadala ubadilike na kugeuka kuwa mitaala ipi ya elimu ni bora zaidi, lakini ningependa kutoa maoni yangu kwa kifupi.
Richard amesema:…hivyo wakati wa kutuma maombi anashindana na waliosoma elimu ya IB au GCSE ambazo kwa maoni yangu ni marahisi – admission office hawatofautishi mitaala.
Nadhani watu wanaochagua wanafunzi wanajua tofauti za IB, GCSE na A-levels. Wanajua kuwa 7 kwenye IB sio sawa na A (au hata A* ya A-levels na GCSE). Ila naweza kukwambia kwamba, mara nyingi wao wanaangalia mwanafunzi yupi anaonekana atafanikiwa na kufanya vizuri zaidi kwenye masomo chuoni na kuhitimu kwenye muda unaotakiwa. Kama mtu niliyepitia IB, nina uhakika 7 ya somo fulani IB “High Level” ni kipimo kizuri zaidi kuliko A*.
Mara nyingi wanafunzi hushtuka baada ya ile transition ya kutoka A-levels hadi chuoni. Wanafunzi wa IB hawashtuki sana; kwasababu yale mambo ya kuwa na work-load muda wote ni kawaida. Na pia, ubunifu na kusoma kwa kujitegemea (yaani, kufanya utafiti) hutiliwa mkazo.
Urahisi (wa IB) unaoengelea sijui ni upi. Sio vema ku-generalize, kwasababu huwa inategemea sana unasoma masomo gani na level gani. Nilifanya Math HL, Physics HL, Computer Science HL, Psychology SL, English A1 SL, Spanish SL… Nilikuwa kwenye timu ya shule ya mpira wa miguu (tizi mara mbili au tatu kwa wiki), tulikuwa tunatembelea vituo vya watoto yatima n.k. Kusema ukweli sitakuelewa ukiniambia IB ilikuwa rahisi.
Pia, kama BK alivyosema, watu hawaangalii alama za mitihani ya mwisho tu. Kwa mfano, mtu mwenye rekodi nzuri kwenye transcript yake na pia labda alikuwa kwenye timu ya shule ya mpira (au alikuwa anachora, au anatembelea, anapanga na kuongoza watu kwenda kutembelea vituo vya watoto yatima atakuwa) ana nafasi kubwa zaidi kuliko mtu mwenye straight A* kutoka kwenye mitihani ya mwisho.
Maisha ya chuo (hasa ughaibuni) ni ya kipekee sana na huhitaji motisha na skills fulani (kama mwananchi tu wa kawaida; kushirikiana na watu kwenye masomo), ambazo bahati mbaya wanafunzi tuna muda mdogo sana kujifunza wakati tuko sekondari.
It’s all about access to information. SN unajua mwenyewe jinsi gani kila kukicha tunaulizwa na dogo fulani nyumbani au msela kuwa ‘umtafutie shule/scholarship’ ughaibuni. Wengi ni kuwa kweli hawajui taarifa kuhusu process za kufuata na hawafahamu waanzie wapi, au hawataki kuhangaikia wenyewe. Utaulizwa; “Tofili, ni nini?” (TOEFL) au “Nini? Esitii?” (SAT) n.k. Kwahiyo VijanaFM tutakuwa tuki’raise hili suala ili liwasaidie vijana wa shule wa sasa na wa miaka ya mbele. Iwe umesoma shule yoyote nchini Tanzania, tutajaribu kugusa suala lako – ikiwa unasoma shule “intaneshno”, vipaji au za wazazi – asikuambie mtu hauwezi.
Ingawa tupo wengi nje ya TZ tukisoma na wengine kwa bure (kupitia fianancial aid, scholarships) etc, still the flow of information to our peers back home is not sufficient. It may sound so trivial to most of us already in the system but imagine how hard it would have been back-in-the-day without that guidance councellor, a relative abroad, or friend abroad from whom we got that insightful tip on the application process. Kwahiyo hapa nia ni kusambaza taarifa bila kuzingatia kujuana, au kupendeleana, au background.
Hii sio kwamba tunaponda vyuo vya nyumbani, la hasha, bali ni muhimu pia vijana wa TZ kuwa na udadisi wa kuchovya nchi nyingine kielimu ili kupata exposure tofauti. Hapo mbeleni tukiwa na jeshi la wasomi waliosoma Korea ya Kusini, Australia, Egypt, Qatar, Spain, Belgium n.k ninadhani ni faida kubwa kwa TZ.
Mmeelezea mengi kuhusu watu ambao ndio wamemaliza a-level karibuni. Je, vipi kuhusu transfer;kwa sisi ambao tayari tupo vyuoni tukichukua degree au diploma? Process zinakuwa zimekaaje?
Kuhama chuo mara nyingi inakuwa ngumu. Lakini nafahamu watu wachache ambao walihama bila matatizo.
Mara nyingi chuo kinaangalia mambo uliyosoma na kuamua kama itakubidi usome kozi nyingine zaidi au la (baada ya kujiunga). Kabla ya hapo, huwa wanaangalia mambo yote muhimu kama mtu anavyo-apply kwa ajili ya undergrad. studies – transcript(s), resume, SATs na TOEFL scores (kwa vyuo vya Marekani na baadhi vya Ulaya).
Ujue, watu wanasitisha masomo vyuoni na nafasi hujitokeza. Lakini sijawahi kusikia hata chuo kimoja kinachotangaza nafasi hizi. Kwahiyo, kama una nia na unadhani una nafasi (hata kama ikiwa ndogo sana) ya kupata admission, usisite kuwasiliana na watu wa admission office wa chuo husika/unachotaka.
Kwasababu uko kwenye pool tofauti au ya kipekee kidogo, ni muhimu sana ukituma e-mail ikiwa na supporting documents i.e. excellent CV, transcripts na labda ueleze kwa ufasaha unasomea nini. Kama wakikupenda na ukawapa sababu ya kuwa na imani ya kuwa utafanya vizuri, watakwambia uwatumie vitu zaidi.
well done Joji for this blessing idea for those who need back home.
good job Richard and BK for ur ellaborations.
Great site. A lot of useful information here. I’m sending it to some friends!
Nashukuru sana kwa hizo taarifa nzuri.Mimi nahitaji kusoma master scince in computer science or finance and accounting. vip PROCEDURES za ku’apply’ na kupata financial aid scholarship huko ujerumani au canada?
@Luta: Check out our Education Resources page (http://vijana.fm/resources/education/), and if that doesn’t help you may need to look into individual school procedures. If there is a way we can assist further, don’t hesitate to let us know! All the best.
how are you?? napenda sana kusoma nje ya nchi katka masomo ya biashara na uhasibu xo unaweza ukanpa muongozo kuhusu vyuo ninavyoweza kusoma kwa scholarship au kwa bure coz nasikia nchi za scandnavia elimu yake n bure ata kama ni raia wa kigeni… kwa sasa nko diploma
Shukurani sana joji