Mashambulizi ya wahamiaji Afrika Kusini

Mwandishi wa habari wa Al-Jazeera aliamua kwenda Afrika Kusini kufuatilia bendi moja ya muziki kutoka Kongo, ili aiambie dunia habari njema… bahati mbaya mambo yakageuka!

Kama wewe ni mgeni hapa Vijana FM, jua kwamba filamu kama hizi zimejaa tele. Bofya hapa ili uone nyingine kutoka sehemu mbalimbali Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 3 Comments

3
  1. Tanzania ina wakimbizi kama laki mbili hivi – na majuzi tu tumesikia wengi wao wakipewa uraia. Ninafurahi upuuzi huu wa mauaji haujawahi kutokea, despite umasikini wa watu wetu na elimu ndogo ya wananchi. Never say never, ila ninadhani ni vigumu mno kutokea TZ. Nchini Afrika ya kusini wana matatizo kwa kweli. Yaani mnawaua waafrika wenzenu? Wengi wao wanatoka katika nchi zilizowasaidia kipindi kile cha ‘apartheid’. Hili tatizo ni la kizazi cha sasa cha SA, na ni kampeni kubwa tu ya kuwapa shule wananchi – that’s it. Perhaps educating the masses won’t be enough, they seriously need to get their actions right – social engineering could help, waje Tanzania wafundishwe mawili matatu. On top of that, bado kuna ‘bifu’ la chini chini kati ya wazungu na watu weusi. Sielewi bado.

  2. Hii ilivyotokea na mimi nilisema hivyo hivyo, hivi wanawezaje kuwauwa Waafrika wenzao, wale waliowasaidia kipindi kile cha apartheid. Nakubaliana na wewe kuwa hiki ni kizazi kipya, lakini apartheid yao ya sasa ni umasikini na uendelezwaji wa kutowapatia vijana opportunities.

    Sasa kuna swala jingine, swala la wakimbizi au migrant workers kutoka nchi nyingine za Afrika. Wakati unapambana na mfumo ambao umekufungia nje, sasa unalazimika kushindana na mgeni kupigania opportunities hizo chache, hapo lazima mwenye kwao anze kupandwa na hasira. Tanzania tungekuwa na vijana wengi kutoka nchi nyingine wanakuja kugombania kazi ambazo ni chache sana hata kwa sisi, utaona msuguano. Lakini sidhani kama tutafikia walipofikia hawa wenzetu, lakini kila kukicha tunachoma wezi moto, hivyo roho ya ukatili wa namna hiyo Watanzania tunayo.

    Sasa tusubiri jumuiya ya Afrika Mashariki itengemae alafu tuanze kufurikiwa na watu kutoka nchi kama Kenya, Uganda n.k. Hapo hapo wachina nao wameanza kubanana na vijana wa biashara ndogo ndogo, hivyo kuanza kuwakosehsa ridhki. Sasa hayo yote, itakuwa ndo yale ya haba na haba hujaza kibaba, sasa sijui kibaba chetu mwisho wa siku kitakuwa kimejaa nini..yangu macho..

  3. People are tired, hopeless,no means of wealth…no opportunities…in this century tusipokuwa na vita Tanzania,sijui…if the trend continues watu watapata hasira….Naomba Mungu tu..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend