Ze Utamu arudi kuwapangusa!

Na Msemakweli

Makala ya wiki iliyopita, ambayo ilikuwa inajaribu kuwabana na kuwapiga roba za mbao vijana wavivu wasiotaka kujifunza, nadhani ilitafsiriwa vibaya na baadhi yenu — wachache. Ilikuwa inawalenga vijana ambao wameenda shule, wakaelimika na wakapata ‘bahati’ ya kutumia mtandao na kujifunza madhara ya utandawazi kwa ujumla. Wewe msomaji ndio ulikuwa mlengwa haswa.

Sasa, kama wewe msomaji (ambaye nina uhakika ni msomi) ukiwa hutilii maanani mambo yanayotukabili vijana na nchi yetu, je, itakuwaje kwa vijana wenzetu ambao hawakupata nafasi ya kupata elimu?

Mimi ninaandika mambo kama ninavyoyaona; sitakupa maji ya muarobaini yaliyochanganywa na asali. Hapa unapata muarobini pekee; kujaribu kuondoa hayo maradhi ambayo nina uhakika yanasababisha matatizo kama haya kwenye nchi yetu kujirudiarudia!

Unadhani mioyo ya vijana wangapi iliongeza kasi ya mapigo baada ya kusoma kichwa cha hii makala???… Sisemi kwamba vijana wanatakiwa wawe siriazzz muda wote na kujadili mambo ya elimu, siasa, maendeleo ya nchi n.k. Lakini, binafsi sitakuelewa unapopata buku ya kwenda  internet cafe halafu unaishia kuangalia udaku tu. Angalia madude yako kwa dakika tano; pandisha mzuka. Zilizobaki tumia kusoma mambo yatakayokujenga kifikra au yanayokuathiri moja kwa moja kama kijana.

Sijui mara ngapi nilipokuwa cafe nilikuwa naona picha au kusikia sauti za ajabu ajabu kutoka kwenye tarakilishi za jirani zangu. Halafu watu haohao baadae wanakuja kukuuliza, “Dogo una bahati. Hivi ulipataje shule Mamtoni?” Upuuzi!

Kinachotuua ni visingizio. Kijana anaweza akapata hata sababu ya kujitetea kuangalia madudu kwenye mtandao. Mjadala kama huu ukija, mtu anakutolea mimacho tu kwasababu hajui hata wapi pa kuanzia. Tena usinikumbushe kuhusu Zain Africa Challenge!

Tutalaumu elimu, vizazi vilivyopita, malezi na siasa za ujamaa na mambo mengine lukuki, lakini sote tunapaswa kujiangalia kwanza. Mipaka ya nchi imeshafunguliwa, utake usitake. Unadhani watakaokuja kutafuta sehemu za kujishikiza Tanzania watakuwa na visingizio? Sijui Tanzania tungekutwa na mkasa kama wa Wahutu na Watutsi sijui ingekuwaje — tungepata visingizio vya karne mbili zijazo!

Hivi, unajua kuna ‘utani’ kuwa Wachina wengi wakifika kwenye mji mpya wanatafuta maktaba kwanza? Mi’ kusema ukweli hata sishangai ninaposikia pilikapilika zao Kariakoo.

Kisingizio kikubwa cha vijana au wasanii wa Bongo ni cha hati miliki. Hivi, umeshawahi kujiuliza: Ingekuwa vipi kama wangeamua kulifanyia kazi wenyewe? Kwa mfano, kila baada ya hafla au kutumbuiza, kila msanii angekuwa anatenga shilingi 50,000 zitakazoenda kwenye mfuko wa kutetea haki zao. Kuanzia kutangaza, usambazaji wa kazi zao na hati miliki? Nina uhakika mpaka sasa hivi wangekuwa tayari wana kampuni yao/zao za kurudufisha kaseti na CDs.

Ras Inno alishatupa hekima na busara zake kuhusu matatizo ya haki miliki na kurudia tena kwenye semina ya Kili Awards na kutoa mifano halisi. Unajua nini kilifanyika baada ya jamaa kumaliza kuongea? Wadau walipiga makofi tu na mawazo yake yakafa kifo cha mende!

Mwishowe, wasanii wanakuwa na ghadhabu na wanaishia kutukanana! Anti-virus.. Sijui nianzie wapi? Kusikiliza ile mixtape ni kama kuvuta bangi tu. Stimu inapanda wakati unaisikiliza (tunajiita ‘wazeeeeiiiiya’). Baada ya siku mbili tatu unagundua ilikuwa upuuzi tu. Mixtape nzima hakuna mawazo mbadala ya nini haswa kifanyike ili matatizo yasijirudie!

Pia, nani atakuheshimu na kusikiliza kilio au matatizo yako ukitumia lugha chafu? Bongo? Fikiria tena. Sasa hivi mtu akinipa ushauri mzuri, halafu mwishoni akanitukana, bila shaka hisia zitachukua mkondo na nitabakia kujiuliza au kukasirika na kuhoji, “Kwanini amenitukana!??”

Labda baada ya kusoma makala chache zilizopita utagundua kuwa matatizo yanayotukabili yanajirudiarudia. Iwe kwa vijana au Serikali. Na tunaonekana hatujifunzi kabisa na nadhani hilo ndilo tatizo kubwa.

Ulipata kuperuzi ile ripoti kuhusu kwanini nchi za Afrika hupoteza hela nyingi kwenye sekta ya uchimbaji wa madini? (Taarifa kuhusu jinsi wawekezaji wanavyokwepa kodi Tanzania inapatika kwenye ukurasa wa 38.) Ukiperuzi zaidi utajua kwanini majina tu ya kampuni zinazowekeza nchini ndio yanabadilika. Kwa maneno mengine, mtu yoyote yule ambaye anataka kutengeneza hela ataona upenyo kwenye sheria zetu zinazowabana wawekezaji.

Kuna wakati nafikiri bora tu wangetuachia madini yetu tuchezee gololi, drafti au bao!

Kwa wale ambao mmezoea udaku na hamjui wapi pa kuanzia ili kupata taarifa muhimu, jaribu kutembelea tovuti zifuatazo: Wavuti, Shurufu Anasema, Udadisi, Swahili Street, Mzee wa Changamoto, The Mikocheni Report, Dar Sketches, Zed Books, Hapa Kwetu, Marafiki wa Vitabu, Taifa Letu, Zitto na Demokrasia na Soma Book Cafe.

Bila kusahau, dondoo za Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki zinapatikana hapa.

Kwaheri!

FeDë Nestory, shukrani sana kwa kutupa ruhusa ya kutumia katuni zako kwenye makala hii.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 11 Comments

11
  1. Karibu sana Vijana FM.

    Pia shukran kwa makala njema!

    Mi si mzuri ktk maandishi, ila ningependa kuchangia kwa ufupi. Kwamba makala ya juma lililopita inaweza kuwa mojawapo ya jibu la makala hii, kwamba uvivu ndio chanzo cha yote haya. Wengi wetu tunapopata matatizo hatutafuti njia ya kusuluhisha na kudhibiti, badala yake tunatafuta njia ya kujitetea na kujiona hatuna makosa.

    Na wa kulaumiwa si wazazi, walezi au kiongozi fulani. Ni sisi wenyewe na dawa ni sisi wenyewe, tusiishie kuongea tu bali walimu kwa kile tunachokijua kwa wenzetu. Na isiwe kwa mtandao tu hata “face to face” pia. Ni hayo tu kwa sasa.

  2. Kwa kusema ukweli, SN anasema ukweli kabisa. Unfortunately, watu tutasoma tutapata stimu halafu baada ya wiki ya mihangaiko ya kazi tunasahau. Mimi nitatoa mfano, hii ishu ya Mtikila kutaka kugombea uraisi kama mgombea binafsi, watu wengi tulishabikia hii ishu, hata mimi nikiwa mmoja wapo mwanzoni.

    Ila baada ya muda, nikasema ngoja niitafute katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania niangalie inasemaje. Ni kweli katiba yetu tukufu inasema :-

    Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama:-

    39-(1) (c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

    Bofya hapa kusoma zaidi.

    Sasa, sijui kwanini Mtikila anaendelea kukimbizana na hii kesi. Ila katiba nayo inajichanganya kidogo ukiangalia 21-(1) and 21-(2).

    Yah, ila nachotaka kuonesha ni kuungana mkono na SN. Sometimes ndio cheki udaku, lakini it does make a difference ukifuatilia ishu zinagusa taifa lako. Vijana ni taifa la leo, sio kesho. A little bit of effort goes a long way.

    Mimi sijawahi kuiona katiba ya nchi maisha yangu yote, nilikuwa naisikia tu. Just last month I googled and read it, kufuatilia ishu za uchaguzi and n.k.

  3. Thanks for the wake-up call, Bata. Ngoja nami niitafute katiba. Ni ngumu kusoma yote, ila kuna vipande vinavyostahili kusomwa. Lakini, katiba kama ilivyo haistahili kubadilishwa? Mbona Tanzania hatuna ‘referendum’ kuhusu masuala makuu ya kitaifa kama wenzetu Kenya? Wataalamu wa sheria msaada…..

  4. Nimekuwa nalia na vijana wa kitanzania kila siku. Kweli kuna haja kubwa ya kubadili namna ya kufikiri na kutenda, kama kweli tunataka umasikini na hali zetu kimaisha kuwa ni wimbo wa kale. Bado taifa linashindwa kupiga hatua kwa sababu vijana ambao ndio nguzo kuu ya kuleta na kuishi falsafa za mabadiliko wapo kwenye dimbwi zito la mawazo yasiyoleta tija kwa kizazi cha sasa na chaa baadae…..

    Sijui tunakwenda wapi. Hii ni rai yangu;hatujachelewa bado. Mshike mwenzako mkono na tubadilike.

  5. Shukrani kwa maoni; hasa kwa kutuletea katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania!

    Ile kuperuzi tu vitu au taarifa muhimu inasaidia sana, ili baadae ukikutana na tatizo au jambo fulani angalau utajua wapi pa kuanzia. Baada ya hapo utajua ni vitu gani haswa (vya maana) vinavyokuvutia.

    Ukifuatilia mijadala muhimu kwenye mitandao ya Wabongo, utashangaa mtu anaitwa ‘genius’ kwasababu tu amekaa kitako akasoma na kuelewa jambo fulani; kisha akawasilisha maada in a certain comprehensive way. Sio dongo kwa mtu au kikundi cha watu fulani, ila wahusika wanajua ukweli kwamba mambo wanayoongea ni ya kawaida, lakini hadhira haijui hiyo.

    Na matokeo yake ni kushindwa kuwa na midahalo au mijadala ya maana — kwasababu watu hawana taarifa, misimamo au itikadi tofauti…

    Kwenye mjadala uliopita nilijifunza mengi sana!! Na nitashukuru mijadala kama hii ikiendelea. Hakuna mtu anayejua kila kitu, na kusoma taarifa muhimu, kujenga fikra husaidia sana kwenye kutatua matatizo.

    Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania inapatikana hapa [bofya].

  6. This is a much better article as far as I am concerned. It is easier to make a clear point when one sticks to one or two examples and also give recommendation for solutions. But I still want more articles with ideas even if dreams for now; but we need ideas on how to solve the problems.

    Another thing that we all seem to forget, is majority of youths and the general population are uneducated yet they have carried our country for years. My point is, we should focus on the general public rather than the educated few.

    And then there is a question of who do we consider to be educated? majority people who spend most of their time on facebook and other social networks are students of different levels. Tanzania as country has very few educated people (as a percentage of general population).. But all that should not derail your point, however the mere that we have kids or people who have gone to school does not mean we have educated Tanzanians.

    Bottom line, discussions are great, only if they are not just a hobby. Action speaks louder than volumes. Lets herald the successful young Tanzanians and maybe others will be inspired.

  7. Ninakuelewa. Lakini ukifuatilia mifano/makala nilizotoa (kwenye makala zote mbili) utaona kuwa waandishi na wachangiaji wengine walishajadili kwa kina; na wachache tu ndio waliouliza maswali ya msingi na hata kutoa mapendekezo. Kwa maneno mengine, hakuna kitu kipya kabisa — nilichofanya ni kama kuunganisha mambo yote yaliyonigusa kwenye wiki kadhaa zilizopita na kutoa mtazamo wangu.

    Ninachosema ni kwamba watu hawajui jinsi kutafuta taarifa muhimu. Na taarifa fulani zikipatikana, watu hawajui jinsi ya kufikiri na kujadili kwa kina. Sababu? Kila mtu ana ‘visingizio’ vyake.

    Kinachonikereketa ni ile hali ya matatizo fulani kujirudia kila baada ya muda. Ambayo inamaanisha – kwa namna moja au nyingine – hatujifunzi kitu… Na nadhani vijana wenzangu mnaliona hilo.

    Pia, hii sio “hobby” tu. Vijana FM na watu wanaotusaidia wana malengo makubwa. Hii tovuti inatumika tu kuwakutanisha watu. Muda muafaka ukifika tutajaribu kuwafikia vijana wengine kwa njia ya newsletter ambayo itakuwa inasambazwa bure nchi nzima (ikiwa na makala kama hizi)! Kwahiyo, nadhani ni muhimu kupata mawazo tofauti kutoka kwa watu mbalimbali.

    Mwisho, napenda kuwaambia kuwa kila mtu anaruhusiwa kutuma makala au taarifa ambazo anadhani zitawasaidia vijana [submit (at) vijana (dot) fm]; wasilisha halafu wahariri watakusaidia kurekebisha mambo mawili matatu.

  8. Hii makala imenichekesha sana!Yaani very interesting.In fact nadhani UVIVU utaendelea kutula sisi vijawa wa kizazi hiki.Yaani nimependa hiyo sehemu inayosema washikaji wanakuuliza umepataje hiyo nafasi ya kusoma mamtoni ha ha ha….ebana that’s very interesting!

    Kwa kawaida watu wanafikiri scholarships na nini ziko automatic yaani you just press a button na mara huyo una-ticket ya ndege na fees ya kusoma mamtoni.Ukiwatumia some important links waangalie they dont even bother.Ukisema wafanye some tests kama TOEFL au IELTS wao wanaona shida ku-invest pesa kwenye hilo ila watu hawa hawa wanatumia zaidi ya $100 wakati wa weekend….vijana wa Tanzania tuamke…

    We need to start investing kwenye mambo ambayo tunataka yatokee kwenye maisha yetu.Hakuna accidents zitakazotokea na kutuletea neema maisha mwetu…tupigane kuelekea tunapotaka kwenda….

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend