Vijana wanachama wa YUNA (Youth Of United Nations Association) mkoani Kilimanjaro wanategemea kufanikisha kongamano la vijana litakalohusu ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu Oktoba 2010 na mapambano ya vijana dhidi ya rushwa wakati wa uchaguzi.
Kongamano hili lenye manufaa kwa jamii nzima ya Watanzania linatarajiwa kufanyika tarehe 21 Agusti, 2010 katika ukumbi wa Kilimanjaro Cranes uliopo Moshi Mjini.
Lengo la kongamano hili ni kuwahamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za Uchaguzi Mkuu kwa kuwa vijana ndio nguzo kuu ya Taifa!
Vijana wanapaswa kushiriki kikamilifu katika:
- kampeni ili kuweza kutambua kiongozi sahihi
- kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
- kupiga vita vitendo vya rushwa katika kipindi cha uchaguzi
- kuwa waelimishaji kwa raia wengine juu ya umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi
- kuchagua viongozi wenye sifa kwa manufaa ya Watanzania kwa ujumla
Washiriki wa kongamano hili:
- Wanachama wa YUNA wanafunzi (sekondari na wanavyuo)
- Wanachama wa YUNA wasio wanafunzi (wahitimu wa kidato cha sita na vyuo)
- Vijana wasio wanachama wa YUNA
Washiriki wasio wachangiaji:
- Wanasiasa
- Waandishi wa habari
- Viongozi wa Serikali
- Walezi wa YUNA na asasi nyingine za kiraia
Kongamano litaendeshwa kwa lugha ya Kiswahili na litakuwa katika muundo wa mdahalo; ambapo kutakuwa na washiriki watakaopewa fursa ya kutoa maoni yao, kujenga hoja, kupinga hoja na kufanya marekebisho ya baadhi ya hoja zitakazotolewa.
Shukrani kwa Japhet Joseph kwa kutuletea ujumbe huu. Na timu ya Vijana FM inawatakia kila la kheri kwenye kongamano!
Shukrani kwa VijanaFM Team.