Na Mkunde Chachage
Leo katika pitapita zangu nikajikuta nimefika kwenye kimondo cha Mbozi, Mbeya, kinachodaiwa kuwa ni cha nane (8!) kwa ukubwa duniani na kimoja cha vivutio vikubwa huku Mbeya. Cha kustaajabisha ni kwamba hakukuwa na hata kibao kinachoelekeza jinsi ya kufika huko!
Yaani, hiyo sehemu haitunzwi wala kuboreshwa hata kidogo kuweza kuvutia utalii. Sidhani hata kama kuna ulinzi mahali hapo. Nilipouliza wahusika, waliniambia kuwa Serikali imechelewa kuboresha sehemu hiyo, lakini wana huo mpango.
Kweli kimondo kilichogunduliwa karne ya 16 na kufanyiwa utafiti karne ya 19 kimeshindwa kuchukuliwa kama kitu muhimu kinachostahili kuiweka Tanzania yetu kwenye ramani ipasavyo!?
“…lakini wana huo mpango…”. Kwa mipango tu, tuko juu!!!
Ukifikiria chap chap, kipindi hiki nchi yetu ikisuasua kutoa ajira kwa vijana, hapa labda kungepatikana ajira za watu sio chini ya kumi (za kudumu); na hata zaidi ya kumi na tano za muda — kujenga uzio, kujenga ofisi, kuweka mlinzi, kuweka vitabu na vijizuuu (vyenye picha nzuri na data za kisayansi) kwenye ofisi ndogo hapo kwa ajili ya watalii… Halafu, hii yote baada ya muda itapatia nchi yetu pato la maana tu.
Vitu vingine ni kutekeleza tu, sio lazima kuwa na “mipango” isiyo na mbele wala nyuma…
Hapana serikali yetu haina hela ya kuzingushia fence wire kwenye hili lijiwe lililotoka angani, kwanza hatujui limetoka anga gani na lilitupwa kwa makusudi au vipi!
Mabilioni yaliyopo wacha yatumika vyema kujenga na kukarabati nyumba za wakurugenzi wa TANESCO, BOT, nyumba za waheshimiwa mawaziri n.k.! Kwanza serikali ikizungushia fence hapo raisi wetu JK anaweza kukosa hela za nauli kwenda kumuona Obama au David Cameron! Sasa si itakua kichekesho wajameni?
Hela zilizopo ni kwa ajili ya matumizi ya maana tu, kununua mashati, kanga, vilemba na fulana za kijana, waheshimiwa wetu wanazihitaji hizo kuvaa na kugawa kwa washabiki wake!
Halafu mnakuja na hizi za kujenga fence, kwani hamjui BMW za raisi zinahitaji hela? Au yale ma NISSAN PATROL NA VX mnafikiri yanapatika bure? Yana cost si chini ya 200m/- kila moja! Sasa tutayanunua kivipi kama tukizungushia fence wire hapo?
Msimsumbuesumbue JK, kwanza kachoka na kampeni ya kutaka kuendelea kuwa raisi, nyie wenyewe mmeona kadondoka leo, halafu mnataka mambo makubwa kama haya ya fence wire! Bure kabisa nyie!!
Mkunde, nimefurahi kusoma report yako. Nafikiri kuta vitu kadhaa ambavyo ni muhimu kabla hatuja anza kufikiria kuhusu mambo ya utalii. Lazima tuanze na research katika eneo hilo na katika vijiji vilivyo karibu kusudi tuweze kuandika survey report. Pia kunahitajika plan, hii plan inabidi ionyeshe jinsi gani hili eneo lina muhimu kwa mazingira, watu na nchi yetu, na pia nini kitatokea kama tusipo kitunza. Tukisha pata plan naweza kuandika grant-proposal. Hii itatusaidia kupata fedha za kufanya mabadiliko, pia itatusaidia kushirikiana na serikali, scientists, na organizations. Nafikiri inabidi kulete ufahamu kuhusu Mbozi mashuleni na kwenye jamii. Kuna mambo mengi zaidi yanayohitajika….
Inapendeza; tuache kulalamika.. watu mlioko Mbeya, mnadhani mawazo ya Ruth yanaweza kutekelezwa? Mko huko kwa muda mrefu au kuna watu ambao wanaweza kuwasaidia?
Sasa kama hiko kimondo tunakishindwa kukitunza, je, yule mjusi/dinosari wetu aliyepo Ujerumani tutaweza kumtunza kweli?
Chambi, karibu sana Vijana FM. Naona leo umeamua kuperuzi kila sehemu.
Niko mzigoni sasa hivi, lakini hili swali lako limenichekesha sana… Hahahahahaha!
serikari ya wilaya hicho kimondo niutarii tosha ambao unaweza kuingizia wilaya mapato mengi sana hivyo wekeni utaratibu mzuri ili Mbozi ijulikane zaidi