The Chinese Investment in Africa has increased in the past few years. Their presence in the continent cannot be overlooked or even missed. I am sure the Western countries have realized that there is a new sheriff in town. I personally look at this as the Scramble for Africa Part II, although I am not yet sure if that’s a good way to look at it or not.
After watching the video, do you think we should be worried, as Africans, or should we continue to embrace the Chinese investment? I am sure if this same question is asked to a politician, an economist and a common man, the answers will obviously be different, but their perspectives on this issue will be an interesting one. Tanzania is not immune to this Chinese invasion, but at the same time, what do some of these Chinese investors really think of Africa and Africans?
Now shsssss…a moment of silence for Africa.
Thanks to Katebomz blog for sharing the Chinatown, Africa documentary.
Ati why do you think this is happening when the Western world is still hurting from the financial crisis? Glad y’all brought this up, because this is a scramble for resources, and if us Africans aren’t smart enough to hold on to what is ours, you might as well call this the Slave Trade II.
Nimevutiwa na hiyo documentary kwani inaeleza upande ambao mara nyingi hauonyeshwi na ‘western media’. Upande kuhusu ahueni wanayoleta wachina katika bara letu.
Binafsi ninadhani uwepo wa China Africa ni jambo zuri, ingawa hii inalingana na priorities nchi inazoweka kuhusu maendeleo yake. Je, nchi inataka kujijenga ili ijitegemee hapo baadaye? Au inataka kupewa ‘make-up’ tu ya chap-chap ambayo ikifutika baadaye itahitaji mchina aje aifanyie ‘re-makeup’? Investment zinavyofanywa na China Afrika ni wa aina hii ya pili.
China watawajengea barabara, reli, n.k lakini katika kipindi hicho chote cha ujenzi ukuaji wa viwanda na huduma vya wazawa haupigi hatua yeyote ya maana. Waache walete wafanyakazi wao basi, ila basi wasingekuwa wanakuja na kila bidhaa ya ujenzi ambayo ingeweza hata kupatikana nchi au nchi za jirani. Wangejaribu kuinua viwanda vya ndani – hadi rangi kweli inaletwa kutoka china? Kama bidhaa haipatikani Angola, si wa’import kutoka Congo, au TZ? Namna hii wangehakikisha viwanda vya kanda wanapojenga vinakuzwa, na hata kiteknolojia ya nchini humo ikiimarika.
Ila basi tu, wengi tunataka kuona maendeleo SASA. Na ninaelewa kwa nchi kama Angola iliyopitia mengi ya kutisha, hili ni muhimu. Ndio maana ninadhani wachina wanaruhusiwa kufanya biashara kwa jinsi watakavyo bila vipingamizi.
Je, baada ya miaka 15 hizo reli, vifaa vya hospitali, barabara zikiwa hoi na kuhitaji matengenezo tutatoa wapi rasilimali za kulipia? Hizo pesa/rasilimali tutakazopata kutokana na ubora wa miundombinu za wachina, je zitatosha kulipia ukarabati wa reli na barabara zinazohitaji ukarabati? Kipindi hicho maliasili zetu za chuma, uranium, mafuta au dhahabu zitakuwa zimeshakwisha kwahivyo tutakuwa hatuna uwezo wowowte wa kuzitumia kama transaction.
Kwa kweli nakubaliana na wenzangu hapo juu.
Unaweza kuutazama huu ushirikiano wa China na nchi za kiafrika kwa angle mbalimbali.
Inawezekana “the west” wana kijicho na donge kuwa China is getting more and more influence, maana biashara kati yao na sisi Africa inazidi kuwakuza China kiuchumi.
Ila ukiangalia na “the west” nao, kwa sasa wako hoi, ule mtikisiko wa kiuchumi kwa kweli umewawach ahoi kishenzi, wanasema wame recover, lakini bado sana. Wanatangaza tu kuwa wako poa ili shares na market isiendelee kutetereka.
Kwa upande wangu mie naona China kushirikiana na China ni poa tu, kasheshe yetu huwa hatusomi mikataba au tunaisoma lakini 10% huwa ndio inatuangusha, waafrika hasa tukiwa viongozi, maliasili ya nchi haziwekwi kipaumbele kabisa.
Tatizo lingine ni kama wadau walivyosema hapo juu, viwanda vyetu vitumike ku supply bidhaa kwenye ujenzi au maendeleo haya, kama hakuna kiwanda basi kianzishwe kiwanda, kila kitu kinawezekana.
Ila tuutazame huu ushirikiano kwa angle zote, ni mzuri ila una walakini ambao unaweza kurekebishwa kiurahisi.
Ujue jamaa wako maji ya shingo, wanahitaji rasilimali kutoka kila kona ya dunia ili kuweza kuendesha ile idadi ya watu. Kama tungekuwa makini na hizi maliasili zetu, tungekuwa na cha kusema na nguvu ya hoja kwenye mikataba na China… Lakini ukimsikiliza yule Mchina anayefanya madili Ghana, dah, kazi ipo.
Yaani lazima kutakuwa na watu ambao watachokonoachokonoa na kutibua kila kitu kwasababu tu ya ubinafsi wao! ‘Wanauzi.’
Kitu kingine ambacho labda nimeshawahi kusema wiki chache zilizopita: Chinese are hustlers! Tutasema mpaka tutachoka, lakini kama tusipoanza kuchangamka na kuyavalia njuga haya mapambano, nadhani tusahau…Mipaka inafunguliwa kila siku. Jamaa wanaingia kwenye mji, wanatafuta maktaba kwanza (ulizia wanaoishi Ulaya). Waafrika wengi tu wangesita kuingia kwenye jangwa la Kalahari. Lakini umeona jamaa wakilalamika? Wameingia jangwani; hakuna vyoo, hakuna nyumba, hakuna maji lakini wametimiza kilichowaleta. Na wamepata hata mabinti wa “kuponea”! Mimi kama kijana ninayetaka kuona watu wakipiga mzigo kuanzia asubuhi hadi jioni, nadhani kuna mambo ya kujifunza kutoka kwao (ukiacha kuponea kwa mabinti vijijini!).
Nani zaidi au bora kati ya watu wa Magharibi au Wachina? Nadhani nitakuwa nina mawazo tofauti na baadhi yenu (kwasababu na mimi niko kwa watu nabangaiza maisha). Kama tu tungekuwa na kiongozi mzuri, anayewaelewa Wachina na kujua sehemu ya kuwabana na kujaribu kuwafaidisha wananchi wengi wa kawaida, nadhani tusingekuwa tunalalamika.
Lakini, pia, tujiulize, hivi wangapi tuko tayari kusitisha tunachofanya, kujitoa mhanga, kwenda vijijini kwa miaka miwili au mitatu kutimiza azma fulani? Je, tuna haki ya kuwalaumu Wachina kwasababu tu wao wako tayari hata kuishi jangwani miaka mitatu?
(Najua kuna watu wataosema labda wananchi wa Angola hawakupewa nafasi ya kufanya kazi jangwani. Lakini hapa nazungumzia ile attitude towards hard work. Na hapo ndipo hata viongozi wetu wanapotuangusha pia. Hivi vitu vidogo vidogo vinasema vitu vingi sana kuhusu sisi na viongozi tunaowachagua.)
Kwa kumalizia tu, Wachina tunaowaona Afrika wengi wao wameshindwa na ushindani China na Asia kwa ujumla…
Fantastic response SN. Damn you now I do not have anything add!
Anyway, ni kama wazee msemavyo, hawa wachina ni wahangaikaji, ni juu yetu kuwabana hawa wachina ili nasi tufaidike.
Kidogo yale mambo ya kukaa kijiweni kupiga zogo, kupenda kukaa chini ya mti kusifia watu walivyolipua madili na kuwa matajiri, au kusifia majambazi, kinachoniuzi na kuniumiza ni ile baada ya ajali, ambapo watu hukurupuka na kwenda kukomba mali za waliopata ajali, yote hayo ni matatizo yetu ya kukaa kusubiri vya bure, je ni sababu watu hawana kazi? Au ni uvivu? Au ndo maisha yetu bongo yalivyo sasa?
Inasikitisha jinsi tunavyolala, wakati wageni wakija wanasema na tunawaona wanapata utajiri tulioukalia!
Mie inasikitisha sana.
Mawazo mazuri, lakini mimi nigependa kuwatazama Wachina na jicho la machale, manake hawa jamaa mhhh!!. Watu wanaweza kudai kuwa, wanaleta ushindani, lakini ushindani upi kama bidhaa zao ni za ubora wa chini. Nadhani sote tunajua simu za wachina zilivyo. Je, hizo dawa zao za kuongeza makalio, na mengine mengi, nasikia mpaka kandambili zao zina madhara.
Mimi wasiwasi wangu ndio huo, kuwa tunakuwa dampo la bidhaa zenye madhara, eti kwakuwa ni bei rahisi, basi tena. Watu wanasemaga hivi, cheap things are very expensive. TBS wako wapi?, au ndio wafanye watakavyo kwakuwa kuna dili na 10% kati yao na wakubwa.
Tatu, ukisoma vizuri hiyo makala ya Khai, utaona kuwa, machinga taratibu wataanza kuwa kwenye hali ngumu. Sasa kama kazi hizo za kuuza vitu vidogo vidogo nazo zinachukuliwa na wageni, vijana hao walio wengi wataenda wapi?
Kwa upande wa uchumi, watu wanaweza kusema, oh well hiyo miundombinu wayayojenga, itabaki kwa miaka na miaka hivyo tuwavumilie tu kwa miaka kadhaa mpaka mikataba yao itakapokwisha. Hiyo ni kweli, lakini tunahakikisha vitu wanavyotujengea vina ubora? Au wanashikizia tu ili kesho kutwa tuwaite tena kuja kukarabati?
Hao jamaa wako tayari kufanya lolote kuhakikisha wanauza vitu bei chee, manake nilipata kuona documentary moja nikaishiwa na hamu. Huko kwao, wanakula kila kitu, literally, yaani you name it, they eat it. Sasa kuwa ambitious si kitu kibaya, lakini ya hawa jamaa inatisha, manake wao ni for whatever the cost, by any means necessary..
“Msije mkababaishwa kwamba wawekezaji Wachina wana lengo la kuwanyonya na kuwanyang’anya ardhi Waafrika. Kinachotakiwa ni mpango mzuri wa kujadiliana nao na kuweka mfumo mzuri kwa manufaa ya kiuchumi,” alisema Mkapa baada ya marais wastaafu wa nchi za Afrika kumaliza mkutano wao Jijini Dar es Salaam jana.
“Jambo la muhimu nchi za Afrika zinapaswa kuchunguza na kujua ni mwekezaji gani ambaye ana uwezo wa kuleta mapinduzi ya kiuchumi haraka na kuwaletea wananchi maendeleo, na siyo kuangalia ni nani watashirikiana naye,” alisema Mkapa.
Suala la Wachina limekuwa ni wimbo kwetu kila siku, na zaidi imekuwa ni propoganda za hao mabepari waliotunyonya tangu mababu zetu na utumwa juu; wakitufanya sisi kama ni wanyama. Ni hizo hizo propoganda zao baada ya kukosa ushawishi kwa nchi nyingi za Afrika wakati wakiona China inazidi kujipenyeza kila siku.
Mabepari hawana lolote na siku zao zinahesabika sana — maana 19th century ilikuwa ni ya Europe, 20th ya Amerika na sasa ni ya Asia (China,India etc.) — kitu ambacho hakipingiki hata kama wakisaga meno. Juzi tumeona jinsi China ilivyoiacha Japani na kuwa taifa la pili kubwa zaidi kiuchumi duniani baada ya USA. Hivyo ni ukweli usiopingika kuwa hao mabepari matumbo yako moto na nchi zao hazistawi kama ilivyokuwa zamani kama nchi nyingi za Asia na Afrika.
Kama ni suala la kuwekeza mbona hao wa magharibi wapo kila nchi na watu huwa hatusemi? Au tulishawazoea sababu wametutawala tangu mwanzo na kutuachia uhuru (ulio na katiba yao; nashukuru wenzetu Kenya wameliona hilo na kuamuwa kuwa free at last); wakati kila kitu ni faida kwao, hayo hatuoni?
Kama wakiongea hao wa magharibi nadhani hawana hoja yeyote.
Kwa upande wa wananchi wa kawaida kulalamika hilo ni suala lililo wazi na tatizo sio Wachina (jamani tuwe wawazi, tusiwe wanafiki), bali tatizo ni hao viongozi wenu mnaowachagua kila siku hali mkiona hawasimamii mikataba ya kumwezesha mwananchi wa hali ya kawaida. Hapa kunatakiwa kuwe na mazingira mazuri ya kumwezesha mwanachi au machinga aweze ku-compete, lakini sio kuwafukuza au kuwakimbiza Wachina.
Jamani sijui kuna mtu kati ya wanaosoma hizi makala ameshafika Guanzhou? Nadhani anaweza akaelewa naongea nini hapa. Ukiwa kule nadhani kila baada ya hatua mbili ni Muafrika, huo mji mpaka unaitwa African City na kuna wengi tu Waafrika wanakaa illegally (wengine wanauza CD, DVD’s etc; kazi ambayo inaweza ikafanywa na Wachina. Mbona hawafukuzwi?). Naamaanisha kuwa Muafrika yupo kila sehemu, kwanini Mchina kuwa Afrika ni nongwa?
Tatizo letu sisi ni wazembe na waoga kushindana katika kila kitu; leo tunawasema Wachina, juzi mlikuwa mnalalamikia Wakenya, kesho sijui Waganda… then? Katika ulimwengu huu watu kama hao nadhani ni chachu kubwa kwetu walau tuamke — maana tunapenda sana kuongea ila vitendo ni sifuri (watu hawafanyi kazi kila ofisi watu wazembe na wanaonekana wameridhika kama sijui ni wafalme vile)! Hata hao Wachina mkiwakataa hayo maeneo yanaweza kaa hata miaka mingine 50 bila kuendelezwa lolote. Je, bora lipi?
Tufike wakati tuwe na ufikiri mkubwa sio kushabikia tu hao mabepari. Hapo juu nimejalibu ku-quote Mh.Mkapa alipokuwa akiongelea kuhusu masuala hayahaya ya ardhi na propoganda za mabepari.
[Edited: Dr. Mallaba, maoni yako yamehaririwa na kupangwa vizuri tu; hakuna kilichopunguzwa au kuongezwa. — Mhariri]
Mjadala bomba.
Ila kutoka kwenye mjadala huu, sikuweza kujizuia na kutamani raisi wetu JK awe anazunguka Tanzania yetu at least twice a year. Maana kama anaweza kufanya hivi kwa sasa wakati wa utafutaji wa kura, why not iwe tabia, at least twice a year?
Sasa atasema diary yake haitamruhusu, lakini si kweli, ni kwamba sie wananchi hatujamtaka awe anatutembelea, hasa kwa gari, maana ndio ataona hali halisi, kama ni barabara, afya, shule za watoto wetu, umeme, maji na means of communications.
Ila naona kwangu its just another wishful thinking, it will never happen nor will they think of it!
Kwake raisi, ndio itakua fursa kujua kazi na maendeleo ya wawekezaji, kama wanasaidia na kutunufaisha au la.