Kama wengi tunavyojua, madini ya tanzanite yanapatikana nyumbani kwetu tu. Filamu ifuatayo (ya mwaka 2006) inaonesha hali halisi ya mambo yalivyokuwa yakiendelea kabla ya wachimbaji wadogo (wananchi) hawajafukuzwa au kuondolewa kwenye migodi huko Mererani.
Watoto wadogo – waliokuwa wakiitwa “manyoka” – ndio walikuwa wakitumiwa kwenye shughuli chungu ‘zima; kuanzia kuingia mashimoni hadi kuchekecha vumbi na kutafuta madini kutoka kwenye vifusi.
Jionee mwenyewe jinsi wadogo zetu walivyokuwa wakiteseka… ili mradi tu mkono uende kinywani.
Kama filamu ikileta kwikwi, bofya kwenye ‘kitufe’ cha mviringo cha kijani kilichopo hapo juu kwenye player (If the video does not play, click on the circular green button on the player).
Serikali yetu inatia aibu sana,sasa watu kama hawa utawaambia nini kuhusu Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.?!!