Mambo gani haya

Lekchara kaniboa kichizi leo! Yaani nilikuwa nina lekcha moja tu, lakini sikumuelewa prof wala nini. Kichwa kilikuwa kinauma kinoma… Nadhani keroro za jana usiku hazikunisaidia. Kama kawaida, usiku ukiwa mnene, lazima leo nipate gambe tena.

Sina mzuka wa kuongea na mtu — yaani hata kutoa hi kwa waliopendeza siwezi. Kugeuza shingo kuwakagua ninaopishana nao imekuwa adhabu. Jua la utosi linanipiga makonzi, kwahiyo bora nitulie kidogo kwenye internet café kabla ya kwenda maskani.

Baada ya kulipa, kuketi na kuanza kutumia kompyuta, kitu cha kwanza ninachoona mbele yangu ni homepage: Globu ya Jamii. Yaani kampeni mpaka huku? Rangi ya bluu inamezwa na ya kijani! Haiwezekani, labda Ankal ni kada wa CCM! Na kuna watu wanatoa maoni yao; kwa maneno mengine, wanampaka Issa.

Ila hiyo sio shida yangu,naamua kuzama kwa mdogo wake. Yale yaleeee. Huku ni kijani kitupu pia. Mambo gani tena haya?

Hisani ya Juma Mtanda via http://www.wavuti.com

Hivi, Wabongo wangapi wanatumia mtandao? Hizi kampeni zinalenga kina nani hasa? Wazamiaji na wabeba boksi hawatapiga kura — angalau mwaka huu.

Na leo kila sehemu kuna nyuuuz za Dr Slaa kumnyang’anya mtu mke. Dah, watu wanaongea kama vile wake za watu ni mizigo. Yaani unaweza kumpokonya mtu tu mwandani wake mtaani. Ingekuwa hivyo, sasa hivi mi’ ningekuwa nimeshamuoa Faraja Kotta zamaniiii!

Ngoja nipandishe mzuka kabla ya kwenda nyumbani. Huu ndio muda wa kucheki skillzz zangu za kutumia Google. Maujanja ni kujua key words; na leo najaribu “Ze Utamu arudi.” Kama zali vile, Ze Utamu amerudi kutupangusa! Nabofya link ya kwanza kabisa

Mambo gani haya? Inanipeleka kwenye hiki kijiwe kinachoboa kinoma.

Ngoja niende kuanza kufaidi weekend… Sh*t! Kumbe leo Jumanne.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 3 Comments

3
  1. tehe he, kijana, leo umepata wapi ‘msuba’? rudi darasani! nhe he!
    Leo Jumanne uko hivi, utatoboa Ijumaa kweli? unalo!
    Siasa si hasa, bali visa na mikasa, mwanzo-mwisho!

  2. Theme song. Check.
    Clothing line. Check.
    Own energy drink/ liquids. Check.

    CCM ‘got swagger. I am just waiting for that CCM fragrance line 😀

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend