Tarehe 4 Septemba, 2010, Metty Nyang’oro wa Radio Mbao alipata fursa ya kumhoji mjasiriamali Modesta Mahiga kwa kirefu. Ni mahojiano ya kina yanayogusa nyanja mbalimbali nchini Tanzania. Ukiacha suala la ujasiriamali kwa ujumla, Modesta alijadili kwa kirefu mambo yafuatayo:
- Fikra za Watanzania (kwenye suala la kutafuta ajira)
- Juhudi na kuwajibika
- Jinsi ya kuleta mabadiliko nchini
- Kufanya mambo ya ziada kujiendeleza
- Mfumo wa elimu
- Uwekezaji
- Vipaji vya vijana
- Na mambo mengine chungu mzima…
Nakusihi, ukipata muda sikiliza mahojiano haya:
“Tanzania ndani ya miaka 10 (ijayo) itakuja kubadilika… kuwa kitu cha ajabu.”