Sophia, a young mother

Dada Sophia Hamisi, ana miaka chini ya kumi na nane, tayari akiwa ni mama katika umri huo mdogo. Simulizi ya maisha yake inaakisi hali halisi ya wasichana wengi katika jamii yetu.

Baada ya kutazama hii video, niliishia kujiuliza maswali kadhaa.

Je, msukumo wa kufanya ngono mapema miongoni mwa vijana wengi ni kutokana na kubalehe tu au mazingira magumu yanayowazunguka, kama anayoishi dada Sophia? Huku ushawishi wa marafiki ukipata upenyo kwa urahisi kurubuni mwelekeo wa kijana.

Pili, dada Sophia anazungumzia suala lake kama tu ni “ajali kazini,” na ni hivi ambavyo vijana wengi huchukulia masuala kama haya. Hii dhana ya vijana kuchukulia mambo mazito kama haya kirahisi-rahisi, ni ubishi wa ujana au ni kutokana na kukosa matumaini katika maisha yao, hivyo kufanya maamuzi bila kujali?

Tatu, kwanini jamii hupenda kunyoshea vijana vidole pale mambo yanapokwenda mrama? Hasa ukizingatia ni jamii hiyo hiyo ambayo huwa bubu katika kumwandaa kijana na maisha ujana!

Suala la nne na la mwisho ni hili la vijana wa kike kutupiwa lawama pale wanapopata mimba, huku watoto wa kiume wakiachwa huru kukwepa majukumu yao. Kwanini kusiwe na utaratibu ambao utawabana vijana wa kiume pindi watakapowapa ujauzito wasichana? Kwani, hata kama kijana akikimbia, familia yake italazimika kusaidia katika malezi. Nadhani hii itasaidia familia za watoto wa kiume kuhakikisha vijana wao wanakuwa makini, na hata kuwa makini zaidi na ufanyaji wa ngono zembe.

Shukrani nyingi zimwendee kaka Dotto Mnyandi kwa video hii.

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 3 Comments

3
  1. Yote yaliyozungumziwa hapa ni ya msingi kabisa na yanayohitaji watedaji wa kweli kuyabadilisha kwa kuhakikisha sheria zinafuata mkondo wake na wazazi/walezi wanapata mafunzo au kumbushio la kuwafunda watoto wao kama ilivyokuwa jando na unyago, ikiwa mila na desturi hizo zilifutwa kwa kuwa zilikuwa si sahihi, badala ya kufuta na kutokuweka mbadala wake, waliofuta wangehamasisha njia nyingine ya kuelimisha vijana wanaokumbana na mihemuko ya mwili na wasijue namna ya kutuliza ashki zao na kujiepushana ngono zembe zinazowaharibia maisha.

    Amenikumbusha kisa cha Elisa (sp) – Tandale/Uwanja wa Fisi

  2. JK: “Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao”

    NIPASHE. Juni 2010

    Rais Jakaya Kikwete amesema matukio ya mimba kwa wanafunzi wa kike nchini yanasababishwa na viherehere vya wanafunzi wenyewe.

    Rais Kikwete alitoa kauli hizo katika kijiji cha Kisesa wilayani Magu jana wakati akihutubia wananchi kwenye ufunguzi wa mashindano ya ngoma kwa kabila la Wasukuma; ngoma ambazo zinajulikana kama ‘Bulabo’.

    ” Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule,” alisema Rais Kikwete wakati akijibu risala ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Bujola, Fadha Frasince Sandhu, ambaye alisema ujumbe wa mashindano hayo mwaka huu ni vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

    Kwa mujibu wa Rais Kikwete, suala la zinaa kwa bianadamu, siyo la lazima hivyo binadamu anaweza kujizuia ama kujikinga kwa kutumia kondomu.

    ” Na kwa bahati mbaya shughuli ile (uzinzi) binadamu hana dharura nayo, hivyo unaweza kutumia kondomu kama unaona kwamba huwezi kutii amri ya sita ama huwezi kuwa mwaminifu katika ndoa yako,” alisema kauli ambayo ilizua vicheko miongoni mwa watu waliohudhuria ufunguzi huo. Aliwashauri wananchi watakaoshiriki kwenye mashindano hayo wawe na tahadhari dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.”

  3. dah!!, hata sijui nianze wapi na hii comment ya JK. Is this man serious, yaani kweli hatuna kiongozi, that comment not presidential, no one will ever imagine such a comment can come from a president of a country.

    Ina maana, hajasoma tafiti, manake inaonyesha amekurupuka. But I am guessing, such a comment can only come from a person who has failed to come up with a program and a plan to combat the high infection rates za Hiv/ Aids among youths. Yaani haoni kama umasikini na maambukizo ya ukimwi yanakwenda hand in hand?

    Nadhani Mh. hana tena sera wala game plan, its high time we move on Tanzanians

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend