Vijana FM inatumia Crowdmap, chombo kilichotengenezwa na Ushahidi, kukusanya taarifa, mawazo na uzoefu wakati wa Uchaguzi Mkuu Tanzania. Ni matarajio yetu kwamba chombo hiki kitawapa jukwaa watu kutoa taarifa, maoni, kuanzisha mijadala na kueneza ujuzi wa mchakato wa uchaguzi na matukio mbalimbali.
Taarifa zinaweza kuwasilishwa kwa njia tatu:
- Kwa kutuma barua pepe: TZelect (at) gmail (dot) com
- Kwa Twitter hashtags #TZelect au #uchaguzitz (Shukrani Jamii Forums)
- Kwa kujaza fomu kwenye tovuti
Msisite kuwasiliana nasi mtakapohitaji msaada.
Imetengenezwa na:
Always inspired by vijana.fm’s creativity and positive forward thinking.
Nimefurahi sana na ninapongeza juhudi za VijanaFM kushirikiana na watu mbalimbali na kuipa changamoto sekta ya TEKNOHAMA.
VijanaFM crowdmap ni wazo la mbolea kabisa!
Vijana hongereni sana! Nilikuwa na hamu sana kuona teknolojia za Ushahidi zinaanza kutumika Tanzania. Kwa mwendo huu mwisho wa kura kuibwa na kuchakachulliwa umekaribia sana.
Nadhani kazi kubwa zaidi — ambayo ndio changamoto hasa — ni kuelimisha umma matumizi na faida za hiki chombo. Nimezunguka sehemu kadhaa kuangalia kama kuna mjadala au mwamko wowote ule; lakini inaonekana shughuli itakuwa pevu.
Kwahiyo, wenye nyenzo za kuelimisha umma (waandishi wa habari, bloggers, wana-taaluma n.k.), tafadhali tusaidiane.
Hongereni sana!!
Tunasonga mbele mpaka kieleweke. Vijana nimewakubali.
Huu ndio usomi, nawapa tano!
Kazi nzuri vijana FM. Tunahidaji sana mchango wa vijana katika kuleta mapinduzi ya kweli kwa njia ya habari ili kuharakisha kasi ya maendeleo kwa njia ya elimu habari.
Ushauri, tufanye kazi bila upendeleo, bila kujali itikadi au maslahi ya kikundi fulani cha watu, kwa njia hii tunafikiwa kulijenga taifa letu.
Ingawa kazi iliyoko mbeleni ni nzito kama unavyojua, ushauri wako umefika na wahusika (vijana watakaokuwa wanapokea ripoti mbalimbali) wataufanyia kazi.
Lengo hasa kama unavyojua ni kuwapa watu – hasa vijana – uhuru wa kuripoti matukio. Kwa mantiki hiyo, tutahakikisha tunafanikisha zoezi zima kikamilifu. Usisahau, ushirikiano wa watu ndio utaleta mafanikio.
Vijana ndio taifa la SASA, HONGERENI SANA, tupo pamoja
kila la heri
Great Initiative.
Quick question though. How is this meant to work? From details, i.e.:
Taarifa zinaweza kuwasilishwa kwa njia tatu:
1. Kwa kutuma barua pepe: TZelect (at) gmail (dot) com
2. Kwa Twitter hashtags #TZelect au #uchaguzitz (Shukrani Jamii Forums)
3. Kwa kujaza fomu kwenye tovuti
Perhaps it will be best to run a mock test and establish capacity and any technological or user issues so that these can be dealt with much earlier.
With technology there are bound to be issues unless fully tested and issues are known with “work arounds” in place.
I have added this link to my FB Note @
http://www.facebook.com/note.php?note_id=431556901516
Keep up the spirit!
Temu, wahusika wamejaribu kuripoti matukio mbalimbali tayari na kila kitu kilienda vizuri. Nadhani changamoto kubwa itakuwa ni kwa watu ambao watakuwa wanapokea taarifa, na sio teknolojia yenyewe — kwasababu imeshatumiwa kwenye nchi kadhaa tayari.
Ukitaka taarifa zaidi tembelea tovuti ya Ushahidi.
Shukrani sana kwa kuwataarifu wengine!
How is this being reported? Where are the published reports or how to access them?