Wiki kadhaa zilizopita tuliwataarifu kuhusu chombo tulichokitengeneza, TZelect — Chombo cha Ushahidi, ambacho kitatumiwa kukusanya na kujadili taarifa na ripoti wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Siku chache zilizopita tulipata ujumbe kutoka kwa vikundi kadhaa ambavyo vimeamua kutengeneza chombo kingine (kinachofanana na TZelect), Uchaguzi Tanzania, ambacho kitawezesha watu kuripoti kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi (SMS).
Vyombo vyote viwili, TZelect na Uchaguzi Tanzania, vinalenga Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika tarehe 31 Oktoba mwaka huu, na pia kufuatilia watakaochaguliwa katika kipindi kinachofuata hapo baadae.
Malengo haswa ya chombo cha Uchaguzi Tanzania ni kutoa haraka taarifa zilizoripotiwa na wananchi Tanzania. Na kwa upande mwingine, TZelect itakuwa inakusanya taarifa, maoni na mawazo; ni matarajio yetu kuwa chombo hiki kitawapa jukwaa watu — hasa vijana — kuanzisha mijadala na kueneza ujuzi wa mchakato wa uchaguzi na matukio mbalimbali.
Tunapenda kuwakumbusha jinsi ya kuripoti; kwa njia yoyote ile utakayotaka:
Jinsi ya kuripoti — TZelect
- Kwa kutuma barua pepe (email): tzelect (at) gmail (dot) com
- Kwa kutumia twitter na hashtags zifuatazo: #TZelect or #uchaguzitz
- Kwa kujaza fomu kwenye tovuti
Jinsi ya kuripoti — Uchaguzi Tanzania
- Kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS): 15540
- Kwa kutuma barua pepe (email): elections.tz (at) gmail (dot) com
- Kwa kutumia twitter na hashtags zifuatazo: #uchaguzi or #humanrightstz
- Kwa kujaza fomu kwenye tovuti
Kama unahusika au unajua miradi ambayo inatumia teknolojia kama hizi kukusanya taarifa na maoni kutoka kwa umma wakati wa uchaguzi, usisite kuwasiliana nasi ili kuangalia kama kuna uwezekano wa kushirikiana nao.
ahsanteni sana
Nice one. have shared at this http://www.bongoline.com/blogs/2/86/utapata-wapi-habari-na-taarifa-z