Je, yanayoripotiwa kwenye vyombo vingi vya habari yanatupa hali halisi? Au taarifa nyingi zinapindisha ukweli hapa na pale kutokana na sababu mbalimbali — hasa linapokuja suala la kuzalisha nishati kwa kutumia teknolojia ya nyuklia.
Kama unapenda kuelewa nini hasa kinaendelea, basi soma makala ifuatayo ambayo inachambua yanayojiri Fukushima kwa kurunzi la kisayansi zaidi; na pia kuwapa pongezi Wajapani:
Ukiacha hayo, kama mnavyojua, watoto huathirika kwa kiasi kikubwa kwenye majanga kama haya. Wajapani hawawaachi watoto wao nyuma — wanajaribu kuwaeleza nini hasa kinachoendelea kwa lugha nyepesi.
Mmoja wa Watanzania wanaoishi Japani ametutumia video ifuatayo ambayo inadhihirisha juhudi za jamii kwa ujumla kuwafundisha watoto kuhusu yanayojiri.
tuna uwezo wa kuweka nyuklia wakuu,hatuna tetemeko la ardhi bongo, tuna sehemu iliyokuwa tupu mbaaali na maendeo ya binaadamu,vp kama tukiwaita wajapani waje kutuwekea vinu huko ili tuwe na umeme wa kuweza hata kuweka treni za umeme ? mpo tayari ndugu zangu?
Mimi i’m very skeptical na nuclear energy. Isije ikawa kama yale ya BP oil rigs. If somethin goes wrong, the consequence are so severe if not irreversible. That worries me alot.
On the issue of nuclear waste,Many point out France not having problems with nuclear waste. They claim all of it is recycled and used. I asked a french friend of mine, this is what he replied
——————————————————————————————–
Actually the retreatment plant in Den Haag “recycles” ~ 1700 tons of used fuel. The first step is to separate the three main components: depleted uranium (95% of the total mass), plutonium (1% of the total mass), actinides (4% o…f …the total mass).
The actinides are responsible of more than 95% of the total radiation. These actinides are “neutralized” by (in French) “vitrification”. A glass polymer is doped with the actinides, which results in glass bars that are buried.
The plutonium is directly sent to France, where it is used in the synthesis of MOX (the fuel used in Japan, Sweden, and some French nuclear plants).
As about the uranium, it is slightly enriched (yield ~10%) and used also in MOX fuel.
So around 1450 tons of depleted uranium are sent “somewhere” (rumors say that it’s in Russia) in order to be stored and buried.
Whether France has problems for the waste storage isn’t clear.. Politics and corporations say that there is none. But mainly because most of the waste is sent abroad…
——————————————————————————————
If we end up with too much waste, maybe nuclear energy might not be sustainable. + costs to store the wastes. These nuclear storage wasters would be easy targets in times of war. I’m also thinking maybe some of this waste will be dumped somewhere in Africa. Considering how greedy our leaders are. You just never know!
It true that nuclear energy is the only viable solution for the energy problems in the near future. However, the risk is just too high. Without forgeting nuclear weapons, :-(. I guess science is a double edged sword.
Kabla ya kuweka hiyo mitambo tuhakikishe at least tuna mifumo ya kueleweka ya kupatiana taarifa.
Japan ina automatic system ya kutoa taarifa kabla ya tetemeko halijasambaa.
Vituo vyote vya tv hutangaza ‘tetemeko limepiga jitayarishe kutikiswa”
Simu zote za mkononi hulia alarm (kwa waliojiandikisha kupata huduma hiyo)
Miji karibu ya bahari hulia alarm kuwa taarifu watu kuwa tsunami linakuja wakimbie
Hiyo radiations taarifa inatumwa kila saa na namna ya kujilinda.
Watu wote wana masks, dawa, chakula cha wiki atleast na maji na wanaambiwa wahakikishe hewa ya nje haiingii ndani kwa kufunga madirisha na milango.
Kwetu tunaotumia milango ya kumbesa, chakula cha siku tunakitafuta siku hiyo hiyo, taarifa kuwa kuna leakage haijuulikani itatufika vipi sidhani kama tunaruhusiwa kibinaadamu kuwa na mitambo ya nyuklia.
Tukianza kuingiza kwenye equation, incompetence ya wataalamu wetu, vifaa chakavu vya jeshi, na kutokuwepo na ujuzi wa kukabiliana na dharura (refer to Gongo la Mboto), ni dhahiri kuwa hiyo technology na ipite mbali.
*Tanzania haisubiri natural disaster italitengeneza lake wenyewe. Utasikia jeshi lilikuwa likifanya mazoezi ya makambora yakakosea njia yakatua juu ya mtambo
Shaaban Fundi amekuwa akifuatilia kwa karibu uwezekano wa uranium kuanza “kuchimbwa” Tanzania. Sidhani kama kuna mikakati ya kutengeneza nuclear plants Tanzania. Ni nchi za Ulimwengu wa Kwanza ambazo zinahitaji uranium kwa udi na uvumba:
http://vijana.fm/2010/10/21/uranium-in-tanzania-resource-or-curse/
Tanzania hata tusifikirie kuhusu nuclear energy. Mradi wa Stigler’s Gorge tu umetutoa kamasi:
http://vijana.fm/2010/12/17/electricity-dearth-in-tanzania/
Bata, kukusaidia tu katika sehemu ambazo hizo taka za uranium zinatupwa, hizo nchi tunazifahamu. Ila ndio hivyo, habari zinazimwa; vyombo vya habari huchagua vitu vya kuripoti kama vyombo vya magharibi vilivyochagua nini hasa cha kuripoti kutoka Fukushima. Mambo ya propaganda hayo… Marekani wangeweza kudhibiti janga kama walivyofanya Wajapani, we wouldn’t have heard the end of it!
That’s all I was trying to say. Kwasababu Jumapili iliyopita magazeti yote ya Uingereza na Marekani yalikuwa yanasema “Fukushima Nuclear Disaster”… Sisemi kama watu hawajaathirika, ila ukipekua vizuri kidogo tu basi unapata picha halisi nini hasa kinaendelea.
Kwa kifupi tu, Wajapani wanahitaji moral support sasa hivi na wanastahili kupongezwa pia.
Tukirudi kwenye nchi ambazo ndio madampo ya Ufaransa na hata Uholanzi (Shell):
1. Ivory Coast:
http://www.who.int/ipcs/emergencies/ivory_coast/en/index.html
Hii ilizua kasheshe. Tafuta taarifa zaidi mwenyewe.
2. Somalia:
Chanzo cha ship piracy kilikuwa ni kujilinda… from nuclear wastes dumping
http://towardfreedom.com/home/content/view/1567/1/
Nyongeza tu: Ule mradi wa ITER ukifanikiwa baada ya miaka 50 hivi (nuclear fusion), uranium itakuwa haihitajiki tena. Lakini, kama nilivyowahi kusema, kuna politics ndani yake (man, I hate politics) na kuna manguli wa nuclear physics Ulaya ambao bado wako skeptical kuhusu project nzima. In other words, it works but the main challenge is to have that infrastructure to sustain it. But, Wajapani tayari wametuonesha hata hiyo nayo inawezekana!
Kuhusu ‘Tanzanian Nuclear Energy’, mimi ninadhani tusahau. Ngoja angalau miaka 50 ipite kwanza labda kizazi kijacho kitakuwa tayari kwa haya. Hao physicists wenyewe tunao? Kwa hesabu ya haraka haraka ninadhani nuclear physicists Tanzania hawafiki 6 (Ukimuhesabu Bilal)! 😀
Sita tu? Sasa, waliosomea hiyo kitu na ‘wanao-practice’ wako wangapi? Hawazidi wanne…
Kwenye haya mambo ya kuogopa au kutuatilia mambo ya majanga yanayoathiri mazingira na afya za watu nahisi tuna unafiki fulani. Yaani, kwa upande mmoja tunajali yanayotokea Fukushima, wakati uani kwetu watu wanateseka kuliko Wajapani, na wataendelea kuteseka bila sisi Watanzania au Waafrika kujali.
(Watu wa Ivory Coast waliandamana baada ya Shell kumwaga takataka zao na karibia mji mzima kuanza kuharisha… Sitaki kuwaambia watu walimfanya nini mmoja wa mawaziri walipomkamata mtaani. Hizo habari ziliripotiwa vipi nje ya Ivory Coast? Huu mjadala mwingine… Na inaonekana historia inajirudia kwenye hili sakata la uchaguzi.)
Ukiulizia kwa mfano wataalamu wa mazingira (bahari), watakwambia viumbe wengi wa bahari ya Hindi wanafurika Afrika Mashariki kwasababu ya uchafuzi wa mazingira unaofanywa kwenye pwani za Somalia, India, China n.k. It’s just connecting the dots.
Tumepost hapa visa kutoka Mererani, Niger, Geita, Mara Kaskazini na sehemu nyingine; binadamu akila heavy metals — iwe lead, chromium, zinc, cadmium, cyanide, ruthenium, au uranium — atakufa tu; na vizazi vitakavyofuata ndio hivyo tena… unaweza ukatafuta makala na picha kwenye mtandao.
Labda wengine watasema: hatuna usemi juu ya haya yote kwasababu coorporations zina nguvu sana. Lakini kuna visa vya ku-refute hiyo dhana. Sasa tunafanya nini? Au tufanye nini?
Msinielewe vibaya kwani kila mtu anaruhusiwa kuwa na mtazamo na maoni kuhusu vitu mbalimbali. Ila kuna mambo ambayo mtu anayejali anapaswa kufanya kitu kwa njia moja au nyingine.
Ile ishu ya Mara, watu wamechapisha picha tu halafu wakapotea.
Ujue, labda ndio hivyo nakua mtu mzima na kukubali hali halisi; kuwa labda hatuna final say.
Kwa upande mwingine, wenzetu wametuonesha kuwa inawezekana. Hyperkei alihoji hapa: Je, ikitubidi tuandamane kama Wamisri, wangapi hapa wataingia mtaani? Watu hatukujibu.
Na mimi huku nilipo niliulizwa swali hilo hilo (nikadhani jamaa katumwa na Hyperkei!). Nikajibu, ningekuwa Misri ningewaunga mkono vijana Tahrir Square. Lakini Tanzania kuna unafiki.
Jumapili njema.
By the way, while we are in “interesting” debates about Babu wa Loliondo, there have been rather significant delelopments on the Dowans front. Just saying…
http://tinyurl.com/4nqprjg
Tunajenga tabia halafu tabia zinatujenga.
Kuna na hili janga la e-waste zinazomiminwa Africa. Sijui serikali zetu linalochukuliaje hili.
http://www.independent.co.uk/news/world/africa/dumped-in-africa-britain8217s-toxic-waste-1624869.html
Pia nimeona vitu kama microwaves, fridges, TVs and computers zinazoingizwa kwa makontena na sisi wenyewe Watanzania tukisema ni vitu vya second hand kutoka nchi za Magharibi na kuuzia watu kwa bei nafuu.
Hivi vitu vingi havidumu zaidi ya mwaka, kisha vinatupwa tu ovyo. Tunahitaji kuweka regulations haraka kama hazipo.
Na hili la TV kuanza kutumia mfumo wa digital hivi karibuni, TV zote zilizopo kwenye market sijui tunampango nazo upi.
Wakati Tanzania inasema haina nia ya kuanzisha mtambo wa nyuklia, Kenya ipo njiani kuanzisha wake ndani ya miaka 10 ijayo uwe unafanya kazi. Wanafikiri kuuweka kwenye eneo lake la Bahari au ufukwe wa ziwa Victoria.
http://af.reuters.com/article/topNews/idAFJOE6AP0CR20101126
Nna wasi wasi kuwa tumejijengea tabia ya kutochukua hatua za mapema za kuzuwia mambo kutendwa, na matokeo yake ni majuto baadae.
Kwa kuwakumbusha tu, huko Japan walikoweza kudhibiti kwa kiwango kikubwa, maziwa na mchicha vimegundulika kuwa na kiwango kikubwa cha radiations kuliko kawaida katika eneo la kilomita 50 mbali na kituo cha nyuklia.
Kwa sisi tusiokuwa na mfumo wa kupima chakula, tutaweza kuangamia.