Vijana wa mwaka ‘arobaini na saba’ walikuwa wakitumia nafasi ya kujifunza stadi mbalimbali kupitia mpango wa Elimu kwa Njia ya Posta. Karne hii, kwa walio na access ya internet tungependa kuhimiza matumizi ya Elimu kwa Njia ya Puku. Katika miaka inayokuja Vijana FM inajipanga kuwa mwezeshaji wa aina hii ya elimu kwa ajili ya mazingira na mahitaji ya Afrika Mashariki. Ila kwa sasa, mtandaoni kuna rasilimali tele ambazo vijana tungependa wazitumie kuongeza wigo wao wa kielimu na maarifa. Rasilimali hizi zinazopatikana kwa njia ya video, na ni bure, zinatolewa na taasisi na vyuo vikuu mashuhuri duniani kwa ajili ya masomo binafsi ya wanafunzi.
Tutaendelea kuipigia filimbi KHAN Academy kwa kuwa tovuti hii ina ‘utirio’ ulioshiba katika kila mada utakayofikiria. Ukitaka kupata mandhari ya kidarasa, basi tembelea tovuti ya Chuo Kikuu cha California — Berkeley na kuperuzi mihadhara mbalimbali zinazotolewa na wahadhiri waliobebea katika nyanja zao — kwa mfano, kuanzia elimu ya Astronomy, Afya ya Jamii, Sheria za Hatimiliki mpaka Historia ya China! Zote utakumbana nazo humo. Bonyeza nembo zifuatazo kwa zaidi.
Tafadhali tembelea kurasa yetu ya ‘Resources‘ hapo juu ili kufahamu tovuti nyingine kadhaa za aina hii.
Tunapiga parapanda hii sio tu kwa wale walio vyuoni, bali pia kwa yeyote ambaye angependa kujiendeleza kimaarifa katika nyanja mbalimbali.
That is a very good initiative especially for research work.
NAHITAJI CHUO KINACHOTOA ELIMU KWA NJIA POSTA.