Wanasayansi wanaofanya utafiti kufahamu mbinu ambazo mdudu wa malaria (Plasmodium) anatumia kuepuka mfumo wa kinga wa binadamu hivi karibuni wamezindua mfululizo wa katuni wenye lengo la kusambaza ujumbe kwa umma kuhusu ugonjwa huo pamoja na jitihada zao za kisayansi. Katuni hiyo ‘MALARIA! The Battle Against a Microscopic Killer’ imeandaliwa na jopo la watafiti wa EVIMalaR na imezinduliwa rasmi wiki iliyopita mjini Heidelberg, Ujerumani katika kongamano la baiolojia ya mdudu wa malaria. Tafadhali peruzi kurasa za katuni hiyo ili upate uelewa wa jinsi gani mpaka leo hii hatuna kinga au dawa madhubuti ya ugonjwa huu. Waweza kujipakulia katuni hii au kuisoma mtandaoni hapa.
Previous ArticleAlfred’s Free Press