Kwa mliosoma Tanzania, nadhani mtaguswa mkiangalia filamu fupi inayoonyesha tofauti kati ya shule tatu za msingi za jiji la Dar es Salaam. Dhamira ya mtunzi wake, Allison, ni kuonyesha namna rasilimali za ufundishaji pamoja na mazingira yanavyotofautiana baina ya shule hizo yaani: Shule ya Msingi Bunge, Shule ya Msingi Montfort na Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege. Je, mbinu za ufundishaji baina ya shule hizo zinatofautiana? Na kama ndio, waweza kutabiri mafanikio ya wanafunzi hao kielimu kwa kuangalia mazingira ya ufundishaji wao?
Previous ArticleThe Day I Realized I Wanted To Change the World