Name: Imelda
Institution of study: Jacobs University – Bremen, Germany
University study program: Electrical and Computer Engineering
Tanzania School: St. Francis Girls Secondary School, Mbeya
Kwanini ulichagua kusoma nje ya nchi? Program yako haipo vyuoni Tanzania?
Nilichagua kusoma nje ya nchi kwa sababu nilitaka kuimarisha mtazamo wangu wa ulimwengu na kama ningebaki Tanzania nisingeweza kufanya hivi. Kuwa nje ya nchi naweza kubadilishana mawazo na watu toka sehemu mbali mbali na nimeweza kukua kimawazo kwasababu kila siku inaleta changamoto mpya.
Ni masuala yepi muhimu ya ulizingatia wakati unatuma maombi katika chuo unachosoma sasa au pengine ulipotuma maombi?
Kwanza nilikuwa natafuta uwezekano wa kupata udhamini (kifedha), halafu jambo la pili nililozingatia ni programu wanazofundisha.
Ni muda gani mzuri wa kuanza na maandalizi ya kutuma maombi ya chuo huko ulipo?
Inategemea na chuo kwa mfano chuo nilichopo sasa hivi, muda mzuri wa kutuma maombi ni katikati ya mwezi wa kumi na mbili wa mwaka kabla ya masomo kuanza. Cha muhimu ni kuacha muda wa kutosha wa kuomba visa maana kutegemea na nchi unayoenda, inaweza kuchukua muda kupata visa.
Utamshauri nini mwanafunzi aliyesoma A level na kutihaniwa na NECTA kuhusu kutuma maombi katika chuo chako?
Hakikisha unaweka bidii katika kila jambo ufanyalo na ni muhimu kujua kuwa si masomo tu yanayozingatiwa, michezo na mitaala mingine ya ziada pia inazingatiwa. Kwahiyo usitumie muda wako kusoma tu, jiunge na clubs, michezo na kadhalika.
Ni ushauri gani utampatia mwanafunzi wa A level kuhusu namna ya kujitayarisha na mtihani wa Standardized Assessment Test (SAT)?
Hamna njia nyingine zaidi ya kujiandaa mapema na kufanya mazoezi ya kutosha. Ugumu wa huu mtihani ni namba ya maswali unayopewa. Utakuwa na maswali mengi marahisi lakini muda ni finyu, kwahiyo ukiweza kupata past papers, fanya mazoezi ya kutosha ili ujitayarishe kujibu maswali kwa kasi.
Ni changamoto gani ulikumbana nazo kuhusu transition kutoka maisha ya masomo Tanzania na hapo ulipo?
Changamoto kubwa kwangu kama mwanafunzi wa uhandisi ilikuwa kuzoea mazoezi yanayochukua muda mrefu sana kutatua. Kitu kingine ni kuwa na kazi nyingi kila wiki, mara nyingi una muda kidogo sana wa kupumzika kwahiyo inachosha, usije chuo ukidhani itakuwa rahisi.
Ni yapi yanayohimizwa zaidi huko kuliko Tanzania, na ni yapi unadhani Tanzania tunahimiza na hauyaoni huko?
Nitaongelea uhandisi hapa Jacobs University. Hapa wanahimiza sana mafunzo kwa vitendo kwahiyo hatufanyi lecture tu. Tuna kozi za maabara pia ambazo tunafanya majaribio mbali mbali kwa kutumia vifaa maalum vyenye viwango vya kuridhisha. Hiki ni kitu muhimu ambacho vyuo vya nyumbani havihimizi na mara nyingi ni kwasababu ya ukosefu wa vifaa hivi vya majarabio na maabara zenye viwango vya juu.
Kuna Watanzania wangapi chuoni kwako? Kama hawapo wa kutosha unadhani tatizo ni lipi, kama wanaotoka nchi jirani ya Tanzania ni wengi zaidi?
Kuna watanzania watano tu hapa chuoni. Tatizo kubwa nafikiri ni ukosefu wa taarifa kwahiyo nianze kwa kusema naomba watanzania mtume maombi yenu hapa Jacobs University, kuna udhamini wa kutosha tu kifedha na programu za uhakika kwahiyo msisite kutuma maombi.
Vijana FM thanks Imelda for her enlightening contribution. I believe a student somewhere in the region will put her message to work. More Q&A of this kind can be found here.
Asante sana Imelda kwa majibu yako. Nimefurahi pia kuona jinsi vijana fm wanavyo jali maisha ya vijana wa kitanzania.
Hongereni sana