[From 24th August 2013]
Madai ya katiba mpya ni muendelezo wa vugüvugu lakutaka maendeleo chanya #ChangeTanzania #Katiba
— rahma bajun (@rahmabajun) August 24, 2013
Asasi ya kiraia ya Change Tanzania leo walikusanyika British Council mjini Dar es Salaam, kama baraza la katiba, kwa ajili ya kujadili na kutoa mapendekezo yao kwa tume ya mabadiliko ya katiba. (Kwa maoni yote bofya hapa)
Mwezeshaji alikuwa ni mwanzilishi wa Change Tanzania, Maria Sarungi Tsehai.
Waliochangia mada ni:
- Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Societies, John Ulanga
- Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria
- Mhadhiri wa chuo kikuu cha Tumaini na Mhadhiri mstaafu wa UDSM, Azaveli Lwaitama
- Mhariri wa Jamhuri, Deodatus Balile
- Mwanasheria wa Mahakama Kuu na mwanaharakati, Daniel Welwel
Tweets za kumwaga kuhusu Baraza la #Katiba #ChangeTanzania .. follow hashtags na @VijanaForum @rahmabajun @changetanzania
— Maria Sarungi Tsehai (@MariaSTsehai) August 24, 2013
Mapendekezo yote yatatolewa wiki ijayo, ila kwa ufupi baadhi ya vitu vilivyojadiliwa ni yafuatayo:
- Mawaziri wawajibishwe moja moja na sio kwa pamoja.
- Uwajibikaji wa viongozi kupitia Sehemu ya pili ibara ya 92 (4), Baraza la mawaziri likimshauri rais vibaya katiba lionyeshe kwamba wanatakiwa kuwajibishwa.
- Spika wa bunge asiwe mwanachama wa chama chochote cha siasa.
- Uraia na uraia mbili.
Maendeleo isipimwe kupitia infrastructure ila kwa maendeleo ya watu – John Ulanga #ChangeTanzania #katiba pic.twitter.com/eQzTUBRtKH
— Gaure (@Profesy) August 24, 2013
Teuzi zote za Vyombo vya Kuwajibisha zisitokane na Utashi wa mtu mmoja -Dr Lwaitama #ChangeTanzania #Katiba
— Vijana Forum (@VijanaForum) August 24, 2013
Dada Maria Sarungi akifunga Baraza la Katiba. Change Tanzania ni yako, yangu na yetu #ChangeTanzania #Katiba pic.twitter.com/9HB0H9Mb5j
— rahma bajun (@rahmabajun) August 24, 2013
This post was originally posted at Profesy’s Version on 24th August 2013.
Hakika naamini mmetuwakilisha vyema
Yani kabisa Samuel.