Na Wilbert Maridadi
Nyani mengia njamani, hali njema si njemani,
Wanyonge furahieni, mikono ngali shavuni,
Furahani wajembeni, kilimo ndo mwanzoni
Vibwengo waulizeni, hali mbona si shwari?
Mwatupamba kwa karafu, kwa hayo maneno rojo,
Jembe yatula minofu, uhuru shambani tambo,
Moyoni kwingia hofu, kwa mahubiri urimbo,
Vibwengo waulizeni, hali mbona si shwari?
Kilimo si kalamuni, kutwa wimbo mdomoni,
Kilimo si mabukuni, wenyewe mpo pombeni,
Mapori yavamieni, pembejeo twawapeni!
Sisi tumo mjengoni, kilimo tumekamia!
Nastaajabu ya Musa, kilimo kimo mjengoni
Kilimo yake katiba, wajembe watoe wazo,
Awatoa wasolijua, kwao ufupi kipopo
Vibwengo waulizeni, hali mbona si shwari?
Wilbert Maridadi ni mwandishi wa riwaya, Ushairi na Tamthilia katika uga wa Fasihi ya Kiswahili na hadithi nyingi ametoa katika magazeti, pia ni muandaaji wa kipindi cha ULUMBI katika redio Sibuka 94.5 na Wimbi la lugha.
Hali mbona si shwari? Nimelipenda shairi…