Na Wilbert Maridadi
Ni usiku mmoja
Ulimea moyoni
Uling’ang’ana moyoni
Ulijenga makao
Ama kweli mtambazi uking’oka mtini humea!
Dunia leo si kama zamani
Leo hunena mapenzi hayana woga
Ni usiku mmoja tu!
Uliacha kovu moyoni
Kovu la chungu-tamu
Kovu lisoacha taswira moyoni!
Kovu la mpwito wa huba
Kovu la ukimya uso mfanowe!
Hakika ulimea moyoni
Ni usiku mmoja tu…
Nimelipenda hili shairi –
Inakufanya ufikirie mtunzi anaongelea nini, halafu unavuta taswira ya yaliyokusibu mwenyewe.
Regrets. Longing. Loss. Pain.
Kwenye maneno machache tu, hisia kibao zinakuja.
Asante mshairi.