Maswali matano na Adam A. Duma

Adam A. Duma ni mwazilishi shiriki wa SmartClass Tanzania, Afisa Mkuu wa utendaji SmartClass Tanzania. Tumepata nafasi ya kuzungumza nae jinsi ugunduzi wake wa “SmartClass” unavyowasaidia wanafunzi kipindi hiki wakiwa nyumabani kujikinga na COVID-19.

1. SmartClass ni nini na kitu gani kilikupelekea kufanya ugunduzi huo?

SmartClass ni jukwaa la kiteknolojia linalowaunganisha walimu bora kabisa hapa Tanzania na wazazi pamoja na wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Online Live Classes.

Tofauti yetu:-

Platform zingine zote za E-Learning hapa Tanzania na Africa Mashariki zinaweka material na maswali wanafunzi wana download wanajisomea wenyewe ambapo nature hii inapelekea wanafunzi kukariri na sio kuelewa kiundani zaidi wanachojisomea.

Sisi SmartClass tumejitofautisha kwa kuwapa walimu nafasi ya kufundisha wanafunzi mahala popote walipo kwa live online classes, tumewapa wanafunzi nafasi ya kutafuta walimu bora hapa Tanzania na kujifunza pamoja kupitia live online classes, tumeenda mbali tumewaruhusu walimu kutengeneza madarasa ndani ya jukwaa letu yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 50 na wote wakasoma kipindi kimoja kutoka kwa mwalimu mmoja na wakauliza maswali kwa mpangilio na wakaandika notes vizuri ambazo wanafundishiwa.

2. Katika kipindi hiki cha kupambana na Covid-19, Smart Class imeweza kuwasaidia vipi wanafunzi ambao wapo nyumbani?

Smartclass imewasaidia wanafunzi kuweza kujipatia walimu bora kabisa hapa nchini Tanzania na kuendelea kujifunza topic mpya na kufanya marudio ya topic walizokwisha soma shule na hawakupata kuelewa.

Imekuwa rahisi sana kwao kujifunza bila kwenda kwenye masomo ya ziada au kukutana, sasa wanakutana kupitia Smartclass class group na wanasoma pamoja na walimu wanaopata kuwachagua wao wenyewe kwa ajili ya online live classes.

3. Changamoto gani Smart class inapitia katika kuwasaidia wanafunzi ambao wapo nyumbani?

Changamoto kubwa ni kwamba tunashindwa fikia 55% ya wanafunzi walio katika mfumo wa elimu hapa Tanzania kutokana na wengi kutokuwa na uwezo wa kupata internet.

Lakini ni kwamba Smartclass tumeweza kutengeneza njia mbadala kwa ajili ya wanafunzi wasio kuwa na uwezo wa kupata internet lakini inahitaji nguvu kubwa kifedha ilikufanikisha ilihali sisi hatuna nguvu hiyo kubwa.

Lakini tunategemea kabla ya 2030 tutakuwa tumefikia wanafunzi 95% waliopo katika mfumo wa elimu hapa Tanzania kwani tunaendelea kutafuta washirika wa kufanya nao kazi kwa pamoja.

4. Mpaka sasa Smart Class imeweza kuwafikia na kusaidia wanafunzi wangapi kipindi hiki ambacho wanafunzi wanasoma kutokea nyumbani?

Smartclass imefanikiwa kuwafikia wanafunzi 20000+ na walimu 5000+ na katika kipindi hiki cha Covid-19 tumefanikiwa kuwafikia wanafunzi zaidi ya 427 waliojifunza kwa online live classes mpaka sasa huku kila wiki wakijisajili wanafunzi pamoja na walimu zaidi ya 500 wakitaka kupata huduma zetu na kutoa huduma za kufundisha

5. Nini maoni yako kuhusu “Ubunifu” kwa wanafunzi na vile wanaweza kupambana na Covid-19?

COVID-19 imeleta ufahamu kuwa technolojia inayo nguvu sana hapa duniani katika maswala yote ya kihuduma za jamii na imekuwa kama simu ya uwamsho kuwa Afrika tunapaswa kuamka na kuhamia katika technolojia.

kwaiyo wanafunzi waendele kutumia smartclasstz.com ilikuweza kuendelea kujifunza na mifumo mingine ya elimu katika kujifunza mambo mbalimbali

Mission ya SmartClass:-

Kumsaidia mtu yoyote kujifunza kitu chochote mahala popote wakati wowote.

Vision ya SmartClass:-

Kubadilisha namna watu wanavyo fundisha na kujifunza hapa Afrika.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

This post has 2 Comments

2

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend