Kupata kazi ni kazi. Hivyo ni vyema kuwa na mbinu mbalimbali za jinsi ya kutafuta kazi. Siku hizi hata unao wategemea wakupe connection nao wanatafuta connection. Hivyo inabidi uanze kujijenga mwenyewe from scratch ili kuweza kuvutia connections!
Vilevile siku hizi haitoshi kujua unachokijua tu, bali uwezo wa kushawishi watu waamini kuwa wewe ndiye mtu sahihi katika hilo ndio kitu muhimu zaidi. Wengi wana digrii kama wewe. Wengi wanajua Microsoft Word kama wewe, hivyo CV zenu hazitofautiani.
Ingia na gia mpya katika ulingo wa kutafuta kazi!
Hebu siku moja acha kujiweka kama unatafuta kazi. Hiyo mbinu kila mtu anaitumia na pengine una ushahidi jinsi ambavyo haijakusaidia kwa muda mrefu.
Badala ya kujiunga linkedin na kusema ‘you are actively looking for a job’, Jiweke kama unatoa huduma (professional service) kwenye taaluma uliyosomea. Kama umesoma Accountancy, jaribu kujiweka kama Financial Advisor au Consultant kwa wajasiriamali wadogo.
Ukienda kwenye warsha na semina mbalimbali, jitambulishe kwa watu (elevator pitch) kwamba ‘Unasaidia wafanyabiashara wadogo kufanya maamuzi sahihi ya kifedha katika kukuza biashara zao’
Tengeneza hoja kama vile, umeona makosa mengi ya kifedha wanayofanya wajasiriamali wadogo katika kuendesha biashara zao. Na uko tayari kuwasaidia.
Hakuna kitu kizuri kimewahi kutokea kwa nyakati zetu kama Internet. Internet haibagui wewe mtoto wa nani au umetoka wapi. The internet rewards good effort (consistency and authenticity).
Habari njema ni kwamba hapo ulipo tayari una kifaa chenye nguvu ya kuweza kukufanikishia malengo yako ya kupata kazi. Nazungumzia simu na bando lako la intaneti. Unaweza kutumia mitandao ya kijamii na majukwaa mengine ya kidigitali kujenga chapa binafsi (personal brand)
Changama na watu mtandaoni kama ilivyo katika maisha halisi. Toa maoni kwenye post zinazohusu taaluma yako. Uki-share makala, jaribu kuongeza maoni yako binafsi kwenye hiyo makala.
Kama ni mwandishi mzuri, unaweza kuanzisha blog kabisa. Kwa mfano mimi; mbali na kujinadi kwamba ni mbobezi wa masuala ya Digital Marketing, nina blogu yenye mfululizo wa makala mbalimbali kuhusu digital marketing ambayo itakuondolea wasiwasi juu ya uwezo wangu katika maswala ya kutafuta masoko kwa njia ya digital. Makala hizo zimefanya nionekane kwenye kurasa za mbele za matokeo ya utafutaji (SERPs),hivyo kudhihirisha maarifa niliyonayo katika SEO na uandishi maudhui.
Hivyo ndivyo unaweza kushawishi watu wakufikirie vile ambavyo unataka wakufikirie (personal brand). Tumia muda wako kujinadi mtandaoni na kujiweka katika muonekano ambao watu watakuona unafaa kwa kazi unayolenga kuipata.
Kikubwa ni kutambua unalenga kundi gani la watu. Kama unalenga watu wenye ushawishi mkubwa kwenye makampuni au waajiri (recruiters) ni vyema ukatumia muda wako mwingi katika jukwaa la Linkedin. LinkedIn ni mtandao ambao ma-CEO kwenye makampuni mbalimbali wanapenda kuvinjari huko. Ukiweza kushiriki kwenye posti zao kwa kucomment vizuri, huenda wakakuona na inakuwa rahisi kuwatumia CV yako kupitia inbox.
Wacha nikupe ushuhuda binafsi, mimi sijawahi kwenda kwenye ofisi ya mtu kuomba kazi. Wengi hunipata kupitia Google na wengine kupitia profile yangu ya LinkedIn. Nina followers zaidi ya 24,000 kwenye mtandao wa linkedin na huwa niko active sana huko kwa kupost maswala mbalimbali yanayoshirikisha (engage) watu, hasa yahusuyo digital marketing. Hata makala hii imetokana na post niliyoiandika huko na kufanya watu wengi kunitumia meseji za shukrani. Hivi karibuni nimefanya kazi na kampuni inayojihusisha na maswala ya ufugaji wa kuku, pamoja na kampuni ya ulinzi ambapo wamiliki wake wote waliniona linkedin na kuomba nifanye nao kazi za kutengeneza website pamoja huduma nyingine za social media marketing.
Kitu kingine cha muhimu zaidi ni kuchunga mienendo yako mtandaoni. Ukiposti kitu mtandaoni, kinaonekana dunia nzima. Unaweza ukadhani ni utani, lakini kwa sisi ambao hatukujui tutakufikiria kulingana na ulichopost.
Hivyo, unapoamua kupost kitu mtandaoni, fikiria akikiona mtu unayetarajia akuajiri atakufikiriaje?
Kupata kazi ni kazi. Jaribu kubadili strategy.