Internet ni kitabu chenye maarifa na ujinga ndani yake

Nadhani kitabu sio kitu kigeni masikioni kwa watu wote. Uwe mvivu au usiwe mvivu, uwe msomi au usiwe msomi ila taarifa ya kitabu utakuwa nayo. Nani ambaye hajawahi kutumia kitabu? Hata viziwi wanatumia vitabu, nao vipofu wanasikia elimu iliyopo vitabuni. Hakika hakuna ambaye hajawahi kunufaika na kitabu.

Kitabu ndio kimetoa madokta, kimetoa wanasayansi wakubwa wote unaowajua wewe. Kitabu ndio kimechora ramani za vita vyote ulivyowahi kusikia, kumbe hata wanajeshi pamoja na ubabe wao, nao wanatumia vitabu?

Ni maarifa gani ambayo kitabu kitashindwa kukupa? Jibu ni rahisi: Hakuna. Kila kitu kipo kwenye vitabu.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa Intaneti.

Mtandaoni kuna kila kitu unachotaka kujifunza. Elimu, siasa, uchumi na mambo ya kijamii yote yapo ndani ya Intaneti. Hakuna kitu unachoweza kukosa.

“Mtandaoni kuna kila kitu unachotaka kujua”

Labda nikwambie kitu: Kama unatafuta ajira, ingia katika websites kama LinkedIn, Ajira Leo, Brighter Monday na nyinginezo utapata na kukutana na michongo mbali mbali. Usiseme huna connection – ni bando lako tu ndio linaweza kukufikisha kwenye michongo hiyo yote.

Kama unataka habari na kujuzwa vitu vinavyoendelea duniani kuna sites kama Jamii Forums, blogs na mitandao ya kijamii. Hapa utapata kila habari, udaku, umbea, habari za kiuchumi, ujasiamali, elimu na habari nyingine. Kazi kwako kuchagua habari gani zinakufaa.

Nakuibia hii siri, Google na YouTube kuna kila elimu na michongo unaoitafuta. Kila unachotaka au kukitafuta kipo Google na YouTube. Narudia tena: Chochote unachokitafuta, kipo Google na kwa YouTube. Kuna tutorials, online courses, DIY videos, na maudhui mbali mbali ambayo yanaweza kukusaidia katika mishe zako.

Ila mwisho wa siku, kila mtu na simu yake na bando anajiwekea yeye mwenyewe. Kwahiyo hatupangiani matumizi. Kila mtu anatumia vile Intaneti anaona inafaa kutumika kwake.

Kuna msemo unasema “Ukitaka kuficha utajiri, basi ficha kwenye kitabu”. Kitabu kinaweza kukaa ndani miaka kwa miaka na hakuna mtu atakuja kukifunua. Ndio, watu ni wavivu kusoma ingawa wanajua faida zote na maarifa yaliyopo kwenye vitabu.

Ukitaka kuficha utajiri, basi ficha kwenye kitabu

Ni kama ilivyokuwa kwenye Internet. Tunajua sehemu zote za kwenda kujifunza na kuchukua maarifa. Google, YouTube, Quora na sites nyingine zote tunazijua. Ila bado tumeamua kutumia Intaneti kufuatilia vitu vya ajabu ambavyo havina faida kwetu.

Sio kitu kibaya, ila hiki ndio nilichokiita upuuzi wa Intaneti.

Kuna mambo ambayo yanatupumbaza na tusione fursa na maarifa ambayo yapo mtandaoni.

Kila siku tunatumia Intaneti, tujiulize tunajifuna nini kwa bando letu tunaloliweka? Au tumeamua kutokifunua kile kitabu ambacho kimefichwa utajiri wa maarifa ndani yake?

Tunajifuna nini kwa bando letu tunaloliweka?

Tumekuwa kasuku. Kila siku tunarudia na kutumia Intaneti kwa matumizi yale yale. Tunatoka WhatsApp, tunaingia Instagram, halafu tunamalizia na Facebook.

Kibaya zaidi, huko kote tunafuatilia habari za umbea na udaku ambazo mara nyingi hazina faida yeyote kwetu. Na kwa bahati mbaya Intaneti inatupa kile sisi tunachokitafuta.

Ukiingia mtandaoni kwa nia ya kujifunza, basi utajifunza. Na ukiingia mtandaoni kwa nia ya kuangalia vitu vya kipuuzi, basi Intaneti itatupa kile unachokitafuta.

Intaneti ni kama kitabu kilichofunikwa. Ndani yake kina maarifa na upuuzi. Kazi ni kwetu kutumia vile tunataka. Tunaweza funua na kupata maarifa, au tukapuuzia na kuchukua upuuzi wake.

Intaneti ina kila kitu, ila itakupa na kukulisha kile unachokitafuta ndani yake, maarifa au upuuzi wake. Hilo litakuwa chaguo lako, kwa leo naishia hapa.

Online courses za bure:


Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend