Maswali matano na Faidha Ngaga

Faidha Ngaga ni muhitimu wa shahada ya Mawasiliano kwa Umma (B.A Mass Communication) na pia ni mwandishi wa habari kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Pia ni mwanzilishi wa:

Leo Faidha amejibu maswali matano juu ya uzoefu wake katika habari hususani katika utangazaji wa mtandaoni “Podcast”.

  1. Ni nini maana ya “Podcast”? Na kwanini uliamua kufanya podcast?

Podcast ni mtiririko wa vipindi ambavyo vinaweza kuwa audio au video, ingawa msingi wake mkubwa ni audio ambavyo mtu anatengeneza vya maudhui yoyote. Kwa mfano siasa, vichekesho, burudani na kuongelea mambo mbali mbali ya kijamii na mengineyo.

Audio hizo zinaweza wekwa iTunes, Boom Play, Audiomack na kwa mazingira ya huku kwetu mtu anaweza weka vipindi vyake hata YouTube.

Na niliamua kufanya podcast sababu nilikuwa napenda kutangaza. Kuna rafiki yangu ambaye alikuwa anapenda kunisikiliza kipindi natangaza, hivyo alinishauri nianzishe vipindi vyangu mwenyewe ambapo hapo wazo la kuanza podcast ilipoanzia. Na nilipata msukumo zaidi baada ya kukutana na ndugu yangu mmoja ambaye nilianza kufanya nae pia.

2. Podcast yako ambayo unaifanya, umeipa jina gani na kina nani walengwa ambao wanaguswa na matangazo yako?

Podcast yangu ilikuwa inaitwa “Midday Party Podcast” na ilikuwa inalenga zaidi vijana na watu wengine ambao wanapenda burudani maana ilikuwa inahusu muziki wa sasa na ule wa zamani.

Pia na wale ambao wanapenda mziki maana kuna vipindi vingine tunapiga mziki na kukumbushana historia ya muziki wa zamani.

Podcast yetu tunafanya kwa lugha ya kiingeleza, kwahiyo walengwa wetu wengine ni wale wenye uelewa wa lugha hiyo.

3. Unaweza kuongelea vipi mapokeo ya podcast yako kwa watu na ni kitu gani kilichokufanya usimamishe kwa muda?

Mapokeo ni mazuri tena sana. Nilianza kufanya kwa kuwa napenda na ilikuwa kama burudani tu kwangu. Ila baadae watu walitokea kupenda tunachofanya na kupata wasikilizaji hadi nje ya nchi maana tunafanya kwa lugha ya kiingeleza.

Nilianza kufanya kwa kuwa napenda na ilikuwa kama burudani tu kwangu.

Ilifikia kipindi mpaka watu wakawa wanatamani kuniona na mrejesho wa wasikilizaji wangu ni mkubwa na nzuri pia.

4. Je unadhani podcasting inaweza kusimama kama ajira kwa vijana wa Tanzania?

Ndio, podcast inaweza kusimama kama ajira kwa vijana.

Kwa mfano watu wengi wanapata mapato kupitia YouTube, kwahiyo unaweza tengeneza vipindi vyako na ukaweka kule na ukapata mapato pia.

Vile vile kuna iTunes unaweza kuweka kule na ukapata mdhamini na kusimama kama chanzo cha mapato.

Pia ukipata wasikilizaji wengi unaweza kuanza kupata matangazo kutoka kwenye makampuni au taasisi mbalimbali na kusimama kama chanzo kingine cha mapato.

5. Je nini kifanyike ili kuinua uelewa na fursa zilizopo kwenye upande wa digitali haswa upande wa podcasting?

Kuna kampuni na taasisi nyingi ambazo zinaweza kuwajengea uwezo vijana kujua umuhimu wa matumizi mazuri ya mtandao.

Vile vile semina na makongamano yanahitajika zaidi katika kuwaelemisha kuhusu mambo mbalimbali kuhusiana na teknolojia na sio kwa upande wa podcast tu.

Na vijana wenyewe wanatakiwa kuwa na kiu ya kujifunza vitu. Maana siku hizi kila kitu kinapatikana mtandaoni. Muhimu ni kujiwekea malengo ya kujifunza na kutumia muda wako vizuri popote pale unapotumia Internet.

Na vijana wenyewe wanatakiwa kuwa na kiu ya kujifunza vitu. maana siku hizi kila kitu kinapatikana mtandaoni. Muhimu ni kujiwekea malengo ya kujifunza na kutumia muda wako vizuri popote pale unapotumia internet.


Unaweza kumpata Faidha Ngaga katika mitandao ya kijamii kupitia Instagram @faidha_ngaga na Twitter @faidha_ngaga.

Pia unaweza sikiliza matangazo yake ya Podcast kupitia YouTube na Audiomack.

Header photo by Jonathan Velasquez on Unsplash

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend