Maswali matano na Jirani App

Fanuel Kiano ni mwanafunzi wa Computer Science and Technology kutoka Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere, Dar es salaam. Pia ni mwanzilishi wa Jirani App, mtandao wa kwanza wa kijamii kwa ajili ya Watanzania na kuwaunganisha Watanzania.

Jirani App inapatikana kupitia www.jirani.co.tz au Play Store (JiraniApp).

1. Jirani App ni nini na inapatikana vipi?


Jirani App ni application ambayo inamwezesha Mtanzania na mtumiaji mwengine yeyote anaetoka nje ya Tanzania kufanya mambo mbalimbali kama kupashana habari na kuwasiliana na ndugu na marafiki.

App ina uwezo na kumwezesha mtumiaji kusambaza mafaili kama vile documents, picha na video kwa ndugu na marafiki mbalimbali.

Pia unaweza kutangaza biashara kupitia panel ya Jirani Market, vilevile App ina uwezo wa kumsaidia mtumiaji ku boost matangazo au post zake kwa ujumla.

2. Kwanini ulichagua kuanzisha mtandao wa kijamii na sio app nyingine?

Kwanza wazo la kuanzisha app ya kijamii sikuwahi kuwa nalo ila ilikuja baada ya kukaa na rafiki yangu ambae tulishauriana kwanini tusitengeneze app kama ya WhatsApp, lakini rafiki yetu mwingine akashauri kwanini tusitengeneze ya kubeti?

Lakini mimi na rafiki yangu wa kwanza tulifikia muafaka tutengeneze app ya kijamii lengo lilikuwa ni kuchati tu na si kivingine. Baada ya muda tulitengeneza kundi la watu 4. Tukaanza kazi, app yetu ilisimama kiasi. Kwa wakati ule tuliita “interface” ila badae ilikufa.

Ilipofika mwaka 2019, niliona nisimame mwenyewe niwe natumia baadhi ya watu kama msaada wa kuendeleza safari yangu nikaja na wazo la App iitwayo “Worldgram” na hapo lengo kuu lilikuwa ni kumwezesha Mtanzania kuchat, kushea videos na kusoma vitabu kwa kipindi kile ambapo panel ya vitabu.

Worldgram ilianza kufanya kazi ndani ya miaka miwili mpaka pale nilipokaa na marafiki na ndugu zangu na baadhi ya waalimu kama Dr. Mlelwa, Engineer Anwar Uvilla, na Mr. Jason waliweza kunipa baadhi ya ushauri na niliufata.

Baada ya hapo, mwaka huu mwezi wa kwanza, jina la Jirani App lilianza rasmi kutoka Worldgram ikiwa kwamba tunachukulia app kama kijiji cha watanzania wote ambapo kila mmoja atakuwa jirani wa mwenzie ndani ya app.

Nilichagua kuanzisha mtandao wa kijamii kwa dhumuni la kuwasaidia Watanzania kutumia app ya nyumbani tofauti na za nje ambazo hazina ulinzi mzuri kwetu, hivyo basi hiki ni chetu sote Watanzania tujivunie.

3.Umeweza kuitofautisha vipi Jirani App na mitandao mingine?

Ndani ya Jirani App ili uweze ku boost tangazo lako liende mbali unahitaji uwe na points za kutosha ambapo points hizo utazipata baada ya kutumia app hii kwa muda fulani. Na ndipo points hizi utazitumia kuboost tangazo lako la kibiashara ambapo ni tofauti na mitandao mingine kama Facebook na Instagram itakuhitaji Mtanzania kutumia pesa kwajili ya ku boost matangazo. Tumefanya hivyo ili kuendana na mazingira ya huku nyumbani hali.

Utofauti mwengine ndani ya Jirani App na app zingine, kuna coins au pesa za jirani ambazo Mtanzania anaweza kuzinunua kwa Jirani App au akapunguziwa na mwanajirani mwenzie ili aweze kununua points za ku update akaunti yake kuja kuwa ya kibiashara ili aweze kupost vitu kwenda kwa wengi.

4. Mapokezi ya Jirani App yapo vipi na nini ungependa kifanyike katika kuboresha Jirani App?

Toka nianze kuitangaza mapokezi ya Jirani App ni mazuri sana, kwani asilimia kubwa ya Watanzania wameipenda na wanajivunia vya nyumbani.

Ni tofauti na asilimia ndogo wakiiponda na kusema nimeiga kwa wengine kama Facebook. Wanashindwa kuelewa kumbe hata Facebook aliiga na akishindwa kuiga ananunua.

Mfano mzuri mtandao wa kwanza wa kijamii duniani ulianzishwa mwaka 1997 kipindi nina miaka 4, uliitwa SixDegrees social network na kuja kufa mwaka 2001. Na mtandao wa Blogger ni mwaka 1999, Friendster mwaka 2002, MySpace mwaka 2003, na Facebook 2004 ambapo mwanzilishi wake aliiga mitandao yote iliyopita na akatengeneza kama ile ya zamani na ndipo safari yake ikaanzia pale.

Kwangu sioni kama kuiga kitu kizuri ni vibaya.

5.Ni maono gani yanakufanya uamini katika Jirani App na unaiona wapi baada ya miaka mitano?

Maono yangu ni kwamba nategemea baada ya miaka mitano app ya Jirani imwezeshe Mtanzania kurahisishia shughuli zake zote za kimtandao na kijamii ambazo zinategemea kimtandao.

Maono mengine ni kwamba, app hii ije kuwa app kubwa hapa nchini na hata Africa kwa ujumla. Ninajua kuna ushindani toka kwenye app kubwa kama Facebook na Instagram, lakini watupe muda tu kama Watanzania wenye malengo. Nina imani tutafika huko walipo na tutachuana kitechnolojia.

Jirani App inapatikana kupitia www.jirani.co.tz au Play Store (JiraniApp).

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

This post has 2 Comments

2

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend