Maswali matano na Eileen Mwalongo

Eileen Mwalongo ni Mtanzania na mwanafunzi wa Diplomasia katika Chuo cha Vistula nchini Poland. Eileen amekuwa akijihusisha na masuala mbalimbali yanayohusu elimu na haki za watoto wakike kwa kufanya kazi katika mashirika mbalimbali.

Pamoja na hayo, anamiliki jukwaa la Youtube ambayo amekuwa akitumia kuwasaidia watu mbalimbali kwa kuwapa elimu namna wanaweza ku-apply vyuo mbalimbali na hatua muhimu za upatikanaji visa n.k.

1. Ni kitu gani kilikusukuma mpaka ukaamua kufungua YouTube channel yako mwenyewe?

Kwa kipindi kirefu sana nilikuwa natamani kufungua chaneli ya YouTube. Msukumo mkubwa ulitoka kwa mwalimu wangu chuoni ambaye alikuwa anatufundisha programu ya uandishi wa habari katika diplomasia. Siku moja alitupa kazi ya kutafuta habari na kufungua chaneli za YouTube na kila mmoja aweke habari hiyo kwenye YouTube. Nilipoona nimeweza kufanya kazi hiyo vizuri nikaamua kuendelea nayo. Lengo likiwa kuwasaidia Waafrika wenzangu ambao wanatamani kuja kusoma Poland kwa kuwapa elimu namna ya kupata chuo, visa n.k.

Mpaka sasa una watazamaji wa ngapi na mafanikio gani ambayo umeyapata kutokana na YouTube channel yako?

Mpaka sasa chaneli yangu inawatazamaji 1280 kutoka bara la Afrika, Ulaya, Marekani na bara la Asia.

Kwa kweli, kitendo cha kuweza tu kutimiza ndoto yangu ya kuwa na jukwaa kama hili kwangu ni mafanikio kwa sababu ndoto yangu haijaishia kwenye fikra bali nimeitekeleza.

Zaidi, kuweza kusaidia wengine kufika kusoma Ulaya kwa kuwapa taarifa sahihi ya namna ya kupata chuo n.k ni mafanikio mengine.

Zaidi, kwa kupitia chaneli hii nimeweza kutambulika na Wizara ya Elimu ya nchini Poland na kunichagua kuwa kati ya mabalozi wa elimu (kuvutia wasomi wengi zaidi kuja kusoma Poland) kwa kipindi cha mwaka 2019-2020.

Kwenye upande wa YouTube, ni influencer gani unayemwangalia kama role model wako? Na kwanini ni yeye?

Kwakweli wapo waragabishi (influencers) wengi ambao ninapenda namna wanafanya kazi zao kutoka sehemu nyingi duniani kama Patricia Bright, Whitney Madeuke, Sharon Mundia, Ijeoma Kola, All Things Adriane n.k wengi wa namna yao wamenivutia kwa sababu ya ubora wa kile wanachofanya, ustahimilivu na maudhui wanayotoa.

Ukiachana na YouTube ushawahi au unafanya kitu chochote kingine kwenye upande wa digitali?

Ndio, mwaka 2017 nilifungua blogu ambayo niliitumia kama sehemu ya kuonyesha uwezo wangu wa uandishi lakini baada ya kuona ninapendea zaidi video nikahamisha mipango na kutaka kufungua chaneli ya YouTube ambayo ilianza mwaka 2019.

Matumizi ya mtandao kwa mtoto wa kike hususani wasanii na wanamitindo yanachukulia vibaya sana katika jamii. Una neno gani la kuwaambia waweze kufika hapo ulipofikia?

Kwakweli, mitandao hasa mitandao ya kijamii imekuwa ni mahali ambapo watu hasa wasanii na wanamitindo wanaweza kufanya biashara na kujipatia pesa.

Ushauri wangu ni kujitahidi kuzingatia sheria na maadili na kuchuja kile unachotaka kukionyesha kwa wengine kabla ya ku-share kama kinakidhi maadili ya pale ulipo na kufuata sheria.

Unawezea ungana na Eileen Instagram, Facebook na pia kwenye YouTube channel yake.

Previous ArticleNext Article
Leonce Godfrey has been in the field of Digital media and digital marketing with more than 3 years experience working in various capacities with highly reputable companies and organizations. He is writer, storyteller, content creator, photographer and journalist by professional. He simply amazing.

This post has 1 Comment

1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend