Maswali matano na G3tta

G3tta ni msanii mwenye uwezo wa kurap na kuimba, alianza mziki 2016 ambapo 2017 alitoa EP ya kwanza ‘Mikazo Mwa-Mwi’ iliyokua na nyimbo 4, 2018 akaachia single yake ya kwanza ‘Fareed Kubanda’ pamoja na video.

Mpaka sasa ameachia Ep 2 ‘Mikazo Mwa-Mwi na Mikazo Mwa-Mwi II’. Tulipata nafasi ya kumuuliza G3tta maswali matano na haya ndio tuliyoongea;

1. Unauelezea vipi mziki wako na ni alama gani ungependa kuiacha kwenye tasnia?

Asilimia kubwa ya mziki wangu unahusu matukio nliyokutana nayo katika maisha iwe ni mapenzi au mihangaiko ya hapa na pale. Ningependa mziki wangu uendelee kuishi ata when I’m done singing na uwe ni wa ku inspire wengine kufanya wanalotaka

2. Je muziki unaweza kufanyika kama ajira kwa vijana wengi na mtu unawezaje kuanza?

Zamani mziki ulionekana kama ni uhuni lakini sasa inatambulika kama mojawapo ya ajira kwa vijana, la msingi ni kujua unataka kufanya nini katika mziki na uheshimu kama ambavyo unge heshimu kazi zingine.

3. Mitandao ya kijamii inakusaidiaje katika kazi zako?

Ina play part kubwa sababu inaniwezesha kuwafikia shabiki zangu kwa wakati husika na pia napata kuconnect na other artists.

4. Usingefanya mziki ungefanya kazi gani? Na kwanini ni muhimu kwako kujiamini na kugive music your all?

Tricky, think ningekua a chef by now. Kujiamini inakua rahisi pale ambapo unaamua kufanya jambo unalo lipenda or kutoka moyoni na me ni chizi mziki tangu mdogo so ilikua ni swala la muda tu

5. Ni ushauri gani unao kwa wasanii wengine na creatives wa kiafrika kijumla?

Tuwe huru kutengeneza tunachojiskia na tujitahidi kutengeneza chetu mana kwa sasa focus yote ipo kwetu.


Unaweza kuangalia kazi za G3tta YouTube chaneli yake, unaweza mfollow Instagram na kumpata kwa email – bookg3tta@gmail.com.

Previous ArticleNext Article
Eunice is a multi-niche freelance writer with experience in writing health, lifestyle, finance, interviews, tech, travel, entrepreneurship, automotive, and mental health articles.

This post has 2 Comments

2

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend