Maswali matano na Noel Mpolenkile

Noel Wensteslous Mpolenkile ni mwanachuo wa Sokoine University of  Agriculture, akisoma kozi ya Veterinary Medicine and Biomedical Sciences akiwa mwaka wa 4.

Uandishi ni upande wa pili wa maisha yake ya kila siku ukiachilia mbali shule, Noel ni mwandishi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo huko ndipo alikutana na fursa ya shindano la uandishi wa hadithi fuli la Kalahari lililojumuisha bara zima la Afrika.

Alishiriki shindano hilo mwezi wa tano na akabahatika kuwa mshindi wa tatu kati ya waTanzania wawili walioibuka washindi katika shindano hilo la uandishi Afrika nzima.

Vijana FM tulipata nafasi ya kuhojiana na Noel na haya ndiyo tuliyoongea.

  1. Nini kinakuhamasisha kuandika?

Kinachonihamasisha mimi kuandika ni vile tuu napenda kuandika, napenda kuweka hisia zangu katika maandishi na mara nyingi nikiwa sina mood au niko bored ili nirejeshe hali yangu ya kawaida basi nitaandika chochote tu.

Pia kitu kingine huwa nipo kwenye mashindano binafsi maana siku zote nikiandika hadithi moja nitatamani kuandika nyingine bora kuliko ile ya mwanzo.

Kilichotokea kwenye Kalahari short stories competition ni kwamba ilinikuta kwenye kipindi kigumu sana kwahiyo hasira zangu zote nikazimalizia kwenye keyboard kuandika hadithi ile.

Noel Mpolenkile

2. Kitu gani unadhani kinaweza kuboresha utunzi?

Kwa mwandishi mwenzangu ili kufanya uandishi wako uwe bora ningeshauri mtu uvae uhusika, yani katika kuandika ujione ndani ya hadithi ukiicheza scene fulani, kiufupi uhalisia uwepo katika hadithi. Hiyo itakufanya uweze kutoa kitu kilicho bora, ile kazi ambayo hata wewe mwenyewe mwandishi itakufanya usisimke ukiwa unasoma, ile hadithi ambayo ukiisoma mwenyewe unasikia huzuni au furaha yani sawa na utishwe na kinyago ulichochonga mwenyewe.

Kingine ni kutokua mvivu wa kusoma maana mwandishi mzuri ndio yule msomi mzuri wa kazi nyingine za watu. Hiyo itakusaidia kujua wenzako wanatumia mbinu gani kuandika.

3. Nini ilikuwa dhamira ya stori yako iliyokuletea ushindi?

Dhamira kubwa ya ile hadithi ilikua ni UKATILI WA MAJUMBANI (Domestic Violence) ikimuonesha mwanamke mmoja mzuri wa mwili na roho aliyeteswa na kunyanyaswa na mumewe kwa kushindwa kupata mtoto.

Imekua kawaida kwa jamii zetu za Afrika kumtupia mzigo wote mwanamke linapokuja suala la kutopata mtoto hali ya kuwa mwanaume pia anaweza akawa na tatizo.

Ni hadithi nzuri sana maana hata mimi mwenyewe ilinisisimua mno nikabaki namuonea huruma mwanamke yule.

4. Kwanini unapenda hadithi za kutunga (fiction) kuliko za kweli (non fiction)?

Ninapenda hadithi za kutunga kuliko za kweli kutokana na kwamba naamini za kweli zinakua zina visa ambavyo sio vikali sana vya kuweza kumshtua msomaji lakini kwa hadithi ya kutunga unakua na uwanja mkubwa wa kukinoa kisa mpaka msomaji akashika kidevu akishangaa inakuaje mtu kupitia haya au mtu anawezaje kufanya hivi.

Hadithi ya kutunga inakupa uwezo wa kuelezea jambo dogo kwa ukubwa sana tofauti na hadithi ya ukweli ambapo mtu inatakiwa upite sawa na matukio yaliyotokea. 

5. Ni vitabu gani unapendelea kuvisoma? Na tuambie vitabu vyako bora vya wakati wote?

Napenda sana vitabu vya historia na vingi vya kuongeza thamani ya mtu kupitia Saikolojia na maarifa binafsi. Napenda sana vitabu vilivyoandikwa na Yuval Noah, Dan Brown na Robin Sharma.

Vitabu Vyangu bora vya wakati wote ni: 

  • The Monk Who Sold His Ferrari cha Robin Sharma
  • Angels And Demons cha Dan Brown 
  • The Brief History Of Human Kind cha Yuval Noah 

Unaweza soma kazi za Noel Wensteslous Mpolenkile kwenye tovuti yake, Twitter na Instagram.

Previous ArticleNext Article
Eunice is a multi-niche freelance writer with experience in writing health, lifestyle, finance, interviews, tech, travel, entrepreneurship, automotive, and mental health articles.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend