Kama mtu na kijana mwingine yoyote, kuna siku ambazo mawazo yako hurandaranda kujaribu kutafuta majibu ya mambo mbalimbali.
Je, umeshawahi kufikiria kwa kina kuhusu suala la motisha? Nini hukusukuma kufanya shughuli zako za kila siku? Umeshawahi kujiuliza kwanini unaenda shule au kazini? Nina uhakika kuwa baadhi yenu mtaanza kufikiria watu ambao wanateseka ili tu mkono uende kinywani. Lakini hapa nazungumzia wale ambao kwenye jamii zetu huonekana kufika kwenye kilele cha mafanikio; wanaonekana kama wana kitu zaidi. Ni kipi hicho basi? Tunaweza kujifunza au kuwafundisha wadogo/watoto zetu? Au ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho — na mazingira na mazingara hayawezi kukibadilisha?
Nimepata nafasi ya kujadili hili na marafiki zangu wengi, lakini mpaka sasa hivi sijapata jibu ambalo limeniridhisha. Labda maisha pamoja na lengo la maisha yetu hayawezwi kuelezwa kwa maneno.
Nina uhakika taswira za watu mbalimbali ambao unajua wanafanya kazi zao vizuri zinaanza kutokea kwenye fikra zako. Pia, unajua hadithi zao jinsi walivyofanikiwa kwenye shughuli zao.
Kuna wale ambao hadithi zao hutupa motisha; hulka zao tu hutosha kutusaidia kutupa msukumo kwenye maisha yetu kwa namba moja au nyingine, hasa pale motisha zetu zinapopungua kutokana na vikwazo vya hapa na pale. Mimi binafsi nina orodha ndefu kiasi (mama yangu akiwa namba moja!), lakini mara nyingi napenda kujikumbushia ‘safari’ ya William Kamkwamba:
Hakuridhika na kuishia hapo. Angalia alivyorudi miaka miwili baadae:
William, I salute you. You are one of my heroes!