Msomaji, nadhani wewe ni mmoja wa watu ambao wamebahatika kupata elimu. Je, unadhani unaitumia elimu yako na ujuzi wako ipasavyo? Matatizo unayoyaona kwenye jamii inayokuzunguka yanakugusa kwa namna moja au nyingine?
Mwezi uliopita niliandika makala kuhusu viongozi ambayo ilikuwa imeegemea kwenye siasa zaidi. Lakini leo ninakuomba uangalie video ifuatayo ya Patrick Awuah, kutoka Ghana, kuhusu viongozi kwenye nyanja nyingine muhimu kwenye jamii. Patrick anazungumzia fikra na mawazo yetu; umuhimu wa kuwa na fikra za majukumu ya kijana kwenye jamii. Kama wahenga wetu walivyosema ‘samaki mkunje angali mbichi’, Patrick anaongelea jinsi ya kuandaa watu kuwa Viongozi — kuwafundisha na kuwafinyanya ili fikra zao ziweze kuwa na mawazo ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye jamii.
Tafadhali, ukipata muda msikilize Bw. Awuah kwa makini: