Ukizunguka kwenye blogs utaona TED talks nyingi tu. Lakini, bahati mbaya wapo ambao walidhani labda taarifa na ujumbe unashindwa kuwafikia baadhi kutokana na matumizi ya lugha ya Kiingereza.
Habari njema: kuna mtu — makala zake kuhusu Sanaa na Tamaduni za Afrika kwa ujumla zitafuata — kanidokeza kuwa kuna baadhi ya mihadhara ya TED imetafsiriwa. Baadhi ya makala na mihadhara michache iliyotafsiriwa inapatikana tayari katika lugha ya Kiswahili!
Ukipata muda msikilize Ngozi Okonjo akizungumzia shughuli za biashara Afrika (usisahau kubofya na kuchagua Swahili subtitles):
Aise heko kwa waliojitolea kutafsiri tovuti hii muhimu. Kama unauwezo wa lugha jiunge nao hapa: http://www.ted.com/translate/translators/lang/swa
Itapendeza kuona talks za akina Brian Cox kuhusu Large Hadron Collider zikiwa na Swahili subtitles. http://www.ted.com/talks/brian_cox_on_cern_s_supercollider.html
Kazi njema.
Asante kwa taarifa ya tafsiri ya TED kupatikana katika lugha ya Kiswahili pia. Kiswahili hoyeee!