Mimi na blogs na facebook!

Na “Mtu Fulani

Kama kawaida yangu, napata habari sahihi kutoka kwenye tovuti yangu ya Wavuti huku nikipiga mzigo. Nikipata upenyo natupia jicho blog ya Michuzi Jr kucheki ana picha gani asubuhi hii. Ni mwiko kuvunja utamaduni wa Mtanzania mwenye mtandao — lazima nicheki mambo gani yanajiri kwa Michuzi aka Mzee wa Masafa ya Mbali. Ah! Hakuna atiko mpya ya Mashaka na inaonekana kama pamedoda kiasi fulani. Ninaperuzi kuelekea chini taratibu nikiangalia picha za matukio mbalimbali; nakutana na post ya salamu kutoka kwa Kamau!

Mhh! Kuna maoni zaidi ya 150?? Mashaka kabadili jina nini!? Nasoma ujumbe wa Kamau taratibu halafu najitosa kwenye maoni. Wabongo kumbe tuna hasira kiasi hiki? Wachafuzi wa hali ya hewa ni wengi, lakini kama wahenga walivyosema, penye wengi hapaharibiki neno. Naona baadhi ya maoni yenye mawazo mazuri. Lakini hizi nguvu zingepelekwa kwenye matatizo ya nchi zetu hizi mbili nadhani tungepiga hata hatua moja ndogo ya mtoto mdogo.

Baada ya kumaliza kazi zilizoko mbele yangu, naenda facebook kuona masela wanafanya nini na kutembelea kurasa za maselebriti wa Bongo. Namcheki msela wangu kutoka kitaani, Gillsant — mshkaji hata akiweka nukta kwenye status yake, comments zinatiririka! Ana marafiki karibia buku tano… Kwahiyo wale wenye blogs zinazotafuta umaarufu hutumia ukuta wake kama ubao wa matangazo.

Namcheki Prof. Jay ambaye alipotea kidogo baada ya kuonekana kavaa uzi wa kijani. Kama kawaida yake anabadilishana mawazo na mashabiki wake. Inaonekana muda na ukimya vimepoza maswali yaliyokuwa kwenye vichwa vya wengi. Naenda kwenye ukurasa wa Fid Q kuangalia kama ameposti mistari na vina vipya. Jamaa mistari yake imeshiba; shule tosha na anaweza kukuambukiza uanaharakati kutokana na msimamo wake.

Ngoja ni-search kucheki kama Juma Nature naye yumo facebook. Kudadadadadeki, Nature ndani ya nyuuumba! Ana mashabiki 46 — ngoja tucheki itamchukua muda gani kufika mashabiki 1000.

Dah! Nadhani inatosha, ngoja nirudi mzigoni. Lakini kabla ya ku-sign out lazima nipate ile kitu roho inapenda: Picha murua.

Nabofya sehemu fulani na naishia kwenye ukurasa wa Vijana FM. Dah, panatia huruma kwasababu pamedoda ile kinoma. Labda wakiweka picha nzuri za watu maarufu watapata mashabiki zaidi (angalau wafike 500 tu).

Nachoropoka kutoka Vijana FM na kuishia kwenye ukurasa wa Ray C. Naperuzi picha zake haraka haraka kwasababu nimeshaziona nyingi.

Vitu vitamu havihitaji haraka kwahiyo natembelea ukurasa wa K-Lynn mwishoni kabisa. Mke wa mtu hasifiwi, lakini nimeamini kuwa Wabongo ni wabishi!

Na-sign out na kutupia jicho blog ya Mange. Duh, nilidhani blog bado ni changa lakini inapata hits zaidi ya buku tano kwa siku! Kwa mwendo huu, hii nd’o itakuwa mama ya blogs zote Bongo. Michuzi itabidi akae chonjo.

Ngoja nirudi mzigoni.

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend