Mbwa wa Pavlov

Marafiki zangu kadhaa wameanza kunihoji kuhusu kukosekana kwa zile makala zinazochokoza ubongo na hisia, kwasababu wanajua fika nasoma na kufuatilia habari za nchi yetu Tanzania kila kukicha.

Kitu ambacho wanasahau ni kuwa kukumbushana na kujadili mambo yanayotugusa moja kwa moja au njia nyingine ni jukumu letu sote — mtu mmoja mmoja. Kwasababu tunajifunza mengi zaidi tunapofanya midahalo na kusikiliza hoja zinazokinzana. Sasa, tunapokosea mara nyingi ni kusubiri fulani atupe mtazamo wake kwanza, kisha sisi ndio tunaunga tela na kusema, “Makala nzuri kijana!” Au, “It was a very good read.” Good f***ing read? Yaani, mi’ najipinda kufanya utafiti wa hapa na pale na kutulia kuhakikisha makala zinakuwa na mtiririko mzuri, halafu watu wanakuja na maoni ya kigoigoi?

Wakati mwingine naona ni kama kejeli tu, kwasababu hakuna mtu anayejua kila kitu! Pia, binadamu tuna hulka ya kuwa na mitazamo tofauti; tunajenga hoja kwa kutumia fikra tofauti na ni kawaida kuwa na hoja zinazokinzana. Mbona sijawahi kusikia mtu na mke wake wamehairisha fungate baada ya kugundua mume ni shabiki wa Yanga na mamaa ni shabiki wa Simba. Mlio kwenye ndoa, tafadhali, nifungueni macho.

Ndio, tuna waandishi maarufu kama Jenerali Ulimwengu ambaye ana upeo wa hali ya juu. Ila nikikubaliana naye tu bila hata kuacha kwanza hoja zake ziogelee kwenye bahari ya fikra zangu, basi nitakuwa nawatukana kina Socrates na Aristotle matusi ya nguoni.

Huwa najiuliza, hivi Socrates na Aristotle wakifufuka leo, halafu tuwaoneshe “midahalo” yetu — sisi Watanzania — je, watafanya nini? Namuona Socrates akiomba kamba ya katani na stuli… halafu anatoka mkuku kuelekea msituni, stuli kichwani, anapiga mayowe huku akitengeneza kitanzi!

Yule Mwanakijiji wa Jamii Forums alishawahi kusema kwamba Bongo tunahitaji kuwa na somo la logic kwenye mitaala yetu. Unaweza ukasema jamaa alikuwa anaota. Angalia, mshua mwenyewe tu alisepa mdahalo mwaka jana! Mshua alipaswa kuwa mfano wa kuigwa…

Wakati bado unang’aang’aa macho na kujiuliza kwanini mwandishi ameamua kuiita hii makala “Mbwa wa Pavlov”, turudi kwenye siasa na muelekeo wa nchi yetu. Tanzania.

Ili kuhakikisha fikra zangu hazichukuliwi msukule na wapuuzi, nimeamua kuupa ubongo wangu likizo za hapa na pale. Kitu ambacho nakifanya ni kutosoma habari na makala zinazojadili muelekeo wa Tanzania kwa kipindi fulani. Kwanini? Jibu ni rahisi: mtiririko unatabirika; majina tu ndio yanabadilika. Niliona nifanye hivyo kwasababu kuna kipindi nilijikuta naanza kuamsha hisia fulani kabla ya hata kumaliza kusoma vichwa vya habari!

Tukatae kutoa udenda tunaposikia kelele za kengele tu. Tunapaswa kujua kengele ipi inaasharia msosi uko tayari, wapi tunapaswa kubweka, wapi tunatakiwa kumtoa dima mwizi na wapi tunapopaswa kung’ata! Kama bado hunielewi basi kubali wewe ni Mbwa wa Pavlov. Na hiyo sio sifa.

Leo tumeamka na kukuta habari ya watoto wawili waliomuua mwenzao wa miaka miwili. Wengi watashtuka sana na kutoa maoni yao juu ya jambo hili. Lakini, hebu tajaribu kulichunguza hili tukio kwa kurunzi kubwa zaidi ili tuhakikishe halitokei tena.

Je, mazingira na mazingara ya jamii yetu yanaweza kusababisha matukio kama haya? Watoto wanazaliwa wachoyo? Au wezi? Nini husababisha watoto kupata ‘kiburi’ cha kumpiga mwenzao na mawe hadi kufa?

Unakumbuka, mara ngapi watu wamejaribu kuanzisha mijadala kuhusu mauaji ya vibaka wanapokamatwa na wananchi wenye “hasira kali”? Akili za watoto zinafyonza kila kitu wanachoona na haya ndio matokeo yake.

Mbwa (kushoto) wakishangaa ukatili unaofanywa na Mbwa wa Pavlov.

Mbwa wa Pavlov wataanza kutafuta visingizio badala ya kutafuta njia za kutatua tatizo. Hawaoni miaka kumi, ishirini au thelathini baadae. Kengele zimepigwa sana tu, ila wengi wanadhani kila kengele huashiria chakula kiko njiani!

Mengi sana yametokea kwenye miezi miwili-mitatu iliyopita, ambayo yanafanya ujiulize maswali lukuki…

Previous ArticleNext Article
Steven was born and raised in Dar es Salaam, and moved to Germany for his studies. He graduated with a BSc. in Physics (Jacobs University Bremen), and then a MSc. in Engineering Physics (Technische Universität München). Steven is currently pursuing a PhD in Physics (growth of coatings/multilayers for next generation lithography reflective optics) in the Netherlands. He’s thinking about starting his own business in a few years; something high-tech related. At Vijana FM, Steven discusses issues critical to youths in Tanzania, music, sport and a host of other angles. He’s also helping Vijana FM with a Swahili translation project.

This post has 7 Comments

7
  1. ..dah…sometimes i think you guys are ahead of time…at the moment you are beating on a dead horse…makala zitakuwa relevant 2020 labda…ila kwa wale wanaojali wanaelewa, na it will inspire them kuifanyia kazi inshu. dah…ila angalie usije ukadata…hehe..manake hii nakala inaonyesha
    uko choka mbaya….bado tunakuhitaji editor, inagwaje sisi wavivu..lol

  2. Huoni hapo ndipo tunapokosea? Tunasubiri kitu kitokee halafu ndio tunaanza kuhangaika. Mbona hata hiyo 2040 sio mbali… acha 2020.

    Fuatilia links za Socrates na mshkaji wake Aristotle hapo juu; walikuwa wanafikiria nini miaka ile Kabla ya Kristo? Hiyo ndio misingi ya Magharibi ambayo matunda yake ndio tunayaona leo. Sisemi tuige kila kitu, la hasha — tunapaswa kujaribu kufikiria mbali zaidi. Na hiyo ndio tofauti kati “yao” na “sisi”.

    Mijadala ya vibaka kuchomwa imeanzishwa mara kibao tu katika vyombo tofauti, lakini watu hawakutilia maanani. Cha kuchekesha tunashtuka leo kuona watoto wakituiga kuchoma ‘wezi’ moto.

    Bata, hapa tunawang’ang’ania nyie ambao mtakuja kushika nyadhifa mbalimbali, serikalini, kwenye makapuni au asasi za kiraia (kama hiyo unayoizindua wiki ijayo). Bila vision mtu huwezi kufanikiwa… Tatizo likitokea utarekebisha wapi wakati hauna muongozo?

    Sasa hivi nikisema TZhiphop.com itakuwa na magazine in 2-3 years na shughuli nyingine lukuki za kijamii wengi watanicheka. Watu waliibeza VFM wakati inaanzishwa… Lakini wanaojua kinachotokea nyuma ya pazia hawacheki.

    Mzee, siko choka mbaya wala nini. Nina nguvu unaweza ukasema I am possessed! Yaani hapa naombea mtikisiko fulani utokee… siku moja iwe na masaa kama 32 hivi ili niweze kusukuma mambo.

    Napenda kurudia: tunajua tunachofanya; na hicho ni kuwang’ang’ania nyie hapo viongozi wa leo na kesho. Tunajua wanaochoma wezi moto hawaji kusoma makala hapa. Ila nina uhakika kuna wabunge sio chini ya watano wanaosoma makala na maoni yetu. And that’s a fact, mzee…

  3. Ujue mimi mwanzo nilikuwa nasoma makala zenu then natoa mchango na kuishia hapo. Ila baada ya muda, na kuona kwa jinsi gani hali ilivyokuwa mbaya, I told myself I had to do something. Manake tunajua hali ni mbaya, ila hatukujua ni kiasi hiki. Inatisha kwa kweli. Kwahiyo vijanaFM ni moja ya sababu ya kuanzisha Ifoza Foundation.

    Mimi nadhani tunao akina Socrates wetu (Ulimwengu…) ila watu hawataki kusikiliza. Majuto mjukuu, ila naomba Mungu mambo yasije haribika tukashindwa kurekebisha.

    Endeleeni na kazi yenu nzuri. I am sure some of your readers will be inspired. Makala zitawahimiza wajiunge kwenye vita la kuiokomboa inchi yetu. Please continue holding us accountable ili tufike tunakokwenda.

  4. Kama nilivyosema hapo juu, Paul, kila mtu mmoja mmoja ana sehemu yake muhimu kwenye mambo yanayoendelea nchini. Sasa wengine wanakaa kitako pembeni na kusubiri makala za Jenerali, Kiranga, Bahati na Mwanakijiji. Wanabofya “like” kwenye facebook halafu wanaishia hapo.

    Wengine hawataki hata kutoa maoni yao ili watu wazipe hoja na fikra zao changamoto. (Juzi juzi hapa nimejua undani wa tofauti ya Quran na Hadith. Ningejua wapi hayo kama Hyperkei asingechangia? Ingeweza kunichukua miaka kibao.)

    Kila la heri mzee na Ifoza Foundation! Kuna projects nyingi mno zimezaliwa hapa kwenye miezi sita iliyopita — zile kubwa bado zinafanyiwa kazi. Usiwe na wasiwasi, hatupangi kuingia msituni!

    Kilichobakia ni kujaribu kuwalazimisha vijana wa Tanzania kufikiria miaka 10-30 mbele… hapo tabia lazima zibadilike tu. Ila kama hawataki, basi najua zoezi hili litafaulu pale mtoto wangu atakapokuja kusoma mawazo ya “dingi”. Sina wasiwasi wala ‘beef’ na hawa “Mbwa wa Pavlov”… Nikikaa ndani, nikajifungia na kusoma vitabu vyangu, hakuna atakayeathirika. Bahati mbaya au nzuri, hatuchoki kujaribu hata kwa mtu mmoja tu.

  5. George Bernard Shaw once said: The reasonable man adapts himself to the world, while the unreasonable man adapts the world to himself. Progress, therefore, lies in the actions of the unreasonable man.

    Of course, we can debate the meaning of “reason”. But SN has a point: Long-lasting change has never been easy. Indeed, most change hurts.

    The question then becomes: Are we willing to make a sustainable change in the way Tanzanians learn about their country and her people, or are we willing to take anything that is conventionally given to us?

    Vijana FM was built on the assumption that things need to change, especially with regards to how young citizens engage with media, education and entrepreneurship. And things need to change not just today, but for the long run – 2040 and beyond. This was an assumption, yani we took this as is, with no questions, when we came together to do this.

    So Bata, it’s difficult for me to imagine us working any other way. We don’t force anyone to read this blog. We deliberately bring up things that people don’t talk about, and try to facilitate constructive debates. We assume that if we don’t, things will not change, and that’s not something many of us here at Vijana FM are willing to accept. And in two years, we’ve learned – and continue to learn – that we’re onto something, and we need to keep going.

    If not now, when? If not us, who?

  6. @SN.
    Mie naona wana blog ya vijana mnajitahidi, wachangaiaji mada ni lazima wanaongezeka siku baada ya siku, ukichukulia hapa Tz mambo ya nishati na uunganishaji kwenye mtandao bado unasumbua.

    Ni kweli usemavyo, inabidi vijana tujue kubweka kwenye uhalifu gani na hatimaye kung’ata kama uhalifu huo unastahili, ila meno tunayo? Wengine wanaweza kubisha.

    Kutokuangalia na kupima matendo yetu, kwa ajili ya sasa au siku zijazo, labda ni sababu tumerithi kutoka kwa wazazi wetu au labda ni elimu na kukataa kutumia akili tulizozaliwa nazo! Tumeshuhudia vijana wenzetu wakiingia kwenye mtandao na post za kueleweka, za kuweza kuleta maendeleo na mabadiliko, lakini wakapotelea humo, kwa kisingizio cha kutokuwa na meno na hatimaye kucheza ngoma iliyopo! Watu wengine wenye “ambitions” hudai “sky is not the limit” kwa maana there is no limit to what we can do, hasa sisi vijana wa ki-Tz, je, sisi vijana wa Bongo hatujiamini? Kwanini basi hatushiriki ipasavyo katika kuleta maendeleo ya Taifa letu kwa namna tunayoijua?

    Endelea kuleta mada SN, tuko pamoja, tutajongea mdogo mdogo mpaka tutajaa. Ila mwamko kwa wenzetu utaletwa na mifumo mizuri ya miundo mbinu, labda na mie nachamesha tu…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend