Bwana Ametoa, Binadamu Akatwaa

Najua Ikulu siwezi fika, basi naomba umeme japo kwa dakika,
Napangilia majonzi chini ya maneno mia, labda hii twitter itawafikia,

 

Boti ya MV Ukimwi, bado inazamisha kwa wingi,
Kondom ndio maboya, lakini zipo chache melini,
Moyo watapatapa, ndani ya bahari ya umasikini,
Napiga kelele kuomba, lakini matumaini ghafla gizani.

 

Lakini Mungu hamtupi mja, kwani nasikia waokozi,
Mtumbwi unakaribia, lakini waokoaji ndio mafisadi,
Kimya sala najisalia, kwani mfuko hauna hata sumni,
Je tutaokolewa nafikiri, au mapapa ndio watalishwa sisi?

 

Rambirambi mwachangia, naomba wafiwa changa kutotiliwa,
Wanasema boti ilizidiwa, kama uhalisi wa moyo wa Mtanzania ,
Haikuwa meli ya abiria, lakini wengi tuligombania,
Wao na yao mashangingi, sisi na yetu majeneza yanayoelea.

 

Mbona leo kwenye kina nimefia, ndio kila mtu analia,
Jana pale niliponusurukia, hakuna aliyeonyesha nia,
Pamoja mauti yalikaribia, lakini hilo halikupalilia njia,
Hivyo kama yesu nakuhubiria, hapana mimi kunililia,
Badili majonzi kuwa fikra, kesho hapa maafani usije fikia.

 

Futa chirizi lako la chozi, kwani langu lilishafutwa na mawimbi,
Usinitazame machoni, yangu samaki walishaniibia,
Tuagane tu kimya kimya, kwani kauli yangu ilishasitishwa,
Mungu alikuwa bado na mengi ya kunipa, ni uzembe wenu ndio ulionikatishia.

 

Previous ArticleNext Article
Bahati was born and raised in Tanzania, and then moved to California to pursue his college education. He graduated in 2008 with a Bachelor’s Degree in Political Science and a minor in Sociology. Bahati expects to be doing his Masters in African Studies in the near future. He is currently working on starting a t-shirt business and a possible publication of some of his writings. One thing that Bahati cannot live without is music, specifically Hip Hop & Bongoflava which he argues are both the voice of the youth today, and is excited to look into how Bongoflava can be a source of further entrepreneurship among the youth in Tanzania. Bahati believes that Bongoflava can help to reduce poverty in Tanzania, as can a more collective effort among key players.

This post has 1 Comment

1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Send this to a friend