Kutokana na juhudi za wenzetu, nadhani leo idadi ya watembeleaji kutoka Dar es Salaam (hasa UDSM) imeongezeka zaidi ya maradufu!
Kwahiyo, napenda kuchukukua fursa hii kuwakaribisha (wageni na wenyeji): Karibuni kwenye tovuti yenu ya Vijana FM!
Ukiacha filamu fupi zinazotoa mafunzo mbalimbali kupitia hadithi na mahojiano (ya kitaaluma, burudani, shughuli za kijamii n.k.), kuna kurasa ambazo itakuwa jambo la busara mkiperuzi; ukiona kitu ambacho kitamfaa mwenzako, usikalie taarifa, bali jaribu kumtumia.
Kuna kurasa zifuatazo:
- Resources – Education
- Funding for organisations
- Technical assistance
- Orodha ya tovuti zenye taarifa mbalimbali
Pia, tumepata kuwa na makala zilizozua mijadala mizuri:
- No mdahalo, no vote
- Vijana wa Tanzania tuamke!
- Ze Utamu arudi kuwapangusa
- Tukemee ufedhuli
- Five questions with Natasha Shivji
- Mifumo ya Elimu Tanzania
- Education for self-reliance
- KwaWote Inc.
- China in Tanzania n.k.
Mijadala niliyoitaja hapo juu inaweza ikafufuliwa (kwa kuisogeza mbele) kama tukiona watu wanaendelea kutoa maoni!
Msisite kuwasiliana nasi au kutuma makala — tuna timu ya wahariri wa Kiswahili na Kiingereza (samahani sana kwa wale wanaopenda kujadili mambo kwa Kichagga, Kipare, Kihaya, Kisukuma…). Pia, unaweza kututumia maoni kupendekeza vitu gani kwenye tovuti viboreshwe.
Shukrani.
SN, big ups for your work. tovuti wa vijana fm safi zaidi.
Shukrani Jack D kwa kuja hapa mara kwa mara! Tunajua tukiweka makala hapa, watu wafuatao lazima wataipitia (na mara nyingi wataacha maoni): Jack D, Nionavyo, Subi, Vin, SL, Mzee wa Changamoto, Bata, Bihemo, Dr. Mallaba… orodha ni ndefu, lakini hayo majina ninayaona mara nyingi.
Pia itakuwa si busara kutowashukuru wale waliokubali “kuhojiwa”; na kubadilishana taarifa na ujuzi (kwenye masuala ya kutafuta vyuo, taaluma n.k.).
Kwa nilivyopitia, if kweli vjana tutaamka nchi itaendelea.
Nafurai sana kwa wale wa2 mnao22mia hizi ambazo zip juu ya ku2elimisha vijana na ku2fanya 2fikilie mbali kupitia maisha yetu yapoje au yatakuwaje huko mbele (this time 2morro ) kwa kweli natoa pongezi zangu za dhati kwa wale wote mnao tuamsha kw.mf. ile ishu iliyopita ya jitambue kipaji chako nikweli jama 2jalibu ku2mia muda mwingi kwa kufikiri kubuni na sio kwa kufikiri eti unakaa na wenzako mnadai eti Diamond sijui atatoalini wimbo mpya jiangalie nawewe pia .